Mkuu kuna maeneo umedanganya.
-Kamikaze drone za Iran hazikufeli Russia,zimeprove kuwa na ufanisi na zishapelekwa zingine zinatumika.
Drone iloshambulia Tel Aviv kwa kutumiwa na Houthi haikuwa detected mpaka ikafanya shambulio it means iron dome ilifeli kuigundua,na hiyo ni Iranian made.
Drone zote ambazo anatumia Hizbollah Lebanon kumshambulia Israel ni Iranian made.Na hazikuwahi kufeli zote zimeshambulia Galilaya kwa ufanisi na kuleta damage.
-Makombora anayotumia Hizbollah ambayo ni guided ballistic missiles ambayo yalionesha kukwepa air defence system na kushambulia Northern Israel kikamilifu na yalirushwa guided missiles 680 tokea October yote yalipenya succesfully na hakuna hata moja Iron dome waliweza kulidungua.Na yote hayo ni Iranian made.
-Iran ana varieties of missiles ambazo zina uwezo tofauti tofauti nenda kafuatilie mkuu,yale makombora alotumia Iran dhidi ya Israel hayakua guided missiles,Na cha kushangaza ni light unguided missiles licha ya mataifa manne kumsaidia Israel kuya intercept bado makombora 7 yakapenya.Jiulize kama Iran angetumia kombora lenye usanifu kama lile alilopiga kwenye kambi ya USA Iraq 2018 lingetokea nini.
Tukirudi kule kuhusu teknolojia ya ndege,mkuu teknolojia ya drone na aircraft hazifanani.
Huwezi ukafananisha uundaji wa drone na helikopta au ndege kamili.
Iran ana teknolojia kubwa katika uundaji wa kamikaze drone ila uundaji wa aircraft bado haijajipambanua.
Kuhusu ADS kazifuatilie BAVAR-373 na Khordak air defence systems.
Ndizo zilidungua drones za upelelezi za USA.
Pia usisahau kipindi cha Obama 2013 kuna drone za USA zilishushwa pasi na kulipuliwa ndani ya anga la Iran,je hiyo ni tech ndogo mkuu.
Shambulio la Haniyeh lilifanyika ndani sio nje ya mipaka ya anga.
Kwenye technolojia yeyote huwezi kupata efficiency 100%, kama Houthis walirusha drone ikapenetrate moja tu Tel-aviv kwanini wasirushe zakutosha sasa maana wako vitani na Israeli ambae amefanya shambulio kubwa na kuleta maafa Yemeni - kupenya drone Moja hatuwezi kusema Iron dome ni totally useless hiyo ndio ile tunasema kwenye tech hakuna 100% ila tunaangalia angalau ufike hata 95% efficiency.
Binafsi Kila siku nasikia Israeli kaua Hizbollah strategic leaders ambao ndio master minder wa operations, ila sijawahi kusikia Hizbollah kaua kiongozi au kamanda yeyote wa Israeli, tafsiri yake master minders na head wa operation wa Israeli wako salama.
Hizbollah na Iran wanatumia style ya kurusha barrage of missiles au drones ili kuoverwhelm ADS, hii technic ni mbaya maana unamaliza stock ya ammunition yako kwa haraka, kisasa ni vyema ukawa na missile ambazo ni self-guided na zenyewe zinaweza kukwepa ADS na kwenda kuhit targets, au uwe na technolojia yakujam batteries za ADS uweze kupenya.
Tunapozungumzia Technolojia tunaangalia maeneo mengi ni kama pia tunapozungumzia uwezo wa kijeshi, Iran angekuwa na ADS za uhakika basi Israeli naye angekuwa anarusha barrage of missiles kushambulia maeneo ya nyuklia ya Iran, lakini mara nyingi tunaona Israel anapeleka kombora chache na ndege kadhaa kupiga maeneo kadhaa yanayohofia kuhusika na urutulubishaji wa nyuklia ndani ya Iran.
Kitendo cha Israel kupenetrate ndani kabisa ya Iran na kuua wale strategic people anaowataka mfano wanascience, wanasiasa nk ndio tunapata red flag kama Iran yuko overated na anahitaji sana kujipanga.
Umeongelea juu Kamikaze drones, sifa ya Kamikaze drones nikwenda na kubaki huko huko, na sio zile ambazo ziko operated kwenda na kuhit target na kurudi, maana unahitaji kamikaze nyingi sana kupigana vita wakati unaepigana naye yakwake inakuja imebeba bomu inapiga na kurudi, Mrusi aliamua kuchukua Kamikaze drones kulinda stock yake ya silaha lakini pia kuzijaribu in real world, ni changamoto kupenya kwenye ADS kama Patriot ndio maana Ukraine amedemand kupewa Patriot batteries za kutosha kuweza kuzipeleka maeneo mengi kulinda anga.
Israel kwa kiasi kikubwa yuko vizuri kwenye technolojia kwenye maeneo mengi muhimu ya kijeshi namaanisha baharini, ardhini, angani nk,
Sasa huwezi kusema kitaalam una muscles wakati Kuna maeneo kijeshi hata mwenyewe unajua hauko vizuri wakati vita kushindwa na kushinda inategemea uzaifu wa adui ndio maana tujaribu options zote kwenye mapigano.
Mbinu anayojaribu Israeli kwasasa kuua wale heads ni kujaribu kumaliza proxy war kuuzunguka maeneo yake na kuineutralize Gaza strip, mbinu ndio hivi karibuni inatumika Mexico kupambana na drugs Cartel, Proxy war ya hivi vikundi vidogovidogo ndio inayomletea stress Israeli maana anabaki vitani muda mwingi, lakini lazima tujue pia hizi proxy style ndio pia zinafanya nchi kama Lebanon, Syria na Iraq kutotawalika ili kuwa safe ground Kwa hivi vikundi na main target ikiwa Israeli ambaye sidhani kama anapata mazara makubwa kuliko Syria, Iraq, Lebanon, Yemen nk.
Binafsi nahitaji kuiona amani siku moja mashariki ya Kati watu wote wakae kwa amani maana jamaa upande ule inateseka sana na kudhidi kukuza chuki za vizazi na vizazi.