Kiongozi aliyehujumu na kuua kiwanda cha TIPER ni wa ovyo kuwahi kutokea Tanzania

Kiongozi aliyehujumu na kuua kiwanda cha TIPER ni wa ovyo kuwahi kutokea Tanzania

Hivi kufufua ATCL na kununua mandege tena kama wanavyo sema wananunua cash na kujenge REFINERY ya uwezo mkubwa hapo lipi LINGEKUWA jambo bora na lenye TIJA KUBWA kwa TAIFA?
Nchi hii hakuna national interests... Kila rais akija anaanza na yake..

Takataka sana nchi hii!!

SGR ATCL JNHEPP vyote vinaenda kufa kibudu kmmkee..

KATIBA ni ya muhimu sana nchi hii!
 
Nachojua tu hiki kiwanda PSRC na serikali walileta ujanja wao wa kutaka kudhulumu malipo yao. Wakatoa tamko kali la kukichoma moto na kuiunguza Dar es Salaam yote. FFU walitumwa kwenda kutuliza vurugu walivyosikia hiyo kauli wenyewe waliondoka katika hilo tukio na serikali ikawalipa. CCM ndio muuaji mkubwa wa haya mashirika kwa kushirikiana na mzee wa Lupaso.
 
Mama Samia asione aibu kuwarudishia bure Agip kwa maslahi mapana ya uchumi wetu!
Mimi na wewe hapa tumeelewa umiliki na umuhimu wa kiwanda hiki na kwa nini kirudishwe kwa mwekezaji hata bure

Siku mama atapofanya hivyo, litaibuka kundi kubwa la kumpiga vita kuwa "anauza nchi", "anagawa Mali za serikali kwa mabeberu", "anagawia bure wapiga dili"

Hao ndio watanzania.. you can never be good enough to them. I feel sorry for the president kwa kweli!!

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mimi na wewe hapa tumeelewa umiliki na umuhimu wa kiwanda hiki na kwa nini kirudishwe kwa mwekezaji hata bure

Siku mama atapofanya hivyo, litaibuka kundi kubwa la kumpiga vita kuwa "anauza nchi", "anagawa Mali za serikali kwa mabeberu", "anagawia bure wapiga dili"

Hao ndio watanzania.. you can never be good enough to them. I feel sorry for the president kwa kweli!!

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Ili kupunguza maneno apeleke hoja bungeni ijadiliwe.
 
Katika utawala wa Mwalimu Nyerere Tanzania tulikuwa na kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi ambacho kilikuwa kinazalisha petroli, dizeli mafuta ya taa, lami nk.

Kwa hiyo nchi ilikuwa ikinunua mafuta ghafi kwa bei nafuu na kuyasafisha kwa gharama nafuu na kufanya bei ya mafuta kuwa nafuu kwa walaji.

Ulipoingia MZIMU wa ubinafsishaji kiwanda kikafa tukaanza kununua mafuta yaliyosafishwa. Hapa ndipo tulipopotea maboya!

Sasa tunakula jeuri yetu kwa kukomolewa kwa bei ghali ya mafuta. Laiti kingekuwepo kiwanda chetu kile tusingeumia kiasi hiki!
Serikali imesema itafufua Tipper
 
Gharama zote zinazolikabili Taifa letu leo na kupelekea ugumu wa maisha haya tuliyonayo, zinatokana na UBINAFSISHAJI, hakuna kingine

Unaamin tungebaki na ujamaa mambo yangekuwa mazuri?
 
Havikuwa vimekufa completely. Kwa mfano Bora shoes, TBL na Kilombero sugar vilikuwa vimekufa? Viwanda vingine vilikufa baada ya privatisation kuingia. Kwa mfano Urafiki ilikumbwa na matatizo baada ya ubinafsishaji kuingia. Watu binafsi waliruhusiwa kununua pamba hivyo wao wakashindwa kununua hivyo wakakosa mali ghafi. so no production. Urafiki ilikuwa inaajiri wafanyakazi nadhani 5000 kipindi kile. Kuna viwanda vitatu pale- spinning, weaving na finishing ya kutengeneza sasa khanga na vitenge na mashuka. Unaachaje kiwanda kama kile kife!!!! Pia viwanda vingi vilipata shida ya ukosefu wa mali ghafi kwa sababu ya kukosa hela za kigeni. Wakati huo Benki kuu ndiyo ilikuwa inatoa allocation ya forex na kulikuwa na scarcity ya forex. Vilishindwa kununua spares nk nk. Matatizo ni mengi na yalikuwa solvable kama serikali ingekuwa na nia. Viwanda vilikuwa na matatizo mengi na mwenye mali alikuwa hajali. Nikiandika hapa kila kitu nafasi haitoshi. Hii kusema vilikuwa vimekufa ni siasa tu ili kujustify privatisation. Nilifanya kazi kiwandani najua ninachoongea na ni mhanga. Ubadhirifu kweli ulikuwepo lakini siyo ulioua viwanda. bad policy. Kwani privatisation ni kuja kuchukua kiwanda kwa bei chee!!!! Mbona hakuna hata kiwanda kimoja kilichoanzishwa cha maana except cha Dangote!!!!

Mfano mwingine, kulikuwa na shirika la kitalii Tanzania Tourist Corporation lilikuwa lifanya wonders. Liliuliwa kisiasa tu na hoteli zote zikabinfsishwa zilizokuwa mali ya TTC. Mkuu siasa mbaya sana watu wakitaka kujustify mambo yao. Yaani hilo shirika lingekuwepo mama asingekuwa na haja ya kuwa rambo.

Kama hio ndo sababu ya URAFIKI kufa basi nasema kife tu
Hatuwez tesa wakulima wa pamba 500k ili tu URAFIKI wanunue pamba kwa bei yao ndogo
 
Wewe ndio wale wale,mimi nilikuwa Agip enzi hizo.
1.Mitambo ya Tipper ilikuwa imechoka wala haitoshelezi mahitaji yetu,World Bank au IMF akagundua it was cheaper to import white product kuliko mafuta kiduchu yaliozalishwa na Tipper. Running cost zilikuwa kubwa mno.Tipper ikageuka liability not asset na matumizi mabaya ya fedha za mikopo yakagunduliwa.
Mataliani walijua fika Tipper ni mzuka wa kufa wakati wowote.Walipoona World Bank au IMF imeikatalia kufadhili wizi wao wakauza hisa zao chapu chapu kwa kampuni ya uswiss wakasepa,na Tipper ikaacha kuzalisha mafuta.

Kumbe mambo yalikuwa yametufika pabaya
 
Unaamin tungebaki na ujamaa mambo yangekuwa mazuri?
Hakuna uhusiano kati ya kubinafsisha mali ya umma na ujamaa! Hata serikali za Ulaya na Marekani zinamiliki baadhi ya makampuni nyeti.
 
Mambo mengine ni ya kujifurahisha tu.

TIPER ilikuwa na uwezo wa kuchakata tone laki sita ya mafuta ghafi kwa mwaka.

Ikaongezewa uwezo mpaka tones laki 7.5 ya kuchakata mafuta ghafi kabla ya kuacha uzalishaji.

Tonnes laki 7.5 ya mafuta ghafi kwa mwaka ni sawa litres million 680 za crude oil. Kwenye crude of barrel kuna litre 153[emoji116]na unapata product zifuatazo.

View attachment 2211911

Hizo ni kwa refineries za kisasa ambazo zinaweza chakata mafuta yenye API gravity kubwa. Kwa technology ya TIPER yield percentage is even lower; hata ulaya refiniries zilizokuwa na technology ya miaka ya 1960’s nyingi zishafungwa not only zinauwezo mdogo wa kuchuja crude oil but also very unfriendly to the environment.

Tanzania ya leo inamahitaji ya mafuta takribani litre billion 3.5 mpaka billion 4, TIPER mpaka inafungwa ilikuwa na uwezo wa kuzalisha million 545-680 litres at maximum (it could be lower given its technology).

That’s is to say kusema TIPER ingekuwa mwarobani wa tatizo la mafuta is simply short sighted uwezo wa TIPER wa kuzalisha na mahitaji ya nchi ni drop in the ocean.

Besides kinachoendelea kwenye soko la mafuta on political side of things it has nothing to do with refineries. Na kujenga refiniries kama bwala la umeme na reli tu mshike mshike wake sio mdogo; kweli tuongelee mambo ya Oil refiniries investment zenye uwezo wa kuchakata mafuta ya Tanzania tu.

Kuna wakati embu tuwe serious on what we can do and what we can’t kwa mapato yetu ya sasa.

Sometimes akili zetu zinatutosha wenyewe; unahitaji TIPER iongeze uwezo wake mara saba ili kuweza kuhudumia mahitaji ya Tanzania. Sasa tunajua gharama ya size hiyo ya refinery kweli au tunajifurahisha.
Mawazo mgando ,!
Kwa hiyo hatukuwa na akili za ku upgrade TIPER kuwa na uzalishaji wa kisasa !!
Utetezi wa hovyo Kabisa mpyuuuuu
 
Kumbe mambo yalikuwa yametufika pabaya
Yaani shida ilianzia kwa wawakilirishi wa Serikali yetu kwenye bodi.
Hawakuwa na uchungu wakanunuliwa kama mafungu ya ndizi.
Taliano aliwaliwatafuna kama ndege atafunavyo kumbikumbi pale mkutano ulipokuwa ukifanyika Italy wakauzwa kwa vibahasha za vijisawadi na vipesa maumivu uchwala.Wakauza umma wa Tanzania kuliko Tip Tip.
 
Na TUSUBIRI MAFUTA GHAFI TOKA UGANDA YAPAKILIWE TANGA YAPELEKWE NJE NDIO TUYANUNUE. TUWAKUMBUSHE WABUNGE JUU YA HILI NI MUHIMU SANA
 
Unaamin tungebaki na ujamaa mambo yangekuwa mazuri?
Kwenye miaka ya mwishoni mwa 80 kuelekea 90 wakati tunasoma Sekondari, nakumbuka watu waliokuwa wanasoma somo la History, kama sikoseai walikuwa mara kwa mara wanakuwa confronted na swali moja kwenye mitihani ya NECTA, lililokuwa likisema ".................................. (dash dash dash)... halafu linaendlea linasema

"....TODAY, TANZANIA IS NEITHER A SOCIALIST NOR A CAPITALIST COUNTRY, DISCUSS!

Kwa hiyo ujamaa tulishauacha siku nyingi huko nyuma kabla hata ya UBINAFSISHAJI; possibly baada tu ya kipindi cha Mwl. Nyerere. Kwa hiyo UBINAFSISHAJI; ilikuwa ni njia tu ya KUHALALISHA kuwanyang'anya Watanzania mali zao wao wenyewe wakiwa wanaona kwa macho yao mawili
 
Na TUSUBIRI MAFUTA GHAFI TOKA UGANDA YAPAKILIWE TANGA YAPELEKWE NJE NDIO TUYANUNUE. TUWAKUMBUSHE WABUNGE JUU YA HILI NI MUHIMU SANA
Viongozi wetu wamelala usingizi wa pono!

Hoja ya kujenga kiwanda cha kuchakata mafuta ingejegwa sasa ili ujenzi wa bomba la mafuta uende sambamba. Soko lipo wazi katika nchi zote za Afrika ya mashariki na kati!
 
Usiihusishe CCM, hata CCM alikuwa anaipeleka kuzikwa bwana yule.

Umesahau alivyoisambararatisha chadema?
Kitathmini inaonekana CCM ya magufuli ndio ilikuwa na mvuto mtaani yani kijani na njano ilikuwa inaleta matumaini kwa wananchi.
 
Zambia wanacho hawakuua kilijengwa same time na chetu

Cost ya kukikarabati sio kujenga kiwanda kipya zinahitajika dola milioni 500 hawana wanahaha kutafuta private investors!!

Kuna biashara Serikali haiwezi fanya Haina pesa za hiyo biashara

Kiwanda cha Tipper waitaliano wa Agip ndio waliwekeza Serikali ikajifanya kutaifisha limewatokea kooni

Private sector capital ina raise capital markets za kimataifa.Miradi kama hiyo Serikali haiiwezi kutegemea ukusanye Kodi dola milioni 500 kwenye mauzo ya nje ya mazao kama ya korosho sijui pamba sio rahisi!!

Mwenye nguvu mpishe Serikali irudishe kwa Agip hicho kiwanda cha kusafisha mafuta Serikali haiwezi kuwa na mtaji wa kufufua hicho kiwanda ni lofa
Kilichoharibika ni kitu gani?Kama Serikali haiwezi nani anaweza?huyo anayeweza amepata wapi fedha?
 
Back
Top Bottom