Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Nani aliyegundua uwepo wa Dr. Ulimboka huko walikomtoa...

na ilikua saa ngapi.?na alitupwa kwenye mazingira gani? Na nani wa kwanza kutoa taarifa wakati yeye alikua haonge.?
 
Habari nilizozipata punde kutoka kwa mtu wangu wa karibu na wakuaminika ni kwamba Dr. Ulimboka amemtambua mtu mmoja kati ya watatu waliomteka akiwa kitandani MOI, huyo jamaa ni afisa usalama alievaa kiraia na kujifanya mwandishi wa habari kwenda kuhakikisha kama kazi waliotumwa ya kumaliza Ulimboka imekamilika ndipo Ulimboka alipomtambua na Madaktari kuweka zana zao za kazi chini na kuanza kumshughulikia kikamilifu kama mbwa mwizi mtu alie husika na mateka ya Ulimboka....

Tunasubiri nini kwenda kufukuza mafisadi kwenye ofisi kuu ya umma?
Walianza na Rwegasira wa TRL, Wameendela na Ulimboka, watamfuata Mgaya kisha wanamalizia na Dr. Slaa!

Tukawafukuze kabla hali haijawa mbaya zaidi! Inuka twende....! aaagh!
 
Wewe uko sawa kweli ? au unafikiria kwa kutumia majani ya matembele ?

Mkuu hata kama nafikiri kwa kutumia makalio, lakini nakuleza kuwa katika zama hizi za “Open Democracy” na “Multi Party”, ishu kama hizi alizofanyiwa ulimboka haziwezi kupita hivi hivi tu. Katika utawala wa JK, yeye kama “rais” wa nchi ameachia mauaji mengi yamefanyika, “torturing” nyingi zimefanyika na wananchi kuishi kwa wasiwasi. Sasa nakueleze, mark my words, JK akitoka madarakani LAZIMA atashitakiwa na watu wa haki za binadamu, tena sio tu wa hapa nchini, watakuwa hata hao kina Human Right Watch, AMNEST International etc, kwa yeye kushindwa kuchukua hatua stahiki. Mfano wa mauaji na hizo tocha ni kama Ulimboka, wabunge kubigwa na kutaka kuuawa, ishu ya Zanzibar (UHAMSHO), mauaji ya arusha, Iringa, mbeya etc. Mkuu subiri utakuja kujionea mwenyewa tu, kwani ni viongozi wengi wameshafungwa kwa uzembe au makusudi kama haya anayofanya JK, mfano viongozi wa Yugoslavia, Serbia. Pia kumbuka Taylor alifungwa kwa makosa yaliyofanyika Sierra Leone na sio nchini wake Liberia ambapo yeye alikuwa mtawala wa hapo. Mkuu subiri utaona, these issues can never go in vein….
 
Mnaomsikitikia huyo fedhuli mmoja, mnajuwa ni wagonjwa wangapi wanaoathirika na upumbavu wake? au wale sio binaadam? binaadam ni huyo kibaraka pekee?

Nasema astahili yake, mtoto akichezea wembe mwachie, na bado.

Sasa kwa kumuumiza huyu ndio vifo havitatokea au idara ya afya itakuwa bora? Jiangalie na jiahtukie, hata mkiua nusu ya watanzania bado tutawang'oa tu mafedhuli kazi kuiba tu na kwenda kuficha hela nnje kwa ubinafsi wenu.
 
hii ni habari ya kweli na imetoka kutangazwa sasa hivi na radio Clouds Fm.... Serikali dhaifu, madakitari kuweni kitu kimoja mgomo kama kawa hadi kieleweke.
 
Sasa tutaogopa......ukiwa mwanaharakati wa kupigania hari ya wanyonge shida tupu....!

Ukipigania haki, utakuwa salama. Lakini ukipigania upuuzi, kamwe waathirika wa upuuzi wako hawatakuacha.
 
Mkuu una akili vizuri?????
Kama huna cha kuongea si ukae kimya??
Selikari yako ingetambua hilo ingemaliza matatizo ya ma doctor kistaarabu kabisa!

zomba nahisi mnala umekaa tenge jirekebishe.je ungekuwa wewe ni dk mgonjwa anafia mkononi kwako kwa kukosa wembe wa opp akiwa kalala chini ungefanya nini?
 
Wewe uko sawa kweli ? au unafikiria kwa kutumia majani ya matembele ?
endelea kuwa mpumbavu vile umeamua kuishi hivyo, hata gadafi na wengine wa aina hiyo walisema kama unavyofanya lakini mwisho ulifika kwao na vizazi vyao, hilo ndio jambo la kusikitisha n kuogopa lisikukute kwa mtu mwenye akili sawa sawa, unasababisha generation yako kishi kwa shida for the rest of their life.
wenzako wanaofanya kazi hii unayofanya huwa wanaacha baada ya muda fulani si mrefu, kuepuka haya unayofanya wewe hapa jf, endelea majuto ni mjukuu...
 
Nime-bahatika kumuona Dk. Steven Ulimboka kupita Clouds TV saa 9.30 akiojiwa na wanahabari mara baada kufikishwa Muhimbili: kwakweli inasikitisha sana na Madaktari wenzie inabidi wafanye kazi ya ziada kuweka sawa afya yake, umeumizwa vibaya sana uso mzima ikiwemo na kung'olewa meno. ''duh! very painful''.
 
Wadau,
Habari ndiyo hiyo.

"Jamani this is iserious nimepigiwa simu sasa hivi na watu wa legal and human rights center wameniambia wametoka kumchukua Dr Ulimboka kule Mabwepande amepigwa vibaya sana na ni emergency wanampeleka MOI sasa hivi please tunaomba mtume habari hii kila mahali please!
Ni habari ya uhakika sana nimeomngea na Patience Mlowe wa Legal and Human Rights center"".
By Dr. Riwa

1) Hao wanaojiita human rights walijuaje kama yuko huko?

2) Hao wanaojiita human rights hawaoni wagonjwa wanaoteseka? mbona hatujawasikia kuwatetea?

3) MOI si tunasikia wamegoma? kulikoni?
 
Acha upumbavu wako bana, sasa unaweka hiyo orodha ya kazi gani. Watu wanachangia mambo ya maana we unaweka orodha lisilo na tija humu.
 
Serikali legelege na dhaifu iliyoshindwa kutawala, hutumia mabavu ili kuendelea kutawala kwa nguvu,

Huku kuchukuana usiku na hao wanaitwa usalama wa taifa, sikuwahi kufikiri kama sikuku moja tutakuja kufika hapa,

Mungu atusaidie tujihurumie,
 
Hana maana huyu hata akifa hakuna wa kumjutia,wangapi wanakufa huko hospitali tena nchi nzima kisa yeye anapingana na serikali tena kwa maslahi binafsi,anapinga mpaka amri ya mahakama hana adabu kabisa,wangemalizia kabisa tujue moja.sina roho ya huruma kwa mnyama/chizi/!!!!!?????? shenz..... kama huyu asiyethamini maisha ya wenzake bora angetangulie yeye akadai hayo maslahi huko kuzimu.
Nadhani wewe ndo huna maana tena kabisa,tatizo ni madaktari kukataa kufanya kazi au ni serikali kukataa kutimiza wajibu wao?Mafisadi wanataka kula kodi wenyewe sasa huo upuuzi hatuutaki,kodi tunalipa wenyewe wao wale peke yao.MADAKTARI UNGANENI MHAKIKISHE HAMRUDI KAZINI HADI WALIOFANYA HUO UNYAMA WAFIKISHWE MAHAKAMANI AKIWEMO SURA MBOVU
 
Huyu Doctor ameonyesha udhaifu mkubwa....kwa nini aliitikia wito wa hawo jamaaa ? alitegemea nini kwenda kufanya reconciliation saa 6 usiku ? au walimuahidi kitu?
 
Mimi ninachosema ni kwamba nimesikitika sana na kipigo alichopata Dkt Ulimboka. Aidha nilisikitishwa zaidi na kitendo cha Dkt Ulimboka kutokutii amri halali ya mahakama inayobatilisha mgomo na kuagiza atekeleze agizo hilo kwa kutoa msimamo kwenye vyombo vya habari. Kitendo cha kugoma, licha ya kwamba Mahakama ishatoa agizo; na pia sentiments zilizotolewa na watu/makundi/asasi/taasisi mbalimbali kimetoa ishara kuwa MAT haikuwa tayari kuingia katika majadiliano, na wameamua kutumia nafasi yao kama watabibu kuwaadhibu wanaowatibu ili kuonyesha misuli yao kwa Serikali. Kutafsiri kuwa Serikali ndio inahusika na shambulio kwa Dkt Ulimboka ni jambo ambalo sikubaliani nalo kwa sasa, mpaka ushahidi upatikane utakaoonyesha bayana kuwa Serikali imehusika. Inawezekana Dkt Ulimboka alikusudia kwenda kutekeleza agizo la mahakama, lakini mahafidhina wachache MAT wakaamua kumshughulikia ili kutoa taswira nyengine. Inawezekana pia kuwa kuna watu wana uchungu kuona Watanzania wasio na hatia wanateseka kutokana na mgomo ambao tayari mahakama ya nchi imeuita batili wamechukua hatua mikononi mwao; au kuna masuala ya ugomvi wa Dkt ulimboka nje ya mgomo ambayo yametekelezwa na wabaya wake ili kuficha taswira hiyo. MAPENDEKEZO YA KISIASA KATIKA SUALA HILI, hususan ya kuitisha maandamano sio masuala ya kushabikia kwa sasa. Tuangalie dhahma zinazoendelea Syria na uharibifu wa mali na upotevu wa maisha tujifunze. Kwa sasa Tanzania tunapaswa tuiheshimu sana serikali yetu na kuipa SUPPORT ili tuweze kupata KATIBA MPYA. Masuala ya kuleta vurugu yataturudisha nyuma miaka 500.

Mwisho kabisa, namtakia Dkt ulimboka matibabu mema na apone haraka ili aje kutusaidia katika tiba ya nchi na uongozi wa MAT; na kuwasihi wanachama wa MAT wasigome, na wamuhudumie Dkt Ulimboka na Watanzania wengine sawia.

Wakatabahu
 
Back
Top Bottom