Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Naona wanasiasa mmeshaanza ku take advantage ya kutekwa kwa huyo DR.against government,kuweni wavumilivu mpaka ushahidi upatikane
 
Kama kusingekuwepo na Mungu udhalimu ungedumu na kuumiza wanyongewengi. Lakinini kwa sababu kuna Mungu Mkuu, mwenye nguvu, uwezo, hekima, haki na hapatikani na mauti milele, haki itashinda na kusimama.

Dr Ulimboka kama ana kosa angekamatwa na kufunguliwa mashitaka. Au angewekwa kizuwizini lakini akiwa hai na salama. Kitendo cha kumpiga, kumvunja mbavu, mikono, meno, shingo, na kung'oa kucha zake, ni zaidi ya matendo ya mtu mjinga na mpumbavu. Watu wanaokubali kujisalimisha mikononi mwa mwovu ndio wanaweza kufanya vitendo hivi.

Tuhuma kwa serikali...

(1) Serikali yetu na uongozi wake vimetuhumiwa kuhusika lakini pasi na ushahidi thabiti
(2) Ushahidi wa mazingira unaonesha kwa kiwango kikubwa kuwa imehusika

Lazima serikali ijitakase kwa haraka na kulifanyia uchunguzi jambo hili kwa haraka na kutoa taarifa mbele ya watu na jumuiya ya ulimwengu. Jambo hili ni baya mbele za bin-Adam na mbele za Mwenyezi Mungu.

Mgomo wa ma-Daktari.. (una mitizamo miwili)

(1) Unaumiza watu wengi wa taifa hili na hivyo inasikitisha sana, lakini ..
(2) Mgomo huo, unatetea maslahi makubwa ya afya za wananchi wote wa taifa letu. Wanaikumbusha serikali kuboresha vitendea kazi, mazigira ya kazi, na maslahi ya matabibu. Haya pia ni muhimu. Bila hivyo ma-Daktari wakuwa watu wa kushuhudia watu kufa tu na siyo kuponya watu. Kwa maana hiyo vifo vya wagonjwa vinawezekana kwa njia ya mgomo wa madaktari au kwa mgomo wa serikali kuboresha vitendea kazi.

Ulinganifu wa wan-Taaluma na wana-Siasa ...
(1) Wana taaluma ni watu waliosoma ili kupata taaluma ya kutumikia taifa letu. Hawa ni watu adimu na ni ghalama kubwa kuwatayarisha. Serikali inatakiwa kuwa nao karibu na kutowanyanyasa
(2) Wana siasa katika nchi hii (waliosoma na wasiosoma) mara nyingi wamekuwa na nafasi kubwa ya kujipatia pesa nyingi kupindukia. Sababu ni hizi:


  • Wao wanapewa mishahara minono zaidi na mara nyingi wanaongezewa mara kwa mara
  • wao hujipatia mapato ya ziada kupitia mikataba ya serikali.
  • Wao wanalipwa vizuri zaidi kwenye vikao na semina za mara kwa mara

Serikali iwasikilize wanataaluma wote, wakiwemo waalimu, madaktari na wanasheria. Bila kufanya hivyo nchi itazidi kulegea katika sekata ya elimu, afya na sheria.

Mwisho naomba Mungu amponye kijana huyu, Dr Ulimboka ili aendelee kuongoza harakati za madai ya sekta ya afya.
 
Sitaki kuamini kama Serikali inaweza ikawa imecheza mchezo huu. Nijuavyo kama Serikali ingetaka kumuua Ulimboka ingemuua kwa njia ambazo hakuna kati yetu ambaye angeweza kuifikiria kuwa Serikali imemuua Ulimboka. Hao watakuwa ni miongoni mwa wenyewe kwa wenyewe. Maana tayari inasemeka kuna makundi kati yao
Agreed with you, pia wasingefanya operation ya kipumbavu hivyo! Tutajua ukweli, Get well soon Dr. Ulimboka
 
Yafuatayo yanawezekana kwa harakaharaka;
  1. Yaliyomkuta Ulimboka ni kama yale ya Igunga; ilipata kusdikika kuwa mauaji ya Igunga yalisababishwa na CCM pinzani ndani ya CCM tawala, hivyo bado kuna nafasi ya kuwa huenda yamesababishwa na serikali pinzani ndani ya serikali tawala, ili kuiweka serikali tawala in a hard situation mbele ya jamii...!
  2. Yaliyomkuta Ulimboka huenda yamesababishwa yamesababishwa na serikali baada ya kumuona kama threat katika utawala wao...! Lakini kama ndio hivi, basi binafsi nazidi kudhibitisha jinsi walivyodhaifu katika mikakati, maana hatua ya kumteka mtu na kumuachia akiwa hai, huku wamekwisha muumiza kiasi hiki ni uzembe wa kutupwa...!
  3. Huenda yaliyomkuta Ulimboka ni kama ya watu wengine wengi waliiopata kutekwa na kupigwa na hata kuuawa...! Hii ni kwa sababu naye ni binadamu, na anaweza akawa na vishawishi vya kuweza kumfanya afanyiwe hivyo...!
  4. nk

4.Yalimpata pia yule m/kiti kule arumeru na wabunge wa cdm kule mwanza kwa kweli inauma sana.
 
kuna kiongozi mmja alikuwa anaitwa dr kombe kama sikosei naimbieni nimelisahau jina .serikali ilimfuatilia toka DSM NAKWENDA KUMUULIA MOSHI MJINI TOKA dsm mkewe akakimbilia kwenye mahindi .nikumbusheni

luteni jenerali imram kombe,alikua mkuu wa idara ya usalama wa taifa by that time
 
Hizo ni chuki binafsi, mimi hazinistui kwa sababu najuwa chuki zenu ni kuwa tu pale wetu anapoweza kufanya vizuri kuliko wenu, huwa hampendi na mnaona vipi huyu katuzidi? hiyo ni roho ya kichawi.
sasa hapa nani kafanya vizuri? ndani ya umaskini wote huu na ufisadi unaoulalamikia kila siku kuna mtu anafanya vizuri? ni nani huyo?
 
FJM nafikiri tupo ktk boti moja kumsubiri pinda anaamua nini hapo kesho. Uongozi hatari kabisa huu!
 
Last edited by a moderator:
Mengi yanafuata, nadhani madaktari wote watagoma kufanya kazi sasa,
 
Madaktari wakiamua kususia kabisa kutoa huduma kufuatia dhahama ya Ulimboka wasitafutwe watu ama kundi la kulaumiwa.Badala yake kitu kinachoitwa serikali kibebe lawama.
Wote wenye moyo wa huruma na utu tumwombee Dokta apone haraka.
 
Mkuu unaushahidi wa serikali kuhusika kwenye hii ishu?Ni jukwaa la Great thinkers hili habari za porojo za vijiweni hazina nafasi hapa.Kama una ushahidi tuwekee hapa then tuendelee kuchangia.Otherwise piga kimya tusubirie taarifa zaidi kutoka vyanzo mbalimbali vya uhakika.
Well-said mkuu. Hatutaki ubabaishaji hapa!
 
Pinda kesho aongee kitu cha kueleweka n sio pumba

kwani kuna kipya zaidi ya

1) police inaendelea na uchunguzi wa tukio .... utakaochukua miaka kadhaa

2) pumba zaidi kuhusu mgomo wa madaktari

nchi ilipofikia ovyo kabisa
 
Hii ni Hatari!!, Sijui watanzania wanahitaji Mungu awaonyeshe nini kuwa CCM haifai!!.
 
Vipi kama mwisho wa siku tunaambiwa "waliuofanya hilo tukio walikuwa watu wenye hasira ambao wazazi au watoto wao wamekufa kwa sababu ya huu mgomo" walifanya hivyo kulipa kisasi....
 
Vipi kama mwisho wa siku tunaambiwa "waliuofanya hilo tukio walikuwa watu wenye hasira ambao wazazi au watoto wao wamekufa kwa sababu ya huu mgomo" walifanya hivyo kulipa kisasi....
hakuna kitu kama hicho.
 
Hii ni stage ya juu ya uuaji inayoendekezwa na serikali yetu. Kama serikali ingekuwa na nidhamu ya kuheshimu maisha na utu wa mtu tusingefikia hapa.
 
Huyo hana maana kabisa serikali imemsomesha ili asaidie jamii yeye kaweka maslahi yake binafsi kwanza kuua watanzania waliomsomesha kwa kodi zao ni kosa kubwa sana,fanya kazi kwa bidii upate fedha, siyo kushawishi na wenzako wagome Hehehee! ili tufe? tena kwa maslahi binafsi!

Haiwezekani anataka utajiri bila kufanyia kazi,mtu mbaya kabisa aliyejitokeza TZ karne hii ya 21 ni huyu,serkali ilishakubali kuwa yanazungumzika kuwa na subira wakati yakitekelezwa siyo kulazimisha tena kwa kusababisha vifo vya wagonjwa huu siyo udaktari ni uhujumu tena mbaya kuliko ukimwi,ingelikuwa China leo hii asingekuwepo duniani,nashauri hivyo mbona kina Kombe,Mahiza e.t.c hawapo na nchi inaendelea.

Nadhani wewe ni mmojawao kati ya wale waliompiga Dr. Ulimboka! Kuna ubaya gani madaktari kudai serikali iboreshe huduma za afya? Kwani si ni kwa faida ya hao wagonjwa? Kuwepo kwa daktari bila kuwa na maabara zenye vifaa na bila kuwa na madawa hao wagonjwa wataponaje? Think out of the box!
 
Vipi kama mwisho wa siku tunaambiwa "waliuofanya hilo tukio walikuwa watu wenye hasira ambao wazazi au watoto wao wamekufa kwa sababu ya huu mgomo" walifanya hivyo kulipa kisasi....

Ngoja tuichambue hoja yako.
1.kwanza kabisa,ikiwa huyo mwenye ndugu aliyefariki angekuwa na uwezo wa kukodi watu wa kumfanya ulimboka walichomfanya,sina shaka angekuwa na uwezo wa kumtafutia huyo nduguye matibabu mbadala zaidi ya muhimbili.

2.Ni vigumu(inawezekana ila sio rahisi) kwa mtu random tu wa kawaida kuhusisha kilichomtokea na dr. Ulimboka.tungekuwa na watanzania wa namna hii,jk asingekuwepo leo.

3.Kwa hali ilivyo sasa hivi,serikali tu ndiyo inaonekana kutokuwa na solution ya huu mgomo,na zaidi ya hapo,mgomo huu unazidi kuongeza idadi ya wanaoichukia serikali,siku baada ya siku.

4.Ni mtu ambaye ameishiwa diplomatic means tu ndiye anayeweza kuchukua hatua kama hii.ninaamini hatua ya rais wa jamhuri yetu kukutana na madaktari ikulu ilikuwa ni moja ya hatua kuu na za mwisho kwa serikali.what more could the Government do??

5.Only a desperate party could do this.who can deny the pressure that the Government have had lately?M4C,a stupid budget,now doctors..this Government is desperate beyond measure.
 
TBC ni stesheni ya ajabu sana wanaelezea masuala ya pinda kuhusu mgomo kuuzuia lakini wanashindwa hata kuelezea suala la dr???? huu ni ujinga sidhani kama nitaangalia TBC
 
Back
Top Bottom