Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

lete ushahidi usilete komedi hapa na wewe ungepingwa wewe sasa ndo uone shame on u
 
Ikulu kuhusishwa na kichapo cha Dr Ulimboka source BBC

Kabisa hata mie naunga mkono BBC Ikulu inahusika na hili hawawezi kujinasua hata wafanyaje, na ningekuwa mie ni daktrari ningewahimiza madaktari wote wasiwatibu watu wa ikulu pamoja na ndugu zao tuone wataenda wapi.

Hii nchi inafanya kila kitu ni siasa roho zawatu wanaziweka kwenye siasa sijui tunakoelekea ni wapi kwakweli inatia uchungu sana ila serikali ikumbuke ukimfanyia mwenzio ubaya nawe yatakukuta malipo ni hapahapa duniani. Auwaye kwa upanga nae atakufa kwa upanga..😡😡😡
 
"kwa kupigwa kwake madaktari na wagonjwa watapona",, mpambanaji wa ukweli ugua pole na upone haraka ,naugua pamoja nawe
 
Kwi! Kwi! Kwi! kwi! hata Usalama wa Taifa wapo kwenye Thread Hii kama Guest Ngoja niondoke nitarudi baadae
 
Pole sana Dr.Ulimboka. Naangalia upande wapili wa shilingi ni huu,unaweza kufanya kitu usijue itakuwaje kesho,lakini naamini sana walichofanya serilaki yetu sikivu ni kumpandisha chati zaidi aonekane ni mkombozi wa wanyonge.
 
Katika hali ya kawaida, kwa serikali yeyote hata ikiwa DHAIFU, nilitegemea hadi sasa, masaa zaidi ya 12 baada ya tukio hili kutokea, waziri au mtendaji mwingine wa serikali ajitokeze hadharani kuzungumzia hili suala.
Serikali ijue kwamba tangu taarifa za kutekwa na kujeruhiwa kwa Dr Ulimboka kusambaa miongoni mwa jamii, hali ya taharuki imeenea miongoni mwa watu. Ni wazi kabisa kuwa hadi sasa kuna mamia ya watu hawajafanya kazi leo wanahaha huku na huko kutafuta taarifa, na wale wenye wagonjwa wakijawa na wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya wagonjwa wao
Jamii ya watanzania hadi wakati huu hawajui ni nini kitatokea

Kufuatia hali hii, naishauri serikali, iwe imehusika au hakuhusika kutoa hadharani tamko la kuwahakikishia wananchi kuwa hali ni shwari (hata kama sio shwari, ndiyo protocol), kuwahakikishia kuwa afya ya Dr Ulimboka inaendelea vizuri (hata kama haiendelei vizuri, but ndiyo protocol), na kuwahakikishia kuwa lilitokea kwa Dr Ulimboka halitaathiri huduma za afya nchini na kuwa mazungumzo yanaendelea na madaktari (hata kama sio hivyo).

Kusema kweli mimi binafsi tangu nimefika ofisini asubuhi na kukuta habari hii, nimeshindwa kabisa ku-concentrate kwenye kazi, na naamini pengine tamko la serikali litanituliza.

Kama wakishindwa, naomba waziri kivuli wa afya wa CHADEMA atoe tamko hilo mara moja...
 
Niki coment hapa nitaandamwa kwa kutishia kuua ngoja nitatekeleza kimya kimya mambo yangu dhidi ya HOMOSAPIEN
 
Last edited by a moderator:
Nitarudi baadae maana sielewi. Moja na moja ni mbili. Pole Dr.
 

Mchongo wa kudundwa ! ........... Duuuuh !.........imekaaje hii !?
 

Naipenda sana michango yako humu JF, hili la Ulimboka tusiingize vyama, ni sawa kabisa na pia tusivituhumu vyama.

1) Inawezekana Ulimboka katandikwa na watu wenye uchungu.

2) Inawezekana kapigana kwa ujeuri wake na wenzake wakamshinda nguvu (hata kama alikuwa chini ya ulinzi anaweza kujidai kupigana na askari).

3) Inawezekana wasoitakia mema serikali wakafanya njama wao wenyewe wamtandike huyu ili ionekane serikali mbaya.

Lakini nasema kuwa, ikiwa ni raia wenye uchungu wamechukuwa shria mkononi na kumtandika huyu, basi hawajafanya makosa. Astahili yake.
 
we unaongea nini mlitaka kumuua kwa kisingizio hiko yaani kwa jinsi ulivyo mvivu wa kufikiri mmefanya hivyo hili mtuaminishe iko ulichosema nilijua tu mtaropoka majibu kwa nini mlifanya hivyo umeona watu wako kimya umeamua kusema mlichoplan kwa taarifa mmefilisika vibaya yaani ndio safari ebu fikiri matukio ya wiki hii tu alafu uniambie 2015 utapona aha wapi utoki wiki hii kwa kifupi ndani ya siku tano mabilioni 300 uswiss,mgomo wa madaktari uliyosababishwa na utapeli wa selikali, na huli la njama ya kumuua ulimboka! ya zamani kidogo taka kumuua kiwia,kumuua m'kiti usa river,mauaji igunga, ya zamani zaidi containa bot,rada,dowans,epa,tangold,merementa,kiwila, buhemba, vijisent yaani mwana hamtoki unajichfua bure
 
Nahisi hata hao madaktari
wenzake ambao wanamtibu
inabidi wachunguzwe kwa
makini katika wakati kama
huu sababu hofu yangu ni
kwamba isije kuwa tayari
system ishaandaa Dokta feki
ili akammalizie pale pale
kitandani ama apigwe slow
poison ya kuharibu kila
system nzima ya mwili wake
 
lete ushahidi usilete komedi hapa na wewe ungepingwa wewe sasa ndo uone shame on u
hiyo ndio hali halisi kabla ya kukurupuka nenda kwa wahusika(waliopokea ripoti ya tukio hilo wakupe data)
wewe ndio unaleta comedy kwa kutuhumu askari wa usalama wa taifa lako kuwa wameshiriki katika tukio hilo muna ushahidi gani??!!
waite viongozi wenu wanaowapelekesha kama gari iliyokosa muelekeo mtoe huo ushahidi,naona mukishapewa pombe za ofaa huwa muna mengi ya kuzungumza,na zikiwaruka kichwani tu munarudi katika hali halisi yenu!
taifa hili kuongozwa na walevi sijui kama itawezekana hapo ndio itakuwa nigeria ndogo!
 
Kwi! Kwi! Kwi! kwi! hata Usalama wa Taifa wapo kwenye Thread Hii kama Guest Ngoja niondoke nitarudi baadae

Sasa kulikuwa na haja gani ya wewe kubandika hiyo orodha nzima hapa?
 
2pashane kuhusu maendeleo ya huu utata mana wengine ndo kwanza tunaiona hii habari hatuna hata la kuchangia
 
Serikali yetu haina uchungu na wananchi ambao ndio wanaumia kutokana na kushindwa kutatua tatizo la madaktari kwa sasa
 
samrich1:
soma tena kwa makini hiyo:

mgomo wa mara hii ulikuwa unaelekea kupotea(kutokuwepo) wakaona ni busara kuchonga mchongo wa kumpiga,na kumchafua zaidi usoni,ili waamshe hisia za ma doctor na kuwafanya wale waliokuwa hawana nia ya kugoma agome.
ushahidi uko wapi kuwa waliomteka ni askari au usalama??!!
hamuoni kuwa yeyote anaweza kujivisha hivyo vyeo tu??!!
kwa nini huyo doctor toka mwanzo asimuulize huyo"abeid au john-ni majina tu-)kitambulisho chake!!
kama watu wangetaka kumuuua wangeshamuua kitambo tu lakini wanajali haki yako kama mtanzania!
huu mchongo umechongwa na wanasiasa kwa kushirikiana na baadhi ya ma doctor wakampigisha mwenzao kwa maslahi yao!
huku ndipo tunapoelekea
 
Kama ni kazi ya serikali, basi wametumia a very crude way ya kusuluhisha matatizo. Kwani is this the only or last 'Ulimboka' living?
 
Si umesema utakuwa wa mwisho kulaumu! umeanzisha thread!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…