Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana


Mbona na wewe unatutisha .... sisi tukiumwa tutakuja muhimbili...mkigoma kutuhudumia tunateka mwengine ....tuna msulubisha...halafu tunaenda kutupa Mabwepande.....Hali itaendelea hivi mpaka muishe wote...kisha tunahamia katika tiba za jadi
 
Subiri siku mamako akufie mikononi mwako pale mpokezi muhimbili huku Ulimboka na wenzake wako pembeni wanakuchekea chekea etu wamegoma ndio utajua watu wanazungumza nini pia utasema kile kipigo hakikumtosha..

Kama hujui kwa nini wanagoma kaa kimya usikurupuke kuchangia,na sina haja ya kukuambia kwanini maana naamini hutaelewa, ila ukae ukijua kila kazi ya mtu sharti iheshimiwe
 
ni kweli kabisa,lakini naamini siku moja inaweza ni zaidi ya mia moja.ipo siku,yaani inauma sana,natamani ningekuwa nipo tanzania kwa mda,then after ntarudi nyumbani bt,nyumbani ni hapa.
 

Usiwe na hofu tukijipanga tunawazidi hao UWT
 
Kusanya data ndipo uje kuchangia, Jibiidishe kupata habari then uje kuchangia. Serikali haikuwa na dhamila ya dhati kutatua mgogolo huu. Serikali haina cha kujitetea katia hili. Ukombozi unakaribia, CCM na serijkali yake ni wauwaji, wameshauwa wengi.
 
Naona Kikwete ameshindwa na kazi tuliyompa. Kwa nini tusitumie mtandao kuita maandamo ya nchi nzima?

Hawa watu wanaotetea serikali kwenye hii blog ni vizuri tuwajue. Tutakapomaliza kuchukua nchi baada ya maandamano makubwa lazima nao wakamatwe maana hawana adabu kabisa, wangekuwa karibu hapa ningeweza kurusha ngumi mafisadi makubwa na wala jasho la watu nyie. Ni vizuri maandamano yaanze wakati huu ambao rais anaondoka maana hii nchi si yake kabisa.

Mungu ibariki Tanzania. Naomba kutoa hoja wakubwa.
 
Polisi wameshindwa kumpeleka majeruhi hospitali mpaka wapigie simu LHRC??????

To this we have to get a statement from LHRC; watuambie ilikuwaje, sio reported speeches zinazoletwa hapa.

LHRC MPO???

Kama unafanyia assignment yako hapa acha, tafuta njia mbadala
 
Vitisho vina ukomo, hata vya Ghadafi vilifika mwisho. Ni kweli Dr. Ulimboka katekwa na kaumizwa vibaya sana. Madaktari tusiogope vitisho, haki haipatikani kwenye sahani
 
ni kweli kabisa,lakini naamini siku moja inaweza ni zaidi ya mia moja.ipo siku,yaani inauma sana,natamani ningekuwa nipo tanzania kwa mda,then after ntarudi nyumbani bt,nyumbani ni hapa.

Kwa nini hiyo siku isiwe leo au kesho? Au watanzania tunasubiri waje wazungu kutusaidia kuondoa viongozi dhaifu serikalini. Inauma sana kuona Tanzania ikibakizwa mifupa tu wakati huo nyama yote inamalizwa. Sijui wajukuu zetu watakuja wapate hata hiyo mifupa kweli.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
 
haya ni madhara ya kuweka watu wadhaifu wa kufikiri katika DOLA,
ni matokeo ya kuwa na watoa maamuzi wanaotumia mak***o!
very sad kwa nchi inayojifanya inahubiri demokrasia!
mbona wanaochochea vurugu huko Z'bar hawajatekwa
wala mapapa wa rushwa wanaodaiwa na HOSEA kuwa wakodip sea wamewashindwa!
KWA HAKIKA MADAKTARI SASA KAZENI KAMBA..ILA TUTAUMIA JAMANI!!!
 

Mkuu unaushahidi wa serikali kuhusika kwenye hii ishu?Ni jukwaa la Great thinkers hili habari za porojo za vijiweni hazina nafasi hapa.Kama una ushahidi tuwekee hapa then tuendelee kuchangia.Otherwise piga kimya tusubirie taarifa zaidi kutoka vyanzo mbalimbali vya uhakika.
 
Idi amini amefufukia Tanzania? Duhhhhhh

wazo lako kama lakwangu, nahisi kama idd amin amerudi tanzania kwani mauaji yanayohusiana na siasa yanaongezeka huku sirikali ikichukua hatua za taratibu na ambazo moja kwa moja zinaonyesha kuwa inahusika na mauji haya. Watu wote ambao wamekuwa msitari wa mbele kupinga namna serikali ya ccm inavyoendeshwa moja kwa moja au kuipinga ccm wamekuwa hatarini.
 
Aisee kama Serikali haioni kama hii sio sawa basi tumekwisha!

Yaani inafikia hatua ya kupiga mwananchi wake na mtaalamu anayehangaikia kuboresha huduma za Afya na Maslahi yake kiasi hiki! Madaktari kazeni kamba!

Kiganyi, JF.
Health - Wotepamoja
 
serikali hii always employ wrong tactic, sasa wanadhan madaktari ni watoto wadogo wataogopa na kurudi kazini bila kinyongo kwa kigezo cha kuogopa? what a mistake! i think hii ni motivation kwa madaktari kuendelea na mgomo tena in a more intense way!
 
Wazungu watakujaje kutusaidia wakati ndo waiba madini na kutia sumu kwenya maji huko vijijini ?....Watanzania huwezi kuwafananisha na walibya au wamisri wengi wao wanaogopa kwenda kutupwa Mabwepande
 
Kama unafanyia assignment yako hapa acha, tafuta njia mbadala

Wewe unajiita Wewe BABA? Siwezi kukujibu kwa lugha ya Jazba wala hasira; assignment gani hiyo?

Mimi nimeuliza hapa; Polisi ikipata mtu kajeruhiwa au kufariki wanatakiwa wachukue hatua gani? Wanatakiwa Kupiga SIMU LHRC?

Let us be realistic.

Na pia kama huna mchango, tafadhali usiweke matapishi Jukwaani.

Assignment inafanywa JF?

You need mental treatment
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…