Kama kusingekuwepo na Mungu udhalimu ungedumu na kuumiza wanyongewengi. Lakinini kwa sababu kuna Mungu Mkuu, mwenye nguvu, uwezo, hekima, haki na hapatikani na mauti milele, haki itashinda na kusimama.
Dr Ulimboka kama ana kosa angekamatwa na kufunguliwa mashitaka. Au angewekwa kizuwizini lakini akiwa hai na salama. Kitendo cha kumpiga, kumvunja mbavu, mikono, meno, shingo, na kung'oa kucha zake, ni zaidi ya matendo ya mtu mjinga na mpumbavu. Watu wanaokubali kujisalimisha mikononi mwa mwovu ndio wanaweza kufanya vitendo hivi.
Tuhuma kwa serikali...
(1) Serikali yetu na uongozi wake vimetuhumiwa kuhusika lakini pasi na ushahidi thabiti
(2) Ushahidi wa mazingira unaonesha kwa kiwango kikubwa kuwa imehusika
Lazima serikali ijitakase kwa haraka na kulifanyia uchunguzi jambo hili kwa haraka na kutoa taarifa mbele ya watu na jumuiya ya ulimwengu. Jambo hili ni baya mbele za bin-Adam na mbele za Mwenyezi Mungu.
Mgomo wa ma-Daktari.. (una mitizamo miwili)
(1) Unaumiza watu wengi wa taifa hili na hivyo inasikitisha sana, lakini ..
(2) Mgomo huo, unatetea maslahi makubwa ya afya za wananchi wote wa taifa letu. Wanaikumbusha serikali kuboresha vitendea kazi, mazigira ya kazi, na maslahi ya matabibu. Haya pia ni muhimu. Bila hivyo ma-Daktari wakuwa watu wa kushuhudia watu kufa tu na siyo kuponya watu. Kwa maana hiyo vifo vya wagonjwa vinawezekana kwa njia ya mgomo wa madaktari au kwa mgomo wa serikali kuboresha vitendea kazi.
Ulinganifu wa wan-Taaluma na wana-Siasa ...
(1) Wana taaluma ni watu waliosoma ili kupata taaluma ya kutumikia taifa letu. Hawa ni watu adimu na ni ghalama kubwa kuwatayarisha. Serikali inatakiwa kuwa nao karibu na kutowanyanyasa
(2) Wana siasa katika nchi hii (waliosoma na wasiosoma) mara nyingi wamekuwa na nafasi kubwa ya kujipatia pesa nyingi kupindukia. Sababu ni hizi:
- Wao wanapewa mishahara minono zaidi na mara nyingi wanaongezewa mara kwa mara
- wao hujipatia mapato ya ziada kupitia mikataba ya serikali.
- Wao wanalipwa vizuri zaidi kwenye vikao na semina za mara kwa mara
Serikali iwasikilize wanataaluma wote, wakiwemo waalimu, madaktari na wanasheria. Bila kufanya hivyo nchi itazidi kulegea katika sekata ya elimu, afya na sheria.
Mwisho naomba Mungu amponye kijana huyu, Dr Ulimboka ili aendelee kuongoza harakati za madai ya sekta ya afya.