Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Nashauri madaktari kama Ulimboka akishafika MoI fungeni hospitali nzima! Wekeni na walinzi, wananchi tunajikusanya tunakuja kuongeza ulinzi!!
 
Naamin na jamaa wa bil 300 nao wataharasiwa very fast,,,,,,,labda ndo ari mpya hii
 
Amekutwa msitu wa Pande.........kule wanapowaulia watu wasiowataka!
 
Serikali inapochoka kushughulikia matatizo ya wananchi wake na ikatukuza ufisadi, humuoana kila mwananchi/raia mpenda haki na ukweli kuwa ni adui mkubwa, hasa anapojitokeza kudai haki na kueleza ukweli. Madai ya madaktari ni mapana na yanagusa ustawi wa jamii. kwa mfano wanaposema vitendea kazi havipo, je ni kosa? mbona wao matumbo yakiunguruma tu, tunawasikia INdia. Hoja kwamba serikali haina pesa ni uongo wa mchana kweupe. Tujiulize serikali isiyo na pesa inakuaje na mabilioni ya pesa benki za nje kama uswisi n.k, serikali isiyo na pesa inakuaje ripoti ya CAG ionyeshe mabilioni ya pesa yakiwa yamepotea/yameliwa na taasisi moja tu/mtu mmoja,serikali isiyo na pesa inakuaje viongozi wake kila kukicha kiguru na njia kwenda ng`ambo kwa kisingizio cha kuona utendaji kazi wa balozi zetu,ooh mara kutafuta wafadhili wa bajeti, mara kutafuta wawekezaji, mara marafiki(sijui wa kike au kiume), mara kutangaza utalii. hiyo ni serikali ambayo viongozi wake wamechoka kufikiri, na viongozi wanaofikiri wapo uraiani na hao ndio wapambanaji wakweli. sas kazi ni moja tu, nayo ni kung`oa magugu yote ya CCM
Natamani wote tuanze kazi mara moja ya kung'oa hayo magugu! Lakini kuna watu waoga wa kutupwa, hata akila andazi moja kwa siku yeye atasema CCM hoyeeeee!! Its bull shit, watu wanapoteza maisha kwa sababu za kipuuzi kabisa, waafrica kwa nini hatujithamini lakini?

Its simple, majority of the Tanzanians are young and jobless, create some small megamilions projects in the health services, we vipaumbele kwa kila mwaka! afya kwanza mfano mwaka 2012/2013 kila kata tujenge na kuhakikisha tunatrain vijana kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa huku wakijiendeleza na hao qualified DRs let them train these youngmen & women taratibu, ikiwezekana weka mawasiliano hospitali zote za rufaa ili madaktari bingwa wote nchiniwawe networked!

Kazi hiyo unawapa makampuni ya simu kwa contract maalumu say within 5 ~ years, lakini viongozi wetu hawataki wala hawasikilizi! POOR TANZANIANS are dying kwa kukosa sindano, pamba za kusafishia na dawa pengine miti ipo ila kuiprocess tu nakupata dawa.
 
Hiyo ni kazi ya Riz1 na baba yake, lakini siku zao zinahesabika, wataishia hell au jela, wanadhani hata wakituibia pesa zote za dunia zikawa zao hawatakufa? wamuulize Hosni Mubarak and the like
 
Hata wakoloni walitumia njia hii.Lakini yaliwashinda naaamini hii ndiyo safari ya mwisho.
 
alikuwa amefungwa kamba miguu na mikono... it is sad; sijui kama atasurvive maana alishindwa kuzungumza kabisa

Ni kweli? Siamini bado! Kweli huu ndio udikteta tena wa zamani kama nini! Kichwa kinaniuma! Huwezi ukamwondoa kiongozi kama mtu ukadhani umeondoa uongozi wote. Ni kama kina Zomba wanaofikiria kumsema Raisi ni Mdhaifu unamaanisha JAKAYA KIKWETE- NO- ni taasisi yenyewe. Kumwondoa Dr kwa mateso kama haya, kunachochea mgomo, kunaleta madhara zaidi- Ulimboka ni sauti ya madaktari, sio yeye bali ni madaktari. Kama suluhisho ni kuwakamata na kuwatesa basi wangefanya hivyo kwa madaktari wote ndio iwe na maana. Aluta Continua.

Nitasali nikiomba sana Dr Ulimboka apone na atusimulie yaliyomtokea. Asanteni wanajamii kwa kuleta taarifa hizi zenye kudhihirisha pasi shaka ufedhuli wa uongozi wetu wa taifa. Mungu ambariki na ampe ahueni Dr Ulimboka!
 
Safi sana serikali ya chama cha mapinduzi!!!!
kamata na wana harakati wa cdm wanao sababisha mshindwe kutawala!
Kamata na wamiliki wa JF;Funga midomo waandishi wa habari makini!!!!
hapo ndipo mwisho wenu utakuja na kuwaweka kwenye kumbukumbu za kihistoria!!!
poor you!!!

halafu maoni yako yatawafikiaje? Au ndio mtahamia kwenye vikao vya ndani vya chama? Vile vya kuzodoana kama EL na JK kwenye kikao cha CC? Acha kuwa na akili fupi wewe!
 
Kama ndo tumefikia huku tujiandae kwa majanga wanaharakati wote.
 
Pole sana dr.uli,2nazidi kumwomba mungu akuponye 2endelee na mapambano ya haki na amani yetu ya ukweli ipatikane.
 
Dr Ulimboka najua ulikuwa unatetea wonyonge, Mungu atakusaidia, utapona haraka, Madaktari wote wako nyuma yako, sasa mgome uwe nchi zima. Tena mgomo hasa, total tools down
 
Serikali ina haki ya kukumata na kukuhoji wakati wowote ule.


Mbona wengine wamewaogopa aka EPA na wenzake? hii haki ya Serikali ni kwa baadhi ya watu tu sio, na wewe unakubali hili?.
 
Kama kavunja sheria za nchi au kakaidi amri za mahakama hawachiwi mpaka sheria za kumuachia zikamilike, hata kiongozi wa upinzani bungeni alipokaidi amri ya mahakama alikamatwa kwa nguvu akapelekwa mahakamani.

Msituvunjie sheria za nchi halafu mfunguwe midomo yenu.

Kwani amri ilitolewa kwa Dr. Ulimboka? Nilikushauri tafuta tiba ya utindio wa ubongo mapema
 
Pamoja na kwamba siungi mkono hoja za mgomo, bali za kudai haki, HILI LA KUTEKA MTU NA KUMHARIBIA MAISHA IT IS VERY UNACCEPTABLE. SULUHISHO NI MOJA TU, ONDOA SERIKALI YA MAGAMBA KWA NJIA YOYOTE ILE!
 
Kama tumefika hatua hii kweli nchi haitawaliki , mwananchi anatendewa unyama wa kiasi hiki na serikali yake hivi basi tumekwisha
 
alikuwa amefungwa kamba miguu na mikono... it is sad; sijui kama atasurvive maana alishindwa kuzungumza kabisa

Shocking !!!! Tanzania imefikia hapo, kwa mtu kutendewa mambo kama hayo. Kama ni kweli, nataamini moyoni mwangu kuwa yaliyowapata Kubenea, Chacha Wangwe, Kombe na wengine wa namna hiyo kulikuwa na mikono kama hiyo !!! Halafu tunasema Tanzania ni nchi ya amani, kweli kuna amani au utulivu ?
 
Back
Top Bottom