Kiongozi asiye mzalendo na anayejali tumbo lake huwa hana huruma na raia masikini na wasio na uwezo

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Dunia nzima kiongozi wa namna hii huwa hana huruma.

Hawezi kujali kama wananchi wanahangaika juu ya ugumu wa maisha na ajira.

Atahakikisha wanakamuliwa kodi za kila namna bila ya huruma.

Wananchi huwa wananug'unika kama ilivyo kwa sasa Tanzania yetu. Ni manug'uniko kwa kwenda mbele.
 
Mtaje jina na nitajie vyanzo vikuu vitatu tu vya mapato ya nchi ili iweze kupiga hatua ya kimaendeleo...
 
Dunia nzima kiongozi wa namna hii huwa hana huruma.

Hawezi kujali kama wananchi wanahangaika juu ya ugumu wa maisha na ajira.

Atahakikisha wanakamuliwa kodi za kila namna bila ya huruma.

Wananchi huwa wananug'unika kama ilivyo kwa sasa Tanzania yetu. Ni manug'uniko kwa kwenda mbele.
Ni wapumbavu, wajinga na washenzi wanao endelea kunung'unika huku huyo kiongozi akila mema ya nchi kama hampendi na hamtuki si mtoe ?
 
Acha chuki zako zisizo na msingi Wala ukweli kwa serikali hii ya mh Rais wetu mpendwa, Serikali hii Ni moja ya serikali inayoendeshwa katika misingi ya kutanguliza maslahi ya Taifa, inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa mwananchi anahudumiwa vizuri, Anapata na kusogezewa huduma karibu, mwananchi anasikilizwa na palipo na kasoro panalekebishwa au kufanyiwa maboresho

Ni serikali iliyojikita kufanya vitu vyenye matokeo chanya kwa mwananchi, Vitu vyenye kugusa maisha ya wanyonge, lakini pia maendeleo yanayopatikana Ni maendeleo yaliyotokana na jasho na nguvu zetu watanzania, hivyo kila mtu anakuwa anajivunia mafanikio hayo
 
Jikite kwenye mada
 
Ndio nimejikita kwenye mada kwa kukuelezea juhudi kubwa Zinazofanywa na serikali hiii kuinua maisha ya mtanzania,Ndio maana unaona serikali inafikia hatua inatoa Hadi Ruzuku ili kumsaidia mwananchi asielemewe na mzigo wa mfumuko wa Bei ambao umeikumba Dunia kwa sasa
 
Back
Top Bottom