Katika hali ya kawaida, kwa serikali yeyote hata ikiwa DHAIFU, nilitegemea hadi sasa, masaa zaidi ya 12 baada ya tukio hili kutokea, waziri au mtendaji mwingine wa serikali ajitokeze hadharani kuzungumzia hili suala.
Serikali ijue kwamba tangu taarifa za kutekwa na kujeruhiwa kwa Dr Ulimboka kusambaa miongoni mwa jamii, hali ya taharuki imeenea miongoni mwa watu. Ni wazi kabisa kuwa hadi sasa kuna mamia ya watu hawajafanya kazi leo wanahaha huku na huko kutafuta taarifa, na wale wenye wagonjwa wakijawa na wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya wagonjwa wao
Jamii ya watanzania hadi wakati huu hawajui ni nini kitatokea
Kufuatia hali hii, naishauri serikali, iwe imehusika au hakuhusika kutoa hadharani tamko la kuwahakikishia wananchi kuwa hali ni shwari (hata kama sio shwari, ndiyo protocol), kuwahakikishia kuwa afya ya Dr Ulimboka inaendelea vizuri (hata kama haiendelei vizuri, but ndiyo protocol), na kuwahakikishia kuwa lilitokea kwa Dr Ulimboka halitaathiri huduma za afya nchini na kuwa mazungumzo yanaendelea na madaktari (hata kama sio hivyo).
Kusema kweli mimi binafsi tangu nimefika ofisini asubuhi na kukuta habari hii, nimeshindwa kabisa ku-concentrate kwenye kazi, na naamini pengine tamko la serikali litanituliza.
Kama wakishindwa, naomba waziri kivuli wa afya wa CHADEMA atoe tamko hilo mara moja...