Kiongozi Kujenga miradi mingi ya maendeleo nyumbani kwao, nini maana yake?

Best comment ya thread Mrangi 👑
 
Kwahiyo anajiandaa kabisa naye asi aibike sifa zote zikaingia ukoko.
 
Mkuu vipi!? Ulitaka ajenge porini?
 
Hakika huyu anatakiwa kuwa Rais wa Maisha Tanzania. Ninaamini akimaliza kupafanya Chato Dubai ataenda tena mikoa mingine kufanya hivyo. Naomba ifuatie kanda ya Kaskazibi hasa mkoa ule anaoupenda wa Kilimanjaro. Hapo ndiyo watanzania tutamuelewa kuwa ni mtu even😎😎😎😎😎😎
 
Yeye mwacheni atake kujengea watu majengo, watu wa maeneo mengine kila ntu ajenge kwao
 
Kila mtu ajenge kwao nchi itaendelea sana. Mtu ana nyumba tano dar ila kwao ni ile ile ambayo babu yake alimrithisha baba yake.
Maendeleo siyo nyumba, ndiyo maana baba yenu anawajengea taasisi
 
maana yake ni kwamba ni mzalendo wa kweli hana wivu na kwao kama ulivyo wewe, kule kwenu unaogopa kujenga hata duka tu, umeenda kujenga sehemu nyingine eti unaogopa utarogwa,
 
Kidume amewaweza, Watanzania wote wameufyata wanamuacha afanye analo kutakua.
Lakini sio kazi nyepesi viongozi wengine sio kwamba huwa hawapendi kujenga kwao bali huwa ni roho mbaya, ubinafsi na wivu tu ya kudharau waliko zaliwa.

Utakuta mtu mfano ni tajiri amejenga majumba Dar es Salaam, lakini nenda kwao sasa, kuchafu vijumba vya nyasi. Mzee angekua ni mbinafsi basi hizo pesa angejengea mahoteli South afrika huko. Sasa mzee anajenga BETA, HOSPITALI, huyu mtu ni mzalendo.
 
Uharo mtupu.
 
Kwani si wanasema ni mburundi kwahiyo kajenga kwao?
 
Jamaa anatengeneza taswira mbaya sana kwa marais wa nchi hii watakaofuata.

Watautumia ubinafsi wake kama case study kujipendelea makwao.
Kinachonishangaza, wazalendo wachache waliopo kwenye system wameruhusu hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…