Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Unapokuwa kiongozi na ukashindwa kujishusha mpaka chini kwa wale unaowaongoza, kwa kisingizio kwamba wapo viongozi husika katika kila eneo, maana yake unatengeneza picha na unatuma ujumbe kwa wale walioko chini yako kwamba nao wanao watu chini yao hivyo hawapaswi kuwajibika!
Mfano kiongozi wa juu anapodhani kwamba hapaswi kwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospital fulani kwa kuwa kuna waziri mkuu, kisha waziri mkuu naye atasema kuna waziri husika, kisha waziri husika naye atasema kuna katibu mkuu, katibu mkuu naye atasema kuna mkuu wa mkoa, wilaya... itaenda hivyo na mwisho wa siku ndiyo hayo utakuta hospital ya majengo mawili inetumia gharama ya mabilioni kujenga!
Kiongozi aliyepo juu lazima awe very humble kwa sababu utendaji wa wale waliopo chini yake hutegemea kwa kiasi kikubwa na mwenendo wake.Vile vile itamsaidia kujua na kutambua uhalisia wa hali za kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na changamoto za msingi katika maisha ya kila siku ya wale anaowaongoza.