Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Achiwe huru kwani yuko gereza lipi?
Dr. Ulimboka inadaiwa amekamatwa na polisi usiku kwenye majira ya saa saba kasoro hivi akiwa na wenzake. Watu ambao hawakujitambulisha na wakiwa na mavazi ya kiraia lakini wakiwa na silaha walimchukua Dr. Ulimboka mkukumkuku kwenda kusikojulikana. JItihada za awali za kufuatilia zilionekana kugonga mwamba. Hata hivyo, habari ambazo tumeweza kuzipata sasa hivi ni kuwa watu waliomchukua wanadaiwa ni polisi na kuwa yuko kwenye kituo cha Bunju nje ya jiji la Dar kupita maeneo ya Mbezi. Sasa hivi wanasheria na vyombo vya haki za binadamu vinafuatilia kujua hali yake huko aliko kwani juhudi za kutaka kuzungumza naye kwa simu zimeshindikana.
Ni matumaini yangu - na bila ya shaka ya wengine - kuwa Dr. Ulimboka ambaye ameonekana kama kiongozi wa mgomo wa madaktari unaondelea nchini hatodhurika kwa namna yoyote ile na kuwa sheria zote zinafuatwa siyo na wale wanaotaka wengine wafuate sheria bali na wale wanaopaswa kufuata sheria.
Kwa niaba yangu na CCTI tunalaani vitendo hivi ambavyo vinaonekana kutaka kugeuza Tanzania kuwa police state hasa baada ya kushindwa kutafuta suluhisho la kawaida. Na zaidi kama kuna jambo lolote ambalo limefanywa kinyume na sheria au haki au utawala wa sheria tunataka wahusika wote wawajibishwe mara moja.
Free Dr. Ulimboka Now!
Nani atafanya hio tracking? kesi ya Nyani hio, hivi hakuna mwenye contact zake au a person ambaye yupo karibu na familiya yake anaweza kuthibitisha hili.
Crazy move by the government. Hii jambo italeta hasira zaidi toka kwa madaktari.
katekwa kwenda wapi? nimezungumza na daktari rafiki wa karibu sana na Ulimboka anasema yuko salama tu
wewe si ndiye uliymshikilia? mwachie huru na utatue tatizo la madaktari na walimu.
Safi sana serikali ya chama cha mapinduzi!!!!
kamata na wana harakati wa cdm wanao sababisha mshindwe kutawala!
Kamata na wamiliki wa JF;Funga midomo waandishi wa habari makini!!!!
hapo ndipo mwisho wenu utakuja na kuwaweka kwenye kumbukumbu za kihistoria!!!
poor you!!!