Kiongozi wa Iran Ayatollah Khamenei, anafanya kosa kubwa kwa kutangaza wazi mahali na muda wa hotuba yake

Huyo kuna namna yake ya kumla kichwa haitaji nguvu kubwa.. siku atashindwa kuamka kitandani ndiyo mwisho wake hapo
 
Wanatafuta sababu ya kufuta lile taifa feki,yaani israel wakitaka kurudi walikotoka 1947 wapige huyo mzee
Ye nani na anatofauti gani na waliouwawa au ndo ushabiki maandazi,Israel hajawahi kusita kwenye maamuzi yake only a right time is waited.
 

Kiongozi wa juu anapotangulia mbele mara zote inatia hamasa zaidi
 

Kiongozi wa juu anapotangulia mbele mara zote inatia hamasa zaidi
 
Kwamba wewe unajua masuala ya ulinzi na usalama wa Ayatollah kuliko taasisi ya ulinzi ya Iran? Watanzania tuna vituko sana.
 
Bado ni hatari sana kwa Iran kama nchi kufanya hivyo.
Iran ina mifumo ya anga madhubuti na imethibitisho hilo awamu ya Obama kwa kuishusha ndege ya kijasusi ya America kama ilivyo!

Kingine unafikiri US haijajaribu kwa namna tofauti ya kuangalia uimara wa anga ya muajemi?

Vita yake na Gaza eneo dogo tu akawa anasaidiwa silaha na US kwa sababu yeye zilikuwa zinamuishia. Kwa nchi kubwa kama Iran atashambulia kwa kiwango gani pasipo kuhitaji msaada wa moja kwa moja kutoka US?

Gulf states Qatar, Kuwait, Bahrain, UAE, Saudi Arabia n.k wametoa tangazo lao jana kuwa hawataki vita ukanda wao.

Sababu ni kwamba ukanda wao ndiyo wenye base za kijeshi nyingi za US. Israel haina uwezo wa moja kwa moja kumvamia Iran lazima US aingilie.

Uwezo wa Israel kijeshi dhidi ya Iran ni mdogo sana labda US aingilie kati na jambo ambalo ni la hatari na ndiyo maan utawala wa Biden umemwambia Benjamin Netanyahu asithubutu.

Njia pekee Israel inaweza kuitumia ni ya kijasusi kwa sababu ndani ya Iran kuna jamii ya wayahudi takribani laki 8.

Na hili jaribio wakilifanya kwa haraka kwa kutumia wayahudi wenzao huko litasomeka moja kwa moja kuwa ni wao.
 
Ye nani na anatofauti gani na waliouwawa au ndo ushabiki maandazi,Israel hajawahi kusita kwenye maamuzi yake only a right time is waited.
Maamuzi yake Israel huwa ni kwenye mataifa dhaifu.

Lebanon alishambulia viongozi wa Hizbullah kwa ndege zake za kivita. Syria anashambulia kwa ndege zake za kivita. Yemen kwa ndege zake za kivita. Iran katumia jasusi kupandikiza mlipuko kwa kiongozi wa Hamas.

Bado huioni tofauti hiyo? Iran imemzidi nguvu na ndiyo maana hataki kutumia mbinu za kufahamika kuwa ni yeye moja kwa moja.

Na ashukuru Mungu kule Iran kuna jamii ya wayahudi ambao anaweza kuwatumka kama chambo wa kukamilisha Misson zake.
 
Sizani kama israel inaweza kuuwa rais wa iran,kumbuka huyo sio gaidi
Kama Iran wamemuweka Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau kwenye list ya magaidi wanaotakiwa kuliwa kichwa, kwanini nao Israel wasim-target Ayatollah?
 
Wao husema hawaogopi kifo.Watakufa kishahidi/martyrs.
 
Kama Iran wamemuweka Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau kwenye list ya magaidi wanaotakiwa kuliwa kichwa, kwanini nao Israel wasim-target Ayatollah?
Hao Iran wanaongea tu,aisee kiongozi wa nchi huwez kumuua kirahis rahis tu,hata kama nchi yake ni dhaifu vipi
 
Unadhani nawao hawana akili??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…