Nchi hii hakuna national interests... Kila rais akija anaanza na yake..Hivi kufufua ATCL na kununua mandege tena kama wanavyo sema wananunua cash na kujenge REFINERY ya uwezo mkubwa hapo lipi LINGEKUWA jambo bora na lenye TIJA KUBWA kwa TAIFA?
Mimi na wewe hapa tumeelewa umiliki na umuhimu wa kiwanda hiki na kwa nini kirudishwe kwa mwekezaji hata bureMama Samia asione aibu kuwarudishia bure Agip kwa maslahi mapana ya uchumi wetu!
Ili kupunguza maneno apeleke hoja bungeni ijadiliwe.Mimi na wewe hapa tumeelewa umiliki na umuhimu wa kiwanda hiki na kwa nini kirudishwe kwa mwekezaji hata bure
Siku mama atapofanya hivyo, litaibuka kundi kubwa la kumpiga vita kuwa "anauza nchi", "anagawa Mali za serikali kwa mabeberu", "anagawia bure wapiga dili"
Hao ndio watanzania.. you can never be good enough to them. I feel sorry for the president kwa kweli!!
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Serikali imesema itafufua TipperKatika utawala wa Mwalimu Nyerere Tanzania tulikuwa na kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi ambacho kilikuwa kinazalisha petroli, dizeli mafuta ya taa, lami nk.
Kwa hiyo nchi ilikuwa ikinunua mafuta ghafi kwa bei nafuu na kuyasafisha kwa gharama nafuu na kufanya bei ya mafuta kuwa nafuu kwa walaji.
Ulipoingia MZIMU wa ubinafsishaji kiwanda kikafa tukaanza kununua mafuta yaliyosafishwa. Hapa ndipo tulipopotea maboya!
Sasa tunakula jeuri yetu kwa kukomolewa kwa bei ghali ya mafuta. Laiti kingekuwepo kiwanda chetu kile tusingeumia kiasi hiki!
Gharama zote zinazolikabili Taifa letu leo na kupelekea ugumu wa maisha haya tuliyonayo, zinatokana na UBINAFSISHAJI, hakuna kingine
Havikuwa vimekufa completely. Kwa mfano Bora shoes, TBL na Kilombero sugar vilikuwa vimekufa? Viwanda vingine vilikufa baada ya privatisation kuingia. Kwa mfano Urafiki ilikumbwa na matatizo baada ya ubinafsishaji kuingia. Watu binafsi waliruhusiwa kununua pamba hivyo wao wakashindwa kununua hivyo wakakosa mali ghafi. so no production. Urafiki ilikuwa inaajiri wafanyakazi nadhani 5000 kipindi kile. Kuna viwanda vitatu pale- spinning, weaving na finishing ya kutengeneza sasa khanga na vitenge na mashuka. Unaachaje kiwanda kama kile kife!!!! Pia viwanda vingi vilipata shida ya ukosefu wa mali ghafi kwa sababu ya kukosa hela za kigeni. Wakati huo Benki kuu ndiyo ilikuwa inatoa allocation ya forex na kulikuwa na scarcity ya forex. Vilishindwa kununua spares nk nk. Matatizo ni mengi na yalikuwa solvable kama serikali ingekuwa na nia. Viwanda vilikuwa na matatizo mengi na mwenye mali alikuwa hajali. Nikiandika hapa kila kitu nafasi haitoshi. Hii kusema vilikuwa vimekufa ni siasa tu ili kujustify privatisation. Nilifanya kazi kiwandani najua ninachoongea na ni mhanga. Ubadhirifu kweli ulikuwepo lakini siyo ulioua viwanda. bad policy. Kwani privatisation ni kuja kuchukua kiwanda kwa bei chee!!!! Mbona hakuna hata kiwanda kimoja kilichoanzishwa cha maana except cha Dangote!!!!
Mfano mwingine, kulikuwa na shirika la kitalii Tanzania Tourist Corporation lilikuwa lifanya wonders. Liliuliwa kisiasa tu na hoteli zote zikabinfsishwa zilizokuwa mali ya TTC. Mkuu siasa mbaya sana watu wakitaka kujustify mambo yao. Yaani hilo shirika lingekuwepo mama asingekuwa na haja ya kuwa rambo.
Wewe ndio wale wale,mimi nilikuwa Agip enzi hizo.
1.Mitambo ya Tipper ilikuwa imechoka wala haitoshelezi mahitaji yetu,World Bank au IMF akagundua it was cheaper to import white product kuliko mafuta kiduchu yaliozalishwa na Tipper. Running cost zilikuwa kubwa mno.Tipper ikageuka liability not asset na matumizi mabaya ya fedha za mikopo yakagunduliwa.
Mataliani walijua fika Tipper ni mzuka wa kufa wakati wowote.Walipoona World Bank au IMF imeikatalia kufadhili wizi wao wakauza hisa zao chapu chapu kwa kampuni ya uswiss wakasepa,na Tipper ikaacha kuzalisha mafuta.
Kama siyo ccm basi wewe ni puppet wa ccm.Aliyekuambia kuwa mimi ccm ni nani? Au akili yako nyingi ndiyo imekudanganya hivyo?
Mzee wa Lupaso alikuwa mwenyekiti wa chama gani!Tipper ilijifia kipindi cha utawala wa mzee lupaso
Mawazo mgando ,!Mambo mengine ni ya kujifurahisha tu.
TIPER ilikuwa na uwezo wa kuchakata tone laki sita ya mafuta ghafi kwa mwaka.
Ikaongezewa uwezo mpaka tones laki 7.5 ya kuchakata mafuta ghafi kabla ya kuacha uzalishaji.
Tonnes laki 7.5 ya mafuta ghafi kwa mwaka ni sawa litres million 680 za crude oil. Kwenye crude of barrel kuna litre 153[emoji116]na unapata product zifuatazo.
View attachment 2211911
Hizo ni kwa refineries za kisasa ambazo zinaweza chakata mafuta yenye API gravity kubwa. Kwa technology ya TIPER yield percentage is even lower; hata ulaya refiniries zilizokuwa na technology ya miaka ya 1960’s nyingi zishafungwa not only zinauwezo mdogo wa kuchuja crude oil but also very unfriendly to the environment.
Tanzania ya leo inamahitaji ya mafuta takribani litre billion 3.5 mpaka billion 4, TIPER mpaka inafungwa ilikuwa na uwezo wa kuzalisha million 545-680 litres at maximum (it could be lower given its technology).
That’s is to say kusema TIPER ingekuwa mwarobani wa tatizo la mafuta is simply short sighted uwezo wa TIPER wa kuzalisha na mahitaji ya nchi ni drop in the ocean.
Besides kinachoendelea kwenye soko la mafuta on political side of things it has nothing to do with refineries. Na kujenga refiniries kama bwala la umeme na reli tu mshike mshike wake sio mdogo; kweli tuongelee mambo ya Oil refiniries investment zenye uwezo wa kuchakata mafuta ya Tanzania tu.
Kuna wakati embu tuwe serious on what we can do and what we can’t kwa mapato yetu ya sasa.
Sometimes akili zetu zinatutosha wenyewe; unahitaji TIPER iongeze uwezo wake mara saba ili kuweza kuhudumia mahitaji ya Tanzania. Sasa tunajua gharama ya size hiyo ya refinery kweli au tunajifurahisha.
Watanzania wanataka biashara zinazotoa faida haraka!Utasikia mtanzania fulani kauzi
Utasikia fudenge kanunua Tipper
Yaani shida ilianzia kwa wawakilirishi wa Serikali yetu kwenye bodi.Kumbe mambo yalikuwa yametufika pabaya
Kwenye miaka ya mwishoni mwa 80 kuelekea 90 wakati tunasoma Sekondari, nakumbuka watu waliokuwa wanasoma somo la History, kama sikoseai walikuwa mara kwa mara wanakuwa confronted na swali moja kwenye mitihani ya NECTA, lililokuwa likisema ".................................. (dash dash dash)... halafu linaendlea linasemaUnaamin tungebaki na ujamaa mambo yangekuwa mazuri?
Viongozi wetu wamelala usingizi wa pono!Na TUSUBIRI MAFUTA GHAFI TOKA UGANDA YAPAKILIWE TANGA YAPELEKWE NJE NDIO TUYANUNUE. TUWAKUMBUSHE WABUNGE JUU YA HILI NI MUHIMU SANA
Kitathmini inaonekana CCM ya magufuli ndio ilikuwa na mvuto mtaani yani kijani na njano ilikuwa inaleta matumaini kwa wananchi.Usiihusishe CCM, hata CCM alikuwa anaipeleka kuzikwa bwana yule.
Umesahau alivyoisambararatisha chadema?
Kilichoharibika ni kitu gani?Kama Serikali haiwezi nani anaweza?huyo anayeweza amepata wapi fedha?Zambia wanacho hawakuua kilijengwa same time na chetu
Cost ya kukikarabati sio kujenga kiwanda kipya zinahitajika dola milioni 500 hawana wanahaha kutafuta private investors!!
Kuna biashara Serikali haiwezi fanya Haina pesa za hiyo biashara
Kiwanda cha Tipper waitaliano wa Agip ndio waliwekeza Serikali ikajifanya kutaifisha limewatokea kooni
Private sector capital ina raise capital markets za kimataifa.Miradi kama hiyo Serikali haiiwezi kutegemea ukusanye Kodi dola milioni 500 kwenye mauzo ya nje ya mazao kama ya korosho sijui pamba sio rahisi!!
Mwenye nguvu mpishe Serikali irudishe kwa Agip hicho kiwanda cha kusafisha mafuta Serikali haiwezi kuwa na mtaji wa kufufua hicho kiwanda ni lofa