Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,129
- 7,321
Gharama zote zinazolikabili Taifa letu leo na kupelekea ugumu wa maisha haya tuliyonayo, zinatokana na UBINAFSISHAJI, hakuna kingineKatika utawala wa Mwalimu Nyerere Tanzania tulikuwa na kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi ambacho kilikuwa kinazalisha petroli, dizeli mafuta ya taa, lami nk. Kwa hiyo nchi ilikuwa ikinunua mafuta ghafi kwa bei nafuu na kuyasafisha kwa gharama nafuu na kufanya bei ya mafuta kuwa nafuu kwa walaji.
Ulipoingia MZIMU wa ubinafsishaji kiwanda kikafa tukaanza kununua mafuta yaliyosafishwa. Hapa ndipo tulipopotea maboya! Sasa tunakula jeuri yetu kwa kukomolewa kwa bei ghali ya mafuta. Laiti kingekuwepo kiwanda chetu kile tusingeumia kiasi hiki!