Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

hii ni habari ya kweli na imetoka kutangazwa sasa hivi na radio clouds fm.... Serikali dhaifu, madakitari kuweni kitu kimoja mgomo kama kawa hadi kieleweke.


huyu ndio kwanza ana post moja

kwanini mnapenda ku cook mambo?

Au ndio nyinyi mliomdhuru ulimboka alafu mnataka serikali ionekane imefanya uhuni huo???

Serikali sio huni
 
Acha kutumika kisiasa wewe'ww unasema hawana vifaa mbona huyo ulimboka wampeleka Moi under emergency case na vifaa hivyo hivyo ndio wanamtibia navyo? kama hakuna vifaa kwa nn wasinge mpeleka nje au hospitali binafsi ? fumbuka bongo , hapa yaonyesha haya madai yao ya vifaa ni janja yao tu, wako kimaslahi zaidi . Mie nasema ni bora tuwafukuze wote tujue hatuna madaktari kama walivyo fanya kenya , kuliko kuwa na madaktari kanjanja

Akili yako ndipo ilipofikia huwezi kufunguka zaidi ya hapo ulipofikia ila iko siku utafunguka na kujiona ulikuwa usingizini na umechelewa kuamka.Nakusikitikia sana kwani unapotea hivihivi ukijiiona.

Wafukuzeni kwani mnashindwa nn kulifanyahilo tangu mwanzo kinachowachelewesha ni nini??
 
Nikweli kabisa naungana na wewe pia. Ila umeruka moja.
SERIKALI
Inawezekana kabisa watumishi wa serikali (wanausalama/polisi) wakayafanya haya hata kama hawajaagizwa hilo. Tumekuwa tukishuudia watu wa usalama wakifanya mambo kinyume cha haki za binadamu/Katiba yetu na bado hakuna mkono unaoweza kuwagusa. Ni mapema sana kuhukumu kwasasa, tuombe Mungu Dr.Ulimboka apate nafuu upesi ili asaidie kupatikana kwa taarifa kamili kuhusiana na tukio hili.

Inasikitisha kwa ili lililotokea!Sina sababu ya kua na shaka ya kua hapa mkono wa serekali umehusika kwa sababu nyingi kwanaza mpaka sasa serikali iko kimya inatayarisha uongo hata kama askari wa usalama wa raia wamefanya vitendo hivyo iko wapi kauli ya serikali angalau kusema inafanya uchunguzi,pili blogs zote ambazo ziko karibu na serikali ambapo wakati wote utoka na breaking News au nyuziii kama wanavyozihita wenye ambazo sitaki kuzitaja mpaka sasa ziko KIMYAAAA! MUNGU AMBARIKI NA KUMRUDISHIA AFYA YAKE MAPEMA DUA ZETU ZIKO NYUMA YAKO.
 
propaganda za kichina peleka kwa mjomba wako hamna maana usalama wa taifa dege la qatar limekuja hapa limebeba wanyama nyie mumekaa munakata makinda makinda ,mara reli imeuzwa kwa wahindi mabovu kazi kunywa juice mara bandari imeuzwa kwa walebanoni kazi kuburura miguu nchi mumeuza nyie kwa tamaa zenu za pesa acheni watanzania waonyeshe hasira zao kwa serikali dhaifu
 
Alivyo mnafiki,ataenda kumtembelea.
Mbona kwa kw kubenea alienda.mawazo mtazamo matendo vyote dhaifu,mpuuzi sana
 
Sipendi kusema hovyo laikini kwa hili napenda kumshauri Babb-babbjrtz akatawaze maana posting yake inanuka uharo!
 
Nadhani hawa watu waliomfanyia hivi walifikiri ameshakufa ndio maana wakamwacha. Wakijua kwamba bado yuko hai kuna uwezekano mkubwa watarudi ili kumalizia asije akawataja atakapopona. Kuna uhitaji mkubwa sana wa kuhakikisha anapatiwa ulinzi wa uhakika. Haya ndio yaliyosabisha kiongozi wa serikali ya wanafunzi miaka ya hapo nyuma, Harun Kimaro, atoroke nchi na kukimbilia Zimbabwe baada ya kupata taarifa uhai wake ulikuwa hatarini toka watu wa vyombo vya "usalama" vya serikali.

hilo nalo lipo maanake hakuna mantiki ya kumwacha akiwa hoi kiasi hicho.
 
Mleta uzi huu anaonyesha ni mzandiki na ni mmbia wa serikali ya CCM! Ulimboka sio taasisi, kipo chama cha madaktari kinaitwa MAT ndicho chenye maamuzi! Ulimboka hakusema huduma zisitishwe, ni taasisi ynayotetea maslahi ya matabibu. Hta hivyo kumuua mtetezi wa haki za wafanyakazi sio jibu la mgomo! Ni sawa na kuwasha petroli! Naam, huu moto hautazimwa! Wazandiki kama nyie ambao mnaujua ukweli na kujifanya hamnazo siku si nyingi wakati utawambia badilikeni pasipo kujijua!
 
Sasa watanzania wote ni lazima tuungane maana sasa hawa mafisadi wanataka kufanya nchi hii kama ni mali yao. Waliua wenzetu wafanya biashara wa Mahenge tulikaa kimya!, walimfanyia mbaya kubenea na wenzake tulikaa kimya! walifanya the same na kuua Arusha wakati wa maandamano ya CHADEMA tulikaa kimya! mpaka mtoto wa mkulima alidanganya bunge tulikaa kimya! Mwakyembe pia kimya! na kwingineko Mara kwenye migodi tulikaa kimya!---SASA BASI TUNAHITAJI KUAMKA NAKUSEME NO NO - MKUU WA KAYA NCHI IMEMSHIDA
 
We (Ngida) ndo nyani na punda kabisa, unafikiri madaktari wakitimiziwa kila kitu ndo yatakwisha? Na walimu nao watasemaje baada ya hapo, Wamuache nae apate machungu ya wagonjwa wanayoyapata pale, Kama una ndugu zako Hospitali sidhani kama ungeshabikia mgomo
 
Kuna tetesi kuwa kiongozi wa mgomo wa Madaktari aokotwa pande akiwa mahitihuti! Kama habari hii ni ya kweli basi tunakoelekea siko! Ipo siku mafisadi wataburuzwa barbarani!
 
Kwanini simtembelee? kwani huyo dokta sio mtanzania?

JK rais mpenda watu ataenda kumtembelea regardless, lakini huyo dokta aeleze ukweli kilichomfika. Isije kuwa amekamatwa ugoni anasingizia usalama wa Taifa. Wewe inakuwaje unaenda kuzungumza na watu usiwafahamu halafu mnakaa kabisa mezani? There must be something hapa na soon tutajua
 
Huyo Dr Ulimboka atakuwa ni mla rushwa (CORRUPT) sana na inavyoonekana anaweza kuwauza wenzake.Nasema hivyo kwa sababu ukiiangalia hii incidence unaona kuwa huyu Dr Ulimboka ana tamaa ya pesa na anaendesha mgomo kwa kushawishi wenzake ili anufaike binafsi.Nasema hivyo kwa sababu hebu fikiria kwa akili ya kawaida tu,wewe una ishu kubwa kama hiyo ya mgomo,halagu unaitwa na mtu usiyemjua ili mkafanye reconcilliation.Bila shaka ni reconcilliation kuhusu mgomo.Hapo naona kuwa anaweza kuitwa na kupewa kitu kidogo na watu asiowajua na yeye akaenda tena peke yake???!!!!!!.Baada ya hapo anaweza kuwageuka wenzake.HAFAI KABISA ANASUMBULIWA NA TAMAA NA NJAA TU.
 
Back
Top Bottom