Pre GE2025 Kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa tiketi ya CCM: Dkt Mwinyi kuwania Urais wa Muungano?

Pre GE2025 Kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa tiketi ya CCM: Dkt Mwinyi kuwania Urais wa Muungano?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Angalizo kwa Wanabodi na Mode

Bandiko hili ni C&P kutoka kwa mwana JF fulani.
Kwasababu mwandishi ni member wetu humu na humu hajaileta, naomba ikitokea ameileta humu, then futa hili bandiko langu.

Nime C&P kwasababu mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo kuandika humu kuwa mgombea urais wa CCM kwa uchaguzi wa 2025 could be Dr. Hussein Mwinyi, kupitia bandiko hili Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Hivyo hoja kama hii inapotolewa na mwajeiefu mwenzetu, mwandamizi kama huyu, hivyo nimejikuta ni muhimu kuisambaza.

Paskali.

(Mwanzo wa kunukuu Barua ya...)

Kwa kiasi kikubwa, siasa za Tanzania zimejikita zaidi kwenye chaguzi, hususan uchaguzi mkuu. Kwamba vyama vya siasa hutumia muda mwingi kujiandaa na chaguzi kiasi kwamba kuna dhana kwamba haviwatumikii wananchi vya kutosha kutokana na hilo.

Lakini lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Na katika nchi za kidemokrasia, kushika dola kunawezekana kwa njia moja tu, yaani uchaguzi mkuu. Kwa mantiki hiyo, ni sahihi kwa vyama vya siasa kujipanga vema kwa ajili ya chaguzi.

Na kwa chama tawala, kisipofanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya chaguzi zijazo, nafasi yake kama chama kinachoshika dola inakuwa hatarini.

Ni katika mazingira hayo ndio maana kumekuwa na maongezi mengi kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 japo bado miaka miwili hivi kabla ya uchaguzi huo. Na japo kuna chaguzi za serikali za mitaa mwakani, maongezi mengi ni kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Taarifa za kiintelijensia zinaeleza kwamba kuna jitihada zinafanyika huko Zanzibar kumwezesha Dkt Hussein Mwinyi kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano mwaka 2025.

Si tayari CCM “ina mgombea wake” 2025?
Naam. kwa mujibu wa utaratibu usio rasmi huko CCM, rais aliyepo madarakani anakuwa automatically mgombea pekee wa urais mwaka katika uchaguzi utakaomuingiza awamu ya pili ya urais wake.

Ilikuwa hivyo kwa Mkapa mwaka 2000, Jk 2010 na Magufuli 2020. Na inatarajiwa iwe hivyo kwa Mama Samia 2025.

Hadi wakati makala hii inaandikwa haijafahamika rasmi kwanini kuna mpango huo amba sio tu utapelekea “kuukoroga utaratibu huo usio rasmi wa Rais aliyepo madarakani kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo ili akamilishe ngwe zote mbili” bali pia utakuwa upinzani baina ya wanasiasa wawili kutoka Zanzibar.

Maandalizi yameanza
Taarifa zinaeleza kwamba tangu Zanzibar ijiunge na Tanganyika mwaka 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna kipindi ambapo upande huo wa Muungano umepokea fedha nyingi kutoka serikali ya Muungano kama kipindi hiki cha utawala wa Mama Samia.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa sehemu ya fedha hizo zimekuwa zikitumiwa na wanamkakati wa mpango huo wa kumwezesha Dkt Mwinyi kuwa mgombea mwaka 2025.

Licha ya ukweli kuwa maandalizi ya uchaguzi wowote hule huhitaji fedha za kutosha, yaaminika kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 utatawaliwa na matumizi makubwa ya fedha hasa kutokana na ukweli kwamba wanasiasa wengi wamepoteza mvuto machoni mwa wananchi na njia pekee ya “kupendeka” ni kumwaga fedha.

Mama Samia anawarahisishia kazi wapinzani wake ikiwa ni pamoja na mwanasiasa huyo wa Zanzibar
Kuna matukio mawili makubwa ambayo yanatarajiwa “kumsumbua” Mama Samia kati ya sasa na uchaguzi mwaka 2025. La kwanza ni suala la mkataba wa bandari ambalo japo “kwa nje ya CCM” linaonekana kama lilikuwa lina mwafaka miongoni mwa wana-CCM, ukweli ni kwamba sio tu lilizua mgawanyiko wakati wa mjadala bali pia limeacha makovu ambayo yanaweza “kukwanguliwa” pindi kampeni za urais zitaposhika kasi.

La pili ni hili la “Mama Samia kujichoma msumari mwenyewe” kwa kumteua Bashite kuwa katika mwenezi wa chama hicho, huku akifahamu fika kuwa kada huyo anachukiwa na wengi ndani na nje ya chama hicho.

Japo Mama Samia anatarajia kuwa Bashite atamsaidia kukabiliana na “wapinzani wake”, nguvu za kada huyo huko nyuma zilitegemea zaidi staili ya uongozi wa kibabe wa marehemu Magufuli, ambayo ni tofauti na satili ya uongozi wa Mama Samia, unless aamue kubadilika.

Hitimisho
Kuna msemo kuwa kwenye siasa, wiki moja ni sawa na uhai mzima (lifetime). Na kwa hakika, kati ya sasa Novemba 2023 hadi Oktoba 2025 ni takriban miaka miwili, na mengi yanaweza kutokea aidha kuimarisha dhamira ya mwanasiasa yeyote mwenye ndoto za kumpiku Mama Samia au urais wa Mama Samia ukaimarika zaidi kiasi kwamba yeyote mwenye ndoto za kum-challenge atakuwa anapoteza muda wake. (mwisho wa kunukuu)

Mwana if fulani.
C&P by Paskali
When you take two and two together unaweza ukajua what’s gonna happen 😅 !
Lakini ngoja Tusubiri tuone ! 🙏🙏
 
Huu Uzi umeletwa na watu wa propaganda kupima upepo. Inakuwaje Mwinyi ampinge Dada yake? Mwinyi ni Rais mzuri Sana ila siungi mkono njia anayotaka kuitumia. Amalizie Kwanza Zanzibar aje na kwa Muungano Kama afya inaruhusu.

Lingine bandiko hili halimhusu Mwinyi bali Kuna mwanasiasa antaka kumfanyia Shambulizi la kushutukiza Rais Samia. Yaonekana hali sio shwari chamani na serikalini.
Ngoja Tusubiri tuone 😅🙏
 
Kama kuna kitu kinanikera hi hichi cha urais wa kisultani. Hapa Tanganyika tuna wasomi wazuri tena maelfu kumpita huyo Rais Mwinyi wenu mimi nikiwa mmojawapo. Leo mnasema eti Mwinyi ndiye anayefaa kuwa Rais wa nchi hii 2025 siwaelewi kabisa. Labda aje mtu anieleze uzuri wa Mwinyi kuliko Watanganyika milioni sitini waliopo sasa
 
Waisiharsmu ndiyo wanaoleta udini mcheki mgagufuli ..mcheki nyerere ...kisha wacheki hao wengine ndiyo wanaleta hadi hijabu kwenye dhule za serikali ..wamegawa kifisadi bandari kisa nimuislamu muarabu
Unajua ni kwanini Nyerere aliviingilia Vita vya Biafra?

Anyway.. Udini ni Uduni wa Kifikra tusiichome hii Nchi yetu nzuri yenye Mito na Mabonde.

Kuna haja sasa nafasi ya Uraisi wa Jamhuri useme wazi kuwa ni lazima uwe Agnostic au Atheist.
 
Msichokijua ni kuwa kile kiti kina addiction sio rahisi kama mnavyodhani mama samia kampita mbali sana mwinyi kwenye uongozi kwa sasa.
Hawezi kubali hilo kila mtu anapenda kuacha legacy ya kipekee na ndio samia anachotaka kufanya kwa upande wake.

Ushauri kwa team Mwinyi kuna mambo sio ya ya kulazimisha na sio kila mtu ameandikiwa au ana haki ya kuwa rais wa jamhuri jifunzeni kwa kwa mhe. Lowasa na mkubali yapite..
Mama anaacha Legacy gani sasa?
 
Kwa hiyo hii nchi Raia wengine hawana haki yaani , watoto wa viongozi tu ndio wanatakiwa kupokezana uongozi !

Tena watoto wenyewe hawana uzalendo wowote ule , Wengine walikataa hata kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa kiburi tu , kwa vile Baba zao ni viongozi .

Poor Tanzania !
Tumpe mlevi wa konyagi mwenye ulafi wa madaraka..mwenyekiti wa milele.

Nah!mlamba asali hana kiasi..akawii kuwa dikteta wa nchi kma alivyo wa chama.
 
Unajua ni kwanini Nyerere aliviingilia Vita vya Biafra?

Anyway.. Udini ni Uduni wa Kifikra tusiichome hii Nchi yetu nzuri yenye Mito na Mabonde.

Kuna haja sasa nafasi ya Uraisi wa Jamhuri useme wazi kuwa ni lazima uwe Agnostic au Atheist.
Najua ...unajua kwa nini muamadi alitaka watu wahukumiane kwa haki siyo kwa kutizama dini gani ? Unajua kwanini nyerere alipinga waisrael japo yeye ni mkristo ? Unajua kwanini nyerere alijiunga na wazee wa kiislamu wa dar es salaam ambao walikuwa waislamu kwenye kupigania uhuru.je unajua kwanini nyerere alikataa pesa ya gadafi ili kuwagomboa waislamu wa libya walio tekwa kwenye vita vya uganda na kuwaachia bure bila ya kupokea hata senti ...usimfananisha nyerere na hizi takataka za kisiharamu zilizo kuja kuongoza baada yake
 
Back
Top Bottom