Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Huyu Doctor ameonyesha udhaifu mkubwa....kwa nini aliitikia wito wa hawo jamaaa ? alitegemea nini kwenda kufanya reconciliation saa 6 usiku ? au walimuahidi kitu?

Mkuu inasemekana huyu bwana alikuwa anawasiliana naye mara kwa mara na ndio maana hakuwa na wasiwasi !
 
Naomba tuwekee ushahidi hapa kuwa Serikali inahusika; hili ni jukwaa makini

kuna thedi umeletwa humu bi helen Kijo Simba anaeleza mazingira ya kutekwa dr Ulimboka.!
 
Sintashangaa kusikia Ikulu inalaani kitendo hiki, kumpa pole na Mkulu kumtembelea hosp. maana huo ndio mwisho wao wa fikra!
 
Kama madaktari wapo serious na mgomo basi wasimtibie huyu Dr Ulimboka

Madaktari mabingwa walibaki mahospitalini lakini baada ya usalama wa taifa kudharau hata huo uwaamuzi sasa hivi ni full tools down mortuary to labour ward wait and see
 
Hakika hili nalo linaonyesha jinsi serikali yetu imeishiwa kifikra mpaka suluhisho linakuwa hilo.kama kweli ni mkono wa serikali basi pia hiyo damu itawafuata ni muda muafaka wa kusema bye magamba.Ni heri kufa kuliko kendelea kuishi katika hofu na udhalimu wa jinsi hii.


NDIO WALE WALE WENYE KUTAKA KUNYOOSHEA KIDOLE SERIKALI BILA YA USHAHIDI. KWANZA NDIO KWANZA UNA POSTS TATU; TAmbaa au weka vitu vyenye akili.

Hili sio jukwa la kushushia pumba
 
Napata shida kidogo kwamba nikupe pole wewe au wale wagonjwa ambao kwa lengo lenu la kugoma na kuiwajibisha serikali wengi wanateseka,wengine wanakufa,mama zetu wanajifungua kwa uchungu bila ya kua na msaada wowote,haya ni mateso makubwa,
Hemu tujiulize vipi kama ulimboka na yeye kama akitelekezwa aachwe bila ya huduma yoyote?
ni vyema madaktari watafute njia tofauti yakuibana serikali kwani watanzania wasio na hatia wanakufa kwa kosa la serikali

duplicate c_rap
 
Kama ni kweli hii habari basi lazima nitamke wazi kwamba serikali haiwezi kufanya jambo la kipuuzi kama hilo wakati madhara ya upuuzi kama huo yapo wazi. Kwa vyovyote vile, hiyo inaweza kuwa ni ama hujuma dhidi ya serikali, au hujuma dhidi ya kiongozi wa nchi au mchezo wa kitoto uliofanywa na madaktari wenyewe, au wabaya wa Ulimboka mwenyewe.

MCHEZO WA KITOTO WA MADAKTARI:
Kikundi kidogo cha madaktari wenyewe wanaweza ku-engineer mpango wa kipuuzi kama huo ili kutafuta huruma ya wananchi.
Michezo ya kitoto kama hii inafanywa sana na huwa inaaminiwa na wale wasio na uwezo wa kuchanganua mambo.

HUJUMA DHIDI YA SERIKALI:
Watu wenye maslahi tofauti dhidi ya serikali wanaweza kufanya upuuzi kama huo ili kujenga picha kwamba serikali iliyopo ni ya kidhalimu inayoweza kufanya lolote dhidi ya raia wake wanaotetea maslahi yao. Watu wanaoweza kufanya haya ni wale wenye maslahi ya kisiasa...ni Political Sabotage.

HUJUMA DHIDI YA RAIS:
Ulingo wa siasa ni ulingo uliojaa uadui baina ya mtu na mtu. Katika hilo, mtu au kikundi cha watu wanaweza kufanya upuuzi kama huo ili kumuumbua kiongozi mkuu wa nchi.

MAADUI BINAFSI WA Dr. ULIMBOKA MWENYEWE: Hawa wanaweza kutumia opportunity ya Dr. Ulimboka kuwa ndani ya mgogoro ili ionekane kwamba waliomdhuru ni watu wa serikalini.

MOJA kati ya hizo inaweza kuwa ndio sababu sahihi lakini there's no way kwamba serikali inaweza kufanya utoto kama huo. Ki


Nikweli kabisa naungana na wewe pia. Ila umeruka moja.
SERIKALI
Inawezekana kabisa watumishi wa serikali (wanausalama/polisi) wakayafanya haya hata kama hawajaagizwa hilo. Tumekuwa tukishuudia watu wa usalama wakifanya mambo kinyume cha haki za binadamu/Katiba yetu na bado hakuna mkono unaoweza kuwagusa. Ni mapema sana kuhukumu kwasasa, tuombe Mungu Dr.Ulimboka apate nafuu upesi ili asaidie kupatikana kwa taarifa kamili kuhusiana na tukio hili.
 
Ndo hapo sasa, madaktari ni wajinga na kisomo chao hakijawanufaisha. Hao wasiopatiwa matibabu wana tofauti gani ya utu na madakatari watakaotibiwa wakati wa mgomo? Au wao wakienda kukata gogo wanalikata huku wamesimama? Kama hawana tofauti, kuna faida gani kuruhusu watu kufa kwa kukosa matibabu ili hali kundi flani likinufaika na huduma hiyo nyeti. Ndo tuseme madai ya madaktari ya kupatiwa vitendea kazi yameshakamilishwa na ndio maana wanamtibia Dr Ulimboka? Kama bado, wamepata wapi vifaa wanavyotumia kwa sasa kumtibia huyo kiongozi wao wa mgomo?
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
 
Inasikitisha sana! Get well soon Dr. Ulimboka!
 
Join Date : 13th February 2012
Posts : 15
Rep Power : 323
Likes Received0
Likes Given0

Munapoambiwa hamna akili hamjielewi huu mugomo ulikuwa quarter of the country sasa hivi mandondocha nyie mumeusambaza nchi nzima kwa maamuzi yenu ya kijinga
 
napata shida kidogo kwamba nikupe pole wewe au wale wagonjwa ambao kwa lengo lenu la kugoma na kuiwajibisha serikali wengi wanateseka,wengine wanakufa,mama zetu wanajifungua kwa uchungu bila ya kua na msaada wowote,haya ni mateso makubwa,
hemu tujiulize vipi kama ulimboka na yeye kama akitelekezwa aachwe bila ya huduma yoyote?
Ni vyema madaktari watafute njia tofauti yakuibana serikali kwani watanzania wasio na hatia wanakufa kwa kosa la serikali
kunamashetni hu jf.huyu nae ni pepo.
 
Ukweli wana JF, hapa nipo machozi yananitoka. Mimi siyo Dr, ila naamini madai ya hawa wenzetu ni ya kweli na serikali ni wahuni. Je kwa hali ilivyo kwelu JK atatoa pole? Na je atamtembelea? Je jeshi la polisi na hao serikali wataenda kutibiwa wapi?
 
Watanzania tuamue tusikubali mtetezi wa wanyonge afanyiwe hivyo hivyo ni vitisho kwamba wanyonge tuogope kudai haki zetu, Kikwete aelewe kuwa naye ni binadamu ipo siku moja naye ataonja mauti licha ya kuwa na jeshi. Suluhisho si kutisha, kupiga, kukimbilia mahakamani na kuua bali ni kutatua matatizo ya watanzania. ITAMFAA NINI MTU KUUPATA ULIMWENGU WOTE LAKINI AJE APATE HASARA YA NAFSI YAKE. VIONGOZI MWOGOPENI MUNGU, NANI ASIYEJUA WANASIASA MNAJIPENDELEA MNO KIMASLAHI. HUKU MKIJUA BILA MWALIMU MSINGEKUWA HAPO NA BILA MADAKTARI MNGEKUWA NA AFYA. AU KWA VILE MNATIBIWA NJE NA KUSOMESHA WATOTO NJE. WALIMU KARIBU TUTAGOMA TUPIGENI TU NA KUTUUA MKITAKA. WABUNGE WA CCM ACHENI KUUNGA MKONO KILA UPUZI WA SERIKALI, JESHI NA MAHAKAMA ACHA KUPINDISHA UKWELI MBONA NYIE PIA MNA NDUGU ZENU WANAUMIA. PESA ISIWE KILA KITU KWENU.
 
NI kweli usalama wa taifa wamefikia hatua ya kushindwa kutumia njia zote wanazoweza kutumia kuzuia mgomo hadi kumpiga mtu huyu? Jamani who is criminal mwizi wa fedha za umma au anayedai nyongeza kutokana na kazi halali anayofanya?

Kama ni usalama wa taifa, ipi kazi bora kuzuia wizi wa mabilioni ambayo yanaweza kusaidia kuongeza mishahara ya walimu na madaktari, au kulinda wezi na kuwapiga wasio wezi?

Jeshi likigoma na kudai nyongeza ya mishahara ntakuwa wa kwanza kuliunga mkono, huenda usalama wa taifa watashindwa kuwapioga wanajeshi.
 
Kabla madaktari hawajaacha ujinga, wewe acha upumbavu wako. Inaelekea hujui wanachokidai madaktari ndiyo maana unaamua kutoa hovyo uharo wako.
 
nyie ni maiti zinayotembea. Hamjui mtendalo. Mngekaa kule serengeti na nyani na masokwe. Ulimboka atatibiwa na mapambano yanaendelea. ****!!!!!
 
Back
Top Bottom