Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Wezi wa mali za umma na wahujumu uchumi wanadunda mtaani bila wasiwasi wowote lakini watetezi wa haki za wanyonge na wanaokemea udhalimu wanakamtwa kama wezi!! Hii ni aibu na fedheha kubwa kwa Serikali na waliokabidhiwa jukumu la kuwalinda raia kwa ujumla.
 
Hii serikali inadhani watanzania bado tupo gizani kwa njia hiyo waliyotumia wamekosea plan A they can switch to another plan

Free Dr. Ulimboka

I support the Doctors
 
Kuna tetesi ina circulate Muhimbili kwamba Ulimboka kauwawa.
 
Habari nilizozipata kutoka kwa moja ya madaktari,wanajipanga kufanya jambo kubwa sana na endapo ma-chief watawapinga basi wako radhi kutangaza bifu na ma-chief,lakini wanakusudia kufanya kitu kikubwa sana ambacho ni kufunga kabisa hospitali na hata kwenye hospitali za halmashauri.

FREE DR ULIMBOKA NOW
 
Ungetaja kituo kama kweli ni confirmed! I wish we acted more matured to command more respect!
 
Dr. Ulimboka inadaiwa amekamatwa na polisi usiku kwenye majira ya saa saba kasoro hivi akiwa na wenzake. Watu ambao hawakujitambulisha na wakiwa na mavazi ya kiraia lakini wakiwa na silaha walimchukua Dr. Ulimboka mkukumkuku kwenda kusikojulikana. JItihada za awali za kufuatilia zilionekana kugonga mwamba. Hata hivyo, habari ambazo tumeweza kuzipata sasa hivi ni kuwa watu waliomchukua wanadaiwa ni polisi na kuwa yuko kwenye kituo cha Bunju nje ya jiji la Dar kupita maeneo ya Mbezi. Sasa hivi wanasheria na vyombo vya haki za binadamu vinafuatilia kujua hali yake huko aliko kwani juhudi za kutaka kuzungumza naye kwa simu zimeshindikana.

Ni matumaini yangu - na bila ya shaka ya wengine - kuwa Dr. Ulimboka ambaye ameonekana kama kiongozi wa mgomo wa madaktari unaondelea nchini hatodhurika kwa namna yoyote ile na kuwa sheria zote zinafuatwa siyo na wale wanaotaka wengine wafuate sheria bali na wale wanaopaswa kufuata sheria.

Kwa niaba yangu na CCTI tunalaani vitendo hivi ambavyo vinaonekana kutaka kugeuza Tanzania kuwa police state hasa baada ya kushindwa kutafuta suluhisho la kawaida. Na zaidi kama kuna jambo lolote ambalo limefanywa kinyume na sheria au haki au utawala wa sheria tunataka wahusika wote wawajibishwe mara moja.

Free Dr. Ulimboka Now!

SERIKALI ifuatilie fedha zetu billioni 300 kule uswisi, na zile za EPA na Richmonduli nk. nk wawalipe madaktari kiishe; kumuua Ulimboka ni kumwagia moto petroli, hakutasidia kitu. udhaifu ule ule wanaosema makamanda.
 
Wanafikiri wakimkamata Ulimboka basi madai ya madaktari yatajitatua yenyewe na mishahara kwa walimu na madaktari automatically itajipandisha, na huduma za afya zitaboreka! Mwe!!! Kweli tuna mAVI-o-NGoZI yanayojua kuwaza.
 
Nani atafanya hio tracking? kesi ya Nyani hio, hivi hakuna mwenye contact zake au a person ambaye yupo karibu na familiya yake anaweza kuthibitisha hili.

Hizi ndio busara. Mko watu watatu tu wenye busara kwenye thread hii ikiwa ni pamoja na wewe.

Tuache malumbano tuhangaike na kupata ukweli wa taarifa hii.
 
Crazy move by the government. Hii jambo italeta hasira zaidi toka kwa madaktari.

Serikali inatumia mbinu za kizamani za wakati wa ukoloni, kuwakamata viongozi kwa matumaini mgomo utasitishwa! Haikuwahi kutokea katika historia, Mandela alipofungwa ilikuwa kama kuchochea moto wa mapinduzi na hadithi nyingi zipo kudhihirisha hili. Je ni kweli uongozi mzima wa taifa umeshindwa kubuni mbinu mpya za kuzuia mgomo hadi kwenda kumshika mtu mmoja! Maskini Raisi Wangu! Kweli tutaweza kutatua matatizo yetu kwa kuyaangalia kwa ubinafisi huu! Never personalize matters.


Indeed when the Doctors announced their intention to strike a third time, their leaders never left Dar, they simply made the announcement and what we witnessed is a choral response to the call from Dodoma to the Lake, from Lindi to Moshi. By holding Ulimboka, the government is only fueling doctors' anger! And who loses? It is the wananchi! Woe to those who designed the move to take Ulimboka in their custody. Ulimboka we salute you!

Free Ulimboka NOW!
 
Uwiii hii thread inakimbia kama ile ya SimbaChewene halafu mwishoni mods wanaichomoa kwi! kwi! kwi! kwi!
 
Inasikitisha sana kuona serikali inatumia nguvu badala ya kutafuta njia muafaka ili kuokoa maisha ya watanzania

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Free Dr. Ulimboka!!!! Kumshikilia huyu Dr. sio mwisho wakumaliza malalamiko na madai ya msingi kwa MaDr.
 
Safi sana serikali ya chama cha mapinduzi!!!!
kamata na wana harakati wa cdm wanao sababisha mshindwe kutawala!
Kamata na wamiliki wa JF;Funga midomo waandishi wa habari makini!!!!
hapo ndipo mwisho wenu utakuja na kuwaweka kwenye kumbukumbu za kihistoria!!!
poor you!!!

Uvivu wa kufikiri ni kilele cha umasikini.
 
Serikali ya Kikwete dhaifu, tumieni chenji ya rada kupata CT scan ya 135,OOO USD (=TZS 212.73 bilioni kununua mashine mpya ya CT http://www.medwow.com/used-ct-scanner/philips/brilliance-6-slice/716665331.item Serikali iachane na utengenezaji wa mashine ya CT iliyoharibika ambayo inatuingiza hasara kubwa ya kuwasafirisha mafundi kutoka nairobi ambao hawakutengeza chochote na bado tuliwalipa, sasa mnaagiza fundi kutoka manufacturers, watatuambia haitengenezeki tutapoteza fedha nyingine kwa malipo na gharama za kuwasafirisha. Madai ya madaktari ni ya msingi, kumkamata Ulimboka si suruhu ya kupatikana vifaa wanavyodai madaktari. Dhaifu, Amka!
 
Back
Top Bottom