Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kama unafahamu historia kidogo tukio la kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Dr. Ulimboka silakustua. Hii ni kawaida wakati tawala chovu kama huu zinapokua ktk hatua ya mwisho kuanguka!
Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI
‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous’
Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.
Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.
Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa ‘agente provocateure‘ kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.
Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.
Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all’
Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.
 
Tumuombee Mungu aponee haraka,arudi kuwa na afya njema. Ukweli wa yote yaliyotokea yatajulikana,hamna siri tena hapa.
 
"Solidarity forever...." nimeunganishwa kwenye simu madaktari wanaimba wakimsindikiza Ulimboka anapoondoka kwenda MOI baada ya MRI. Yaan, weacha tu! Mi sijui kinachofuata. Nahisi harufu ya panya aliyekufa juzi. Serikali inaelekea imehusika, sababu yasemekana mtu mmoja alimpigia simu wakutane, halafu walipokutana wengine wakawa wanaongezeka na ghafla akafungwa kitambaa usoni na kuanza mikong'oto na mapanga. Ati wanaulizana,"tumchome sindano ya sumu nini, au tukamtupe barabarani aonekane kakanyagwa na gari?" Baadaye wakamwacha wakidhani kafa.

Wakati anafikishwa Muhimbili, mwandishi mmoja wa habari akanaswa anaongea kwenye simu, "Aisee hajafa yule jamaa bwana, yuko hai ndio kaletwa hapa sasa hivi, tulikosea mahali fulani" Waliokuwapo jirani wakamrukia kama nyuki na kumpa kichapo karibu afe kama sio wasalama wa Muhimbili kumdaka na kuondoka naye, lakini suti yake nyeusi ikiwa nyang'anyang'a.

Habali ndo hiyo.
Hadithi za shigongo hizi.
 
Sasa mitusi ya nini best, si ujibu hoja? kama huna la kusema bora unyamaze...
unapindisha ukweli kwenye issue sensitive ambayo ipo wazi haiitaji uchunguzi wowote kuitambua hata mtoto wa darasa la pili atatambua na hayo ndio malipo yako ukome na vipropaganda vyako ulivyo tumwa.
 
Naamini njia zao zingine ziligonga mwamba na wameamua kubadilisha tu njia za ubabe, wameona sumu inadunda wameanza kuwadunda sasa. Ila kwa nini Dr. Ulimbooka alikubali kutoka usiku ule wote na alikuwa anajiamini nini? Kwa kweli naye hakufikiria vyema, Japo si mda wake sasa kulaumu ila watu wengine wajifunze wasije kukubali kukutana na mtu yeyote usiku hata kama iweje. Kwa sasa ngoja tuone madaktari watachukua hatua gani kulingana na hili tukio la kusikitisha sana
 
Mkuu wangu coby,
Ni kweli katika tasnia za ukachero si busara hata kidogo kupuuza uwezekano wa aina yoyote katika jambo kama hili. Hata hivyo, labda tu nifanye usahihisho ili kuweka rekodi sawa. Suala la serikali kufanya jambo kama hilo si tu kwamba ni la kitoto bali ni jambo la hatari kuliko hatari yenyewe. Hivyo basi, pamoja na ukweli kwamba serikali inaweza kufanya jambo la kitoto lakini sizani kama inaweza kufanya jambo la hatari kama hilo ambalo madhara yake kwa taswira ya serikali ni makubwa mno. Ni serikali chache sana, ambazo hususani ni za kidikteta wa wazi ndio wanaweza kufanya jambo kama hilo.

Labda niongeze possibility nyingine katika mambo kama haya. Hata wananchi wa kawaida wanaweza kufanya alichofanyiwa Ulimboka. Just imagine, mtu amepeleka ndugu kipenzi halafu akafa kwa kukosa huduma huku yeye akiamini kwamba pamoja na kwamba madaktari wana madai lakini sio busara kwao kuacha watu wanakufa. Mtu au watu wenye mawazo kama hayo wanaweza kumtendea mbaya Ulimboka kama njia ya kulipiza kisasi.

Na wengine wanaweza kutaka kutoa ujumbe kwa Ulimboka na wenzake waone uchungu wa kuuguliwa....! Wahenga wanasema, ukitaka kujua kifo kachungulie kaburi!
usilete nadharia hapa wewe, ya nini kuingia gharama za kumdhuru Dr Ulimboka badala ya kwenda hospitali binafsi? si lazima utibiwe hospitali za umma na hasa unapojua kuna tatizo la mgomo
 
Kipindi hiki ni cha mvutano wa madaktari na serikali pengine jamaa ameamua kuzima simu na kubadilisha makazi kwa hofu yake tu kisha tunasema katekwa ......

sioni sababu ya kusema sana kama hatuna uhakika na jambo hili



Dr. Ulimboka akipelekwa kwa ajili ya MRI hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo..SOURCE:MEDICAL ASSOCIATION OF TANZANIA PHOTOS

292309_10151033920646208_607160914_n.jpg
 
Khaaa serikali yetu inaufinyu wa mawazo na kwahili wameongeza matatizo na sio kutatua wala kupunguza tatizo. Watanzania tuamuke na tusimame kidete ktk hili!
JINSI YA KUMSINGA (massage) na KUMSUGUA (scrub) MWENZA WAKO KWA KUTUMIA VITU ASILIA.
Binadamu wote lazima tuchoke wakati fulani na kupata maumivu ya viungo vya miili yetu.Basi si kila siku tuwe tunakimbizana kwenye massage spas,siku moja moja unatakiwa umsugue na kumsinga mwenzio nyumba.

Oga vizuri kabla ya kuanza, shughuli hii inaweza fanywa kitandani au kwenye mkeka. Unaanza kuusugua mwili wote kwanza kwa kutumia unga wa liwa ulichanganywa na maji ya rose pamoja na machicha ya nazi au unga wa manjano uliochanganywa na maji ya rose pamoja na machicha ya nazi. Sugua mwili mpaka uhisi uchafu na nongo zote zimeisha.Baada ya hapo unaoga nakurudi kwa ajili ya kusingwa.Unachukua mafuta ya mzaituni,ya nazi au ya ufuta unampaka mwili mzima na kuanza kumsinga(kummassage) taratibu na kwa upendo alafu unachukua unga wa karafuu na kuunyunyuzia mwilini sana sana sehem za mgongoni na kiunoni(unga huu usiguse sehem za siri,unawasha).Utaendelea kumsinga mpaka utakaporidhika unamuacha akae na ule unga kama dakika 15 hivi,akipitiwa na usingizi muache apumzike akiwa macho*akaoge au ukamuogeshe alafu kitakacho fuata I.T.V hatutaki kujua..........


Kusugua na kusinga mwili inasaidia kuondoa uchafu mwilini,kupunguza maumivu makali mwilini,inakufanya upate pumziko na kuondoa usongo wa mawazo , kutaiwezesha mishipa ya damu kuwa katika hali nzuri na hivyo kurahisisha msukumo wa damu katika mwili wako.Pia huleta furaha kwa wale wawili wapendanao.

MAHITAJI NI KAMA YA FUATAYO

MACHICHA YA NAZI

UNGA WA KARAFUU

UNGA WA LIWA

*MAFUTA YA KARAFUU

*UNGA WA MANJANO

*MAFUTA YA MZAITUNI

MAJI YA MAUA WARIDI

Nyongeza: kwenye swala la mafuta unaweza tumia mafuta ya nazi,ya ufuta au yoyote yale ambayo hayataleta mchubuko wakati wa kusinga. Kusugua na kusinga inaweza chukua dakika 45 mpaka 60 na baada ya hapo pumzika kiasi kisha unaweza kwenda kuoga. Wataalam wanashauri baada ya kuoga utembee kidogo ili kuuweka mwili sawa kabla ya kwenda kulala.

Mafuta ya karafuu unaweza yatumia peke yake*kuchua sehemu zenye maumivu makali*kama kiunoni,shingoni,mgongo na miguu.

KWA ATAKAE HITAJI UNGA WA LIWA,MANJANO NA KARAFUU, MAJI YA ROSE NA AINA MBALIMBALI ZA MAFUTA YA KUSINGA KARIBU SANA DUKANI KWANGU*EmC's CHOICE SINZA MAPAMBANO 0654450200
Evelyne Michael at 4:49 AM
Share

0 comments:
Post a Comment
›
Home
View web version
About Me


Evelyne Michael
I am a Zigua from Tanga,Tanzania.The first born in a family of five children.I am a holder of Bacherol of Law Degree and a Postgraduate Diploma in Human Reso

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

BONGE LA ANALYSIS....mkuu, you're GREATEST THINKER!!
 
Umeongea vema jemedari wangu,kwangu mimi sina sababu ya kumumunya maneno,hii ni njama ya serikali.Lakini kama serikali yetu imefikia hatua ya kutatua migogoro kwa njia hiyo,na wananchi ambao tumeipa serikali madaraka tumekaa kimya,natamani nisingezaliwa tz,watu wamekosa moyo wa uthubutu. Kwani lazima tufike 2015.Nyie viongozi wa upinzani hasa cdm ambao ndio jicho letu,sikio letu na midomo yetu,kwanini msituambie wananchi nini cha kufanya kabla ya 2015.Amani ambayo ccm imekuwa ikitumia miaka nenda rudi kuwahadaa wananchi iko wapi. nasikitika
wewe kama unaakili timamu kwanini mpaka uambiwe cha kufanya. Hao unao wategemea unafikiri wana jeuri hiyo? Wake up man
 
Dk. Ulimboka akimbizwa hospitali
Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini Tanzania Dk.Steven Ulimboka amefikishwa
katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), akiwa mahututi baada ya kuokotwa eneo la
Mabwepande.

Hivi huko MOI nako si kuna mgomo au?? Yeye amepokelewa kama nani (mgonjwa wa kawaida kama wananchi wengine tulionyimwa huduma au yeye ni spesheli??)

Double standards all the way............

Pole Dr. Ulimboka ila yawezekana pia watekaji walitaka kuona je huyu Dr. Ulimboka akipata shida inayohitaji matibabu atahudumiwaje kipindi cha mgomo!? - Just speculating
 
he he wasali tu apone maana nafikiri hii serikali itafia kwenye hili tatizo na watanzania tusiporeact hapa basi tena, im ready for any move na walah kama kuna the hague one of the government officials need to go for sure, **** the heartless creatures for this, may they be cursed with their children and grand children, its very very bad,
 
ufisadi,dhambi na dhuluma kamwe havitashinda haki,sirikali hii dhaifu kama imefikia udhaifu huu basi ni wazi ina mchoko wa akili na mwili,naona ndo wanalianzisha hili balaa.
 
usilete nadharia hapa wewe, ya nini kuingia gharama za kumdhuru Dr Ulimboka badala ya kwenda hospitali binafsi? si lazima utibiwe hospitali za umma na hasa unapojua kuna tatizo la mgomo

Kama unazani kila mtu ana uwezo wa kwenda hizo hospitali binafsi basi una safari ndefu ya kuifahamu nchi yako unless kama wewe si mwenzetu
 
ila wahusika wa hili jambo watambue kuwa KILA NAFSI ITAONJA MAUTI
 
Back
Top Bottom