Siamini kama Iran anaweza kuwa na air defense ya aina ya S400, Patriot na hizi Iron dome kulinda anga lake maana tayari ameonyesha udhaifu mwingi kwenye technolijia, kama ana uwezo huo asingeweza kutumia Helicopter ambayo ni made in USA kumbeba Rais huku akiwa na vikwazo vyakununua spare parts.
Zile drones bado sana mkuu aisee, drones zake kamikaze nyingi zimeprove failure Russia, na hata hizi tunazosema zimepenetrate air defence ya Israeli inawezekana ni ile tunasema huwezi kuwa na 100% efficiency, zipo drones za Turkey ambazo angeweza kuzinunua na kutumia wataalam wake kucopy na kupaste akafanya mass production.
Kuwa na missiles launcher sio shida, kama huna satellite zinakuwa rahisi sana kukamatwa au hata kuwa diverted kwenye targets.
Anachofanya/alichofanya Iran ni kurusha missiles nyingi kama mvua ili kuoverwhelm air defense na makombora kadhaa yaweze kufika lakini hii unaweza kuipangua kwa kuongeza number za batteries, kumbuka pia unaposhambulia nawe unashambulia hakuna kusubiliana maana uwe na uwezo wa kushambulia na muda huo huo ujilinde.
Kumbuka pia, unaporusha makombola mengi hovyohovyo just kuoverwhelm air defensive system na upate target chache ambazo pia utakuwa unabet basi pia stock ya ammunitions zako inapungua huku hauna uwezo na speed ya production kuendana na matumizi.
Narudia tena, Iran awe mtulivu ajenge technolojia yake kwanza kupambana na hizi superpower, uwezo wake bado sana.