Duh! Maskini ya Mungu!!! Hii Serikali ya wauaji...Inatisha sana. Halafu watu wanasema tutumie majina yetu ya kweli hapa JF!!! Mnaona jinsi Serikali hii inavyoweza kabisa kumaliza uhai wako kwa kuandika ukweli jinsi ambavyo imeshindwa kukidhi matumaini mbali mbali ya Watanzania...Sasa kila atakayeipinga ajue maisha yake yako hatarini anaweza kabisa kukolimbwa!!! Pole sana Ulimboka na madaktari wengine wote kwa tukio hili la kusikitisha na kutisha.
Kweli inasikitisha hiki kitendo walichomfanyia.
Kwa kusema kutotumia majina ndio mtu huwezi julikana hiyo sio kweli, admin wa JF au niseme forum yoyote wana access ya juu kwa mtu anaye jiregister katika forums.
wanaweza mengi, kujua IP address uliyojiungia, wapi unalog in toka, kulink username yako na e-mail (wengi hutumia majina), ni kuwa ukijiunga u basi umewapa ruhusu ya kukujua weye. wengi ukigoogle e-mail zao utakuta majina etc, au hata kwenye facebook kama wapo public utapata kuona profile zao etc. hii kitu inatumika na wengi hata kwenye maofisi kumjua mtu etc
hata mtu uwe Musoma utume ujumbe unajifanya upo Mbeya wakitaka angalia wanajua ukweli.
Cha umuhimu ni kuamini kuwa hawa admin na owners wa forum hawata angukia kupokea pesa za kuongwa ili kutoa data za watu. wanaweza block ip address ya mtu, kwa hiyo mtu inajulikana ni hadi wapi wanaweza fika.
Ndio maana ni muhimu sana owners wa forums kutoa access kwenye sensitive data kwa watu wanaowaamini, humu kuna mods I guess sidhani kama wanawajua wote kiundani as na ma spy wanaweza kuwa wamo. kitu cha michango ya pesa nyingi isifanye wakadhani kuwa hao ndio watakatifu.
mtu anaweza kutumia pesa kupata anachotaka hata kama itawachukua miezi, miaka bali wajilinde na mambo or maisha yao.
ukitaka leta nyaraka na unajua utakuwa huru bila kufatwa au kuwa na wasi basi ni...
kutumia connection ya internet isilink na home kwako, kazini au unapokuwepo mara nyingi, zile za kununua kwa mwezi, fungua e-mail account tofauti, ingia kwenye forum ujisajili thne rusha mambo.
tabu humu wengi wana fikira ndogo wakiona mtu kajiunga siku hiyo au siku chache zimepita wanadhani mambo yanayoletwa ni mchezo hawajui ujanja wa kutumia mitandao.
haya I hope wenye mambo watarusha wakitaka kusaidia nchi yetu.