Mkuu, afadhali tumefahamu alipo, maana watanzania tulianza kuwa na wasiwasi juu ya mtetezi wa ma-DR,
tunawaomba wanaharakati please fuatilieni hilo na kulaani, ukatili dhidi ya jeshi la police na kama wamemdhuru, Solidarity forever
Sasa imefikia mahali ambapo Mungu ambaye nii mtetezi wa wanyoke kujidhihirisha. Hakuna serikali dhalimu kama hii, na serikali dhalimu mwisho wake ni mbaya. Zifuatazo ni dalili dalili za serikali dhalimu ni upofu, uvivu wa kufikiri. dhuluma, unayayasaji, mabavu, ubinafsi na ushirirkina.
Mungu atavishughulikia vyote kwani hizi zote ni dalili za mwisho za utawala wa aina hiyo. Mungu hushughulikia mambo kwa aina ya ajabu ambayo mwanadamu huwa anajiona mshindi na anazidi kujiinua, kumbe ndipo anapofagilia mwisho wake.
Tuna mifano hai ya wizara ya afya ambayo haina muda mrefu. Lakini ni serikali hii hii ambayo imepofuka. Kikubwa ni kusimama katika maombi na kupambana. Haingii akilini kwamba hata madiwani wamepandishiwa mishahara hadi kufikia 250,000/= toka 120,000/= eti mtumishi wa serikali haiwezekani kupandishwa hadi laki tatu!!! Inasikitisha. Hapa wanasiasa wanataka kuonyesha kuwa wenyewe ni bora kuliko walioenda shule.
Kinachonitia hofu kwa kukamatwa kwa Dkt Ulimboka, ni lengo la kumkamata. Kwani serikali hii inatumia sumu kwa saana. Wanaweza kumwachia bila majeraha, lakini baada ya muda mrefu au mfupi, tunaweza kushuhudia Dkt Ulimboka ama akifa ghafla au akiendelea kudhoofika. Tufikirie kwa mazingira hayo.
Lakini huo ni mwanzo wa mwisho wa serikali inayomtegemea Lucifer.
Mungu awabariki Madaktari, watumishi wote wa sekta ya afya na watumishi wengine wote wanyonge wa nchi hii.