Kwanini SGR isikamilike wakati wanakusanya kodi ya Railway Development Levy.Viongozi wa CCM ndiyo walioua ilifanye biashara ya mafuta hata SGR haiendi popote
Nadhani kinachojadiliwa hapa ni kufa kwa kiwanda cha kusafisha mafuta!Kwanini SGR isikamilike wakati wanakusanya kodi ya Railway Development Levy.
Hii kodi inakwenda kufanya kazi gani??
Fikiria tu tumeshindwa kuzalisha mafuta ya alizeti, vijiti vya kuchokonolea meno, ngano, nguzo za umeme nk wakati ardhi ya kutoa raw materials ipo kubwa tu, nani anayehujumu uzalishaji wa malighafi nchiniChangamoto tuliyonayo hata lile wazo la kukifufua kiwanda hiki halipo kabisa!
Jifunze kusoma kila koment ukajua majibu ya coment nyingine yametokana na nini.Nadhani kinachojadiliwa hapa ni kufa kwa kiwanda cha kusafisha mafuta!
Mama Samia asione aibu kuwarudishia bure Agip kwa maslahi mapana ya uchumi wetu!Zambia wanacho hawakuua kilijengwa same time na chetu
Cost ya kukikarabati sio kujenga kiwanda kipya zinahitajika dola milioni 500 hawana wanahaha kutafuta private investors!!
Kuna biashara Serikali haiwezi fanya Haina pesa za hiyo biashara
Kiwanda cha Tipper waitaliano wa Agip ndio waliwekeza Serikali ikajifanya kutaifisha limewatokea kooni
Private sector capital ina raise capital markets za kimataifa.Miradi kama hiyo Serikali haiiwezi kutegemea ukusanye Kodi dola milioni 500 kwenye mauzo ya nje ya mazao kama ya korosho sijui pamba sio rahisi!!
Mwenye nguvu mpishe Serikali irudishe kwa Agip hicho kiwanda cha kusafisha mafuta Serikali haiwezi kuwa na mtaji wa kufufuka hicho kiwanda ni lofa
Muulize m/kiti wako wa chama Tawala Nani walifanya uasi huu wa kuiua TIPER.....Katika utawala wa Mwalimu Nyerere Tanzania tulikuwa na kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi ambacho kilikuwa kinazalisha petroli, dizeli mafuta ya taa, lami nk. Kwa hiyo nchi ilikuwa ikinunua mafuta ghafi kwa bei nafuu na kuyasafisha kwa gharama nafuu na kufanya bei ya mafuta kuwa nafuu kwa walaji.
Ulipoingia MZIMU wa ubinafsishaji kiwanda kikafa tukaanza kununua mafuta yaliyosafishwa. Hapa ndipo tulipopotea maboya! Sasa tunakula jeuri yetu kwa kukomolewa kwa bei ghali ya mafuta. Laiti kingekuwepo kiwanda chetu kile tusingeumia kiasi hiki!
Jaribu kutofautisha kiwanda cha TIPER kilichokuwa kinafanya kazi na SGR ambayo bado inajengwa kwa mkopo!Jifunze kusoma kila koment ukajua majibu ya coment nyingine yametokana na nini.
Viwanda vilikuwa vimeshauwawa na sisi wenyewe pamoja na NMC na RTCUlipoingia MZIMU wa ubinafsishaji kiwanda kikafa tukaanza kununua mafuta yaliyosafishwa.
Ni kweli lakini kuna vitu nyeti kwa ustawi wa Taifa vinapaswa kudumishwa vikiwemo viwanda vya nishati!Viwanda vilikuwa vimeshauwawa na sisi wenyewe pamoja na NMC na RTC
ubinafsishaji ni sera nzuri,tumechoka na ukomunisti wenye laana.
Kwanini SGR isikamilike wakati wanakusanya kodi ya Railway Development Levy.
Hii kodi inakwenda kufanya kazi gani??
Serikali isifanye biashara itafeli vibaya,yenyewe ichukue kodi yake stahiki tu.Ni kweli lakini kuna vitu nyeti kwa ustawi wa Taifa vinapaswa kudumishwa vikiwemo viwanda vya nishati!
Alikipiga bomu au.Magufuli alikiua
Sawa lakini hivi sasa hakuna anayeongelea kuanzishwa kwa kiwanda cha kusafisha mafuta! Kinachojadiliwa ni kutafuta soko la bei nafuu kununua mafuta!Serikali isifanye biashara itafeli vibaya,yenyewe ichukue kodi yake stahiki tu.
Tumeshuhudia jinsi Viwanda vilivyouwawa na vingi Mwalimu aliwazulumu Wakoloni na Waasia.