Kiongozi Mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh afariki baada ya kushambuliwa akiwa Iran

Kiongozi Mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh afariki baada ya kushambuliwa akiwa Iran

Unamaana kama walivyofinywa kina Mandela, Kinjekitile, Mkwawa na wa namna hiyo?
Mandela alisimamia taifa lake Afrika Kusini, Kinjektile na Mkwawa walitetea falme zao, je Hizbollah wamedhulumiwa mimi na nani ?! Waislamu wa Bukoba waliochoma makanisa kisa Quran kuchanwa Canada walidhulumiwa nini na waumini wa makanisa ya Bukoba ?
 
Inasemekana Israel imetumia kombora kumuua. Ikitokea ni kweli basi hilo ni very advanced na dogo na lina mahesabu makali sana. Maana hilo eneo haijasikika mlipuko kabisa. Wakati Tehran iko zaidi ya 1,500km kutoka mpaka wa Israel na ni lazima uvuke anga la Iraq kuingia Iran kama unatokea Israel. Kombora lazima liwe kubwa kufika, ila likiwa kubwa linaacha alama za moshi karibu na impact site. Sasa immediately hawajaona moshi.

Hata hivyo sitarajii Iran kutoa taarifa kamili ilikuwaje maana wana aibu. Hamna cha Mossad wana mawakala, ni hivi Iran bado kuwa level za Israel kwenye ujasusi na mission ngumu.
Kama ni kweli kama Iran wanavosema kuwa Haniyah aliuawa na Airbone projectile, this must one most new advanced weapon we should all be woried of.

Netanyahu alipokuwa Congress alisema Israel and USA has worked together to make some of most advanced weapons in the world.

Pia ikitokea kama ni some sort of AI powered thing, ni jambo kubwa sana na la kuzingatia
 
Arafat hakuwahi kuwaweza Wayahudi na harakati zake zilimfanya awe mtu wa kutangatanga...

Pia alishindwa kuwaunganisha Wapalestina, maana alijikuta anapata upinzani kwa Wapalestina kuanzisha makundi ya wanamgambo kumpinga na hawa Hamas walizaliwa wakati Arafat alikiwa kiongozi wa PLO...

Sifa pekee ya Arafat ambayo inakubalika, alikuwa anafanya movements zake kuepusha sana umwagaji damu wa ndugu zake tofauti na makundi mengine ambayo yamejikita kwenye kufanya mashambulizi ya kijeshi...
kifupi tu arafat hakuwa gaidi hawa hamas and the likes wanaoungwa mkono na iran ni magaidi piwa.
 
Isipokuwa kuna wale wengine wavaa kanzu wao hujilioua ili kuingia mbinguni. Na wana makundi maalum ya kujilipua.
Huyo kauawa na Mossad tu, kwa kombora lazima lingekua detected.

Mossad ni wazuri kwa kuua ila kwenye kufanya 'intelligence gathering ' bado wataendelea kutegemea msaada wa Marekani maana Ina vyanzo na rasilimali nyingi za kukusanya taarifa.
 
Iran security established imeshakuwa 'compromised' na vyombo vya kijasusi kutoka maadui wa Iran.....ndio maana hao wauaji wanaweza kutekeleza matukio aina hiyo na kutoroka bila kukamatwa.

Isitoshe Mossad imeajiri mawakala wake wengi tu ndani ya Iran wanafanya hizo kazi za kijasusi (espionage) kwa niaba yao.

T14 Armata dudus Aleyn
kwa hyo kumbe wairan hawataki maujinga ya ayatoula ndo maana wanakubali kuwa agents wa mossad..
 
Iran kajikita sana sehemu tatu mkuu na hizo sehemu yuko vizuri kuliko Israel.
-Uundaji wa Air defence systems.
-Uundaji wa multi rocket launchers Na ballistic missiles.
-Uundaji wa drones.Hata ile Drone ilopenya Tel Aviv Na kushambulia pasi na kuwa detected ni Iranian made.
Hizo sehemu Iran amepaboresha sana.

Siamini kama Iran anaweza kuwa na air defense ya aina ya S400, Patriot na hizi Iron dome kulinda anga lake maana tayari ameonyesha udhaifu mwingi kwenye technolijia, kama ana uwezo huo asingeweza kutumia Helicopter ambayo ni made in USA kumbeba Rais huku akiwa na vikwazo vyakununua spare parts.

Zile drones bado sana mkuu aisee, drones zake kamikaze nyingi zimeprove failure Russia, na hata hizi tunazosema zimepenetrate air defence ya Israeli inawezekana ni ile tunasema huwezi kuwa na 100% efficiency, zipo drones za Turkey ambazo angeweza kuzinunua na kutumia wataalam wake kucopy na kupaste akafanya mass production.

Kuwa na missiles launcher sio shida, kama huna satellite zinakuwa rahisi sana kukamatwa au hata kuwa diverted kwenye targets.
Anachofanya/alichofanya Iran ni kurusha missiles nyingi kama mvua ili kuoverwhelm air defense na makombora kadhaa yaweze kufika lakini hii unaweza kuipangua kwa kuongeza number za batteries, kumbuka pia unaposhambulia nawe unashambulia hakuna kusubiliana maana uwe na uwezo wa kushambulia na muda huo huo ujilinde.
Kumbuka pia, unaporusha makombola mengi hovyohovyo just kuoverwhelm air defensive system na upate target chache ambazo pia utakuwa unabet basi pia stock ya ammunitions zako inapungua huku hauna uwezo na speed ya production kuendana na matumizi.

Narudia tena, Iran awe mtulivu ajenge technolojia yake kwanza kupambana na hizi superpower, uwezo wake bado sana.
 
Hizi vita akili inahitajika sana zaidi ya mizuka ya ajabu ajabu,, waarabu wanataka kupigana kama enzi hizo za kupigana na majambia, halafu hapohapo kwa ujinga wao wanazungukana,,,,waarabu ni kama waafrika tu sema wao kidogo wameachiwa tusenti ila kichwani hazimo,,, ndo maana hata Iran mwenyewe anacheza kwa step maana anawajua waarabu walivyo
Bro tangu lin elimu ahera ikashinda elimu dunia mzee.
 
Russia, North Korea, China, Cuba nk sina uhakika kama zilishawahi kuwa na mgogoro na Israeli kiasi cha kutarget viongozi wa Israeli.

Japo naamini Russia anaweza kuipeleka Vita Israeli na Israeli akasikia sasa yuko vitani, maana naamini Russia ana resources za kutosha na watu wakutosha wenye maarifa maana yake itambidi Israeli naye atumie resources za kutosha kumkabili adui kuliko ilivyo sasa na waarabu maana naamini Israeli anatumia resources chache sana kuwakabili.

Shida ya waarabu hawana technolojia na watu wenye akili zilizokomaa kwenye technolojia ya vita na vifaa vya kivita, vita ya sasa ni technolojia na watu wenye kuijua technolojia, kama huna hivyo vitu basi nikujisumbua sana kupigana na hizi superpower.
Quote: Shida ya waarabu hawana technolojia na watu wenye akili zilizokomaa kwenye technolojia ya vita na vifaa vya kivita, vita ya sasa ni technolojia na watu wenye kuijua technolojia, kama huna hivyo vitu basi nikujisumbua sana kupigana na hizi superpower.
Hiyo 👆 👆 ni kweli kabisa lakini pia Waarabu hawako Focused, Organised na mambo yao hawafanyi kwa kutulia ni kama wanamhemko fulani hv hawazisomi alama za nyakati - wanakurupuka.
 
Majukumu ya kumlinda alikabidhiwa Iran. Ofisi zao zilihamishiwa Baghdad kutokea Doha Qatar.

Kwa vyovyote vile kauzwa. Pale Iraq, Sunni pamoja na Kurds hawakutaka ofisi za Hamas zihamishiwe Iraq.

Kwahiyo ina maana kuna waliouza movements zake na ku share intelligence na MOSSAD.

Mbaya zaidi, ameuwawa ndani ya Taifa lilotakiwa kuhakikisha ulinzi na usalama wake.

Tena siku ya kuapisha rais wao mpya ambapo ulinzi ulitakiwa uwe wa hali ya juu kabisa!
Kabisa mkuu, tena utakuta mpaka kuuawa kwake kuna uhusika wa nchi kadhaa katika kutoa taarifa au kutoa ridhaa.

Kwa siasa za mashariki ya kati si ajabu kukuta baadhi ya watawala wa hapo wamefurahi jamaa kuondolewa maana uhusiano wake na Iran ulikuwa unawakera

Hata security establishment za Iran Zina matatizo ndio maana hata mwanasayansi wa nyuklia na wenzake waliuawa, kiufupi bila ushirikiano na wasaliti sio rahisi hayo matukio kufanyika.
 
Hawa jamaa hata rais wa Iran utakuta wanajua nyendo zake zote....ni kama vile mossad ina watu wake kwenye vyombo vya ulinzi vya nchi zote maadui wa Israel. Precision kwenye mapigo yao si ya kispotispoti
 
Back
Top Bottom