Kiongozi aliyehujumu na kuua kiwanda cha TIPER ni wa ovyo kuwahi kutokea Tanzania

Kiongozi aliyehujumu na kuua kiwanda cha TIPER ni wa ovyo kuwahi kutokea Tanzania

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Katika utawala wa Mwalimu Nyerere Tanzania tulikuwa na kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi ambacho kilikuwa kinazalisha petroli, dizeli mafuta ya taa, lami nk.

Kwa hiyo nchi ilikuwa ikinunua mafuta ghafi kwa bei nafuu na kuyasafisha kwa gharama nafuu na kufanya bei ya mafuta kuwa nafuu kwa walaji.

Ulipoingia MZIMU wa ubinafsishaji kiwanda kikafa tukaanza kununua mafuta yaliyosafishwa. Hapa ndipo tulipopotea maboya!

Sasa tunakula jeuri yetu kwa kukomolewa kwa bei ghali ya mafuta. Laiti kingekuwepo kiwanda chetu kile tusingeumia kiasi hiki!
 
Zambia wanacho hawakuua kilijengwa same time na chetu

Cost ya kukikarabati sio kujenga kiwanda kipya zinahitajika dola milioni 500 hawana wanahaha kutafuta private investors!!

Kuna biashara Serikali haiwezi fanya Haina pesa za hiyo biashara

Kiwanda cha Tipper waitaliano wa Agip ndio waliwekeza Serikali ikajifanya kutaifisha limewatokea kooni

Private sector capital ina raise capital markets za kimataifa.Miradi kama hiyo Serikali haiiwezi kutegemea ukusanye Kodi dola milioni 500 kwenye mauzo ya nje ya mazao kama ya korosho sijui pamba sio rahisi!!

Mwenye nguvu mpishe Serikali irudishe kwa Agip hicho kiwanda cha kusafisha mafuta Serikali haiwezi kuwa na mtaji wa kufufua hicho kiwanda ni lofa
 
Zambia wanacho hawakuua kilijengwa same time na chetu

Cost ya kukikarabati sio kujenga kiwanda kipya zinahitajika dola milioni 500 hawana wanahaha kutafuta private investors!!

Kuna biashara Serikali haiwezi fanya Haina pesa za hiyo biashara

Kiwanda cha Tipper waitaliano wa Agip ndio waliwekeza Serikali ikajifanya kutaifisha limewatokea kooni

Private sector capital ina raise capital markets za kimataifa.Miradi kama hiyo Serikali haiiwezi kutegemea ukusanye Kodi dola milioni 500 kwenye mauzo ya nje ya mazao kama ya korosho sijui pamba sio rahisi!!

Mwenye nguvu mpishe Serikali irudishe kwa Agip hicho kiwanda cha kusafisha mafuta Serikali haiwezi kuwa na mtaji wa kufufuka hicho kiwanda ni lofa
Mama Samia asione aibu kuwarudishia bure Agip kwa maslahi mapana ya uchumi wetu!
 
Katika utawala wa Mwalimu Nyerere Tanzania tulikuwa na kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi ambacho kilikuwa kinazalisha petroli, dizeli mafuta ya taa, lami nk. Kwa hiyo nchi ilikuwa ikinunua mafuta ghafi kwa bei nafuu na kuyasafisha kwa gharama nafuu na kufanya bei ya mafuta kuwa nafuu kwa walaji.

Ulipoingia MZIMU wa ubinafsishaji kiwanda kikafa tukaanza kununua mafuta yaliyosafishwa. Hapa ndipo tulipopotea maboya! Sasa tunakula jeuri yetu kwa kukomolewa kwa bei ghali ya mafuta. Laiti kingekuwepo kiwanda chetu kile tusingeumia kiasi hiki!
Muulize m/kiti wako wa chama Tawala Nani walifanya uasi huu wa kuiua TIPER.....
 
Serikali isifanye biashara itafeli vibaya,yenyewe ichukue kodi yake stahiki tu.

Tumeshuhudia jinsi Viwanda vilivyouwawa na vingi Mwalimu aliwazulumu Wakoloni na Waasia.
Sawa lakini hivi sasa hakuna anayeongelea kuanzishwa kwa kiwanda cha kusafisha mafuta! Kinachojadiliwa ni kutafuta soko la bei nafuu kununua mafuta!
 
Back
Top Bottom