Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Jamani nikweli hili?Limenistua mno!Isiwe ya singida namuheshimiwa waziri!
 
Dr. Slaa alisema serikali ya CCM imefikia mwisho wa kufikiri! Hizi ndo dalili za wazi, tunahitaji kuichukua serikali mikonono mwa CCM mapema zaidi! Wameshindwa kuiongoza nchi.
 
Nani alishinda?

Watanzania lakini wakadhulumiwa na NEC kwa kumtangaza dhaifu kuwa mshindi na kwa kuwa haturuhusiwi kupiga ikabidi tuwe wadogo kama piritoni hata kama angekuwa mbwa ndiyo katangazwa kuwa mshindi..
 
Ametekwa au amekamatwa na Polisi.

Ritz
angekamatwa na polisi maana angekuwa ktk mikono salama na sheria ingefuata mkondo wake,lakini kwa hili unaweza sema katekwa,maana kutekwa kuna mawili
1.watekaji wakudhuru bila kudai chochote kile
2.watekaji wakushikilie huku wakidai chochote ili waweze kukuachia

la Dr watekaji wamempa kichapo na nadhani walifikiri kuwa tayari kapoteza maisha na ndio maana wakampeleka huko walikopotea wachimba madini wa mahenge.
 
Wakuu huyu mtu nimekuwa nikimsikia mara nyingi sana kwenye vyombo vya habari,ningefurahi sana kama ningeweza kupewa taarifa zake na cv yake ikiwezekana,kwangu anaonekana kama mtu anayepigania haki fulani ambayo wengi hatujaiujua bado,anakuwa kama Dactari lakini the same time ni mwanaharakati na mtu muhimu sana kwa mapambano yanayoendelea ndani ya taifa letu lililojeruhiwa vibaya!
 
naona tz tunaelekea kama kuwa kama Misri sasa...haaooooo....!!!!
 
nadhani sasa badala ya mgomo baridi utakua mgomo moto.!
 
Nimesikia huku mtaani amepatikana eneo la Bunju akiwa hoi, amepigwa haijulinaki, amegongwa haijulikani! Taarifa zilizopo amepelekwa MOI haraka.

Nazidi kufuatilia hili nikipata zaidi nitarudi tena.
 
Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid'.

Habari za kidaku zimesambaa kwamba huyu abeid Mama yake alikufa kwa kukosa matibabu katika mgomo uliopita....
na amesema ata strike back ten times more...hii balaaa
 
kina nani si uwataje basi..

Soma thread zilizopita! habari inaongelewa tangu jana saa 6 usiku we bado unauliza maswali ambayo majibu yake yapo humuhumu kwenye hii thread!
 
Mkuu, afadhali tumefahamu alipo, maana watanzania tulianza kuwa na wasiwasi juu ya mtetezi wa ma-DR,
tunawaomba wanaharakati please fuatilieni hilo na kulaani, ukatili dhidi ya jeshi la police na kama wamemdhuru, Solidarity forever

Sasa imefikia mahali ambapo Mungu ambaye nii mtetezi wa wanyoke kujidhihirisha. Hakuna serikali dhalimu kama hii, na serikali dhalimu mwisho wake ni mbaya. Zifuatazo ni dalili dalili za serikali dhalimu ni upofu, uvivu wa kufikiri. dhuluma, unayayasaji, mabavu, ubinafsi na ushirirkina.

Mungu atavishughulikia vyote kwani hizi zote ni dalili za mwisho za utawala wa aina hiyo. Mungu hushughulikia mambo kwa aina ya ajabu ambayo mwanadamu huwa anajiona mshindi na anazidi kujiinua, kumbe ndipo anapofagilia mwisho wake.

Tuna mifano hai ya wizara ya afya ambayo haina muda mrefu. Lakini ni serikali hii hii ambayo imepofuka. Kikubwa ni kusimama katika maombi na kupambana. Haingii akilini kwamba hata madiwani wamepandishiwa mishahara hadi kufikia 250,000/= toka 120,000/= eti mtumishi wa serikali haiwezekani kupandishwa hadi laki tatu!!! Inasikitisha. Hapa wanasiasa wanataka kuonyesha kuwa wenyewe ni bora kuliko walioenda shule.

Kinachonitia hofu kwa kukamatwa kwa Dkt Ulimboka, ni lengo la kumkamata. Kwani serikali hii inatumia sumu kwa saana. Wanaweza kumwachia bila majeraha, lakini baada ya muda mrefu au mfupi, tunaweza kushuhudia Dkt Ulimboka ama akifa ghafla au akiendelea kudhoofika. Tufikirie kwa mazingira hayo.

Lakini huo ni mwanzo wa mwisho wa serikali inayomtegemea Lucifer.
Mungu awabariki Madaktari, watumishi wote wa sekta ya afya na watumishi wengine wote wanyonge wa nchi hii.
 
Tumuombee apone ili tupate ukweli wa mambo kwuwa nani alimteka jemedari huyu, wakati wanamjeruhi lazima waliongea chochote.Mungu amemuokoa ulimboka wao walidhanoi wamemuua.AIBU YAO CCM
 
Binafsi sikutegemea jambo kama hili lifanyike kwa wakati kama huu! Siamini kama hayo ni maagizo ya serikali ya ccm inayoongozwa na Kikwete! Sasa huku ndo kutatua mgogoro na madaktari?
 
Watanzania lakini wakadhulumiwa na NEC kwa kumtangaza dhaifu kuwa mshindi na kwa kuwa haturuhusiwi kupiga ikabidi tuwe wadogo kama piritoni hata kama angekuwa mbwa ndiyo katangazwa kuwa mshindi..

Tunaongelea issue ya Madaktari wewe unaleta mambo ya Chadema...wewe kila kitu Chadema.
 
Back
Top Bottom