Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

kutokana na kwamba mgomo wenyewe ni wakusua sua, silikali inadhani ni wachache wakina ulimboka ndio wanashinikiza, ile kamati ya madaktari wangetumia kwanza vyombo vya habari ili kuonyesha wananchi jinsi gani selikali haijashughulikia kuimarisha huduma hospitalini

kaka hapo kwenye red umekosea,ulipaswa kusema serikali.
 
Ni kweli Dr. Olimboka katekwa na askari polisi na kapigwa na kwa sasa yupo kituo cha polisi cha uchochoroni tunakifuatilia kujua kama ndipo walipo mficha. Sasa hii imetuamsha hasira na mgomo kamili ndo utafuata.

Hii taarifa ya kupigwa na kwamba anapelekwa hospitali ni za kusikitisha sana. Hii ni aibu kwa serikali nzima. Ni ishara ya utawala wa kimabavu. Ni dhuruma kwa wanyonge na kitendo kisichovumiliwa.

Ndugu zangu, tuoneshe nguvu yetu, tuungane na madaktari na wananchi wote kupinga kitendo hiki kichafu. Kamwe nchi haitakiwi kutawaliwa kimabavu namna hii. Ninalaani kitendo hiki!
 
Haya mambo ya kutekana na kupigwa na kutelekezwa uwa yanatokea Colombia, Mexico, Cambodia, sasa yamefika mpaka Tanzania ni hatari sana tunapoelekea...Umafia umefika Tanzania.
 
Tunaomba Serikali itoe kauli kuwa Nchi imewashinda. Sambamba na tukio hilo, tumemsikia Mh. Pinda akisema kuwa watatilea kauli mgomo wa madaktari kesho, ila liwalo na liwe.
 
Sasa naanza kuona upofu wa viongozi wetu! Huwezi kuwatisha watu wasomi wenye kujua haki zao kwa kuanza kukamata watu na kuwaweka ndani! Uongozi wa kimabavu siku zote huishia pabaya! Kwani wanaona ugumu gani kukubaliana na matakwa ya Watanzania! A better working conditions! Batter facilities! Naambiwa tangu mgomo wa madaktari ulipoanza serikali ilitumia nguvu ya zaidi ya 8bl...
Mahakama imesema mgomo usitishwe na viongozi wa mgomo watangaze kwenye vyombo vya habari watangaze kuwa hakuna mgomo mpaka jambo hili litapomalizwa kusikilizwa na mahakama.

Mwacheni akafundwe adabu huyo mzandik na muuaji wa wagonjwa wetu na watoto zetu wanaoumwa mahospitalini. Na sasa itabidi apewe adabu aseme ni nani wako nyuma yake wakimshindilia kuwa mkaidi.

Tutawajuwa na kila mmoja atachukuliwa hatua na kupewa adhabu kali sana na kama sheria hazina adhabu kali, basi tutatunga sheria ya "dharura" yenye adhabu kali sana iwe fundisho kwake na kwa wengine.
 
Samahani mkuu Riwa amepigwa na nani..
 
Last edited by a moderator:
Huku tunako elekea nchi itanuka muda wowote huu uonevu wa hali ya juu.
 
Waliomchukua jana....sijui TISS au POLISI!
 
Ni kweli Dr. Olimboka katekwa na askari polisi na kapigwa na kwa sasa yupo kituo cha polisi cha uchochoroni tunakifuatilia kujua kama ndipo walipo mficha. Sasa hii imetuamsha hasira na mgomo kamili ndo utafuata.

kama ni polisi nadhan wamemkamata,hawajamteka,,,,,ila sasa ulimboka kama wamemkamata na wale mafisad nao wawabebe
 
Pinda si kasema liwalo na liwe inabidi akafanune kauli yake polisi
 
Busara itumike na Mungu azipe pande zote busara ili nyasi zisiumie
 
Nasikia wale Madaktari bingwa hawajagoma labda ndio watamtibu.

MOI wameshatangaza over and over again...kuwa wanatoa huduma za dharura, kwa kuwa hawana maDaktari wa kutosha kutoa huduma za kawaida za kila siku kama clinic na upasuaji.
 
Eti oo tanzania nchi ya amani, sijui kisiwa cha amani whatever hata mkisema ni bahari ya amani.ukweli ni kwamba hakuna amani ila kivuli cha amani kinatumika kutuongezea umaskini.

Ndiyo maana watanzania wengi wanaogopa uongozi sababu hizihizi za uonevu wa kjinga.ila madaktari nawasihi kazeni buti katika hili,bila kuwa na umoja amani ya kweli haipo.

Kila ukombozi unag'halama zake oneni mwenzenu yaliyomkuta!!!! yaani lazima watu waumie ili mambo yaende sawa, naomba hili liwape nguvu madaktari kutimiza azima.

pole sana kwa dr ulimboka na familia yake.
 
Back
Top Bottom