Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

jitahidi kujenga hoja acha ushabiki,
ulimboka ni nani awe na thamani kuliko ma elfu ya watanzani wanaoteseka kwa mgomo?
madaktari walipo goma sijaona mtu hata mmoja akiwaita wanyama kwa mateso wanayopata watanzania wasio na hatia kwani wao sio serikali.
mlichofanya nikuendelea kuchochea vurugu
Wananchi wanakufa kila siku hospitalini ,kila siku iendayo kwa mungu kwa kukosa dawa za kawaida kabisa,vifaa vya upimaji,kucheleweshwa kusafirishwa ,acha ujinga ,think big
 
Kuna tetesi kuwa kiongozi wa mgomo wa Madaktari aokotwa pande akiwa mahitihuti! Kama habari hii ni ya kweli basi tunakoelekea siko! Ipo siku mafisadi wataburuzwa barbarani!

Ndo umeamka?????

Mod unganisha hizi habari zinatuchanganya sasa!!!!!!
Kila mmoja anaanzisha uzi dah tunachoka sasa!
 
Serikali imetumia kila ustaarabu, mpaka kukubali kuwawachiswa waziri, naibu, katibu mkuu. Kukutana nao, kuongea nao, kuwakubalia kuongeza mishahara, kuwakubalia kuongeza allowances, mpaka kuwaambia sasa tukayamalize kisheria mahakamani lakini msigome, hawasikii.

Hivi wewe, unajuwa watu wangapi wanateseka kwa migomo ya kijinga hii. Nini wanachokitaka zaidi? kama wanavyowatesa wenzao basi na wao watateseka hivyo hivyo, tena sio huyo tu, ni wote na wanaowatumia.

Kwa hiyo ndiop kufikia hatua ya kuua, ina maana ni ruksa kuchukua sheria mkononi.

Usalama wa Taifa ambao tunawategemea wakifanya hivi je, wananchi nao wanaruhusiwa kufanya hivi.

Hii Serikali ya kigaidi mtu akitetea haki basi vitisho vyao ni kumuua.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Wewe una ajenda ya SIRI ya kulipotosha Jukwaa, ndio kwanza una post mbili unaleta RADICAL STATEMENTS; andika vitu vyenye kuleta TIJA na sio UJINGA


PUMBAFFFFFFFFFFF

wewe ndio mpumbafu wa mwisho kabisa mpaka umeenda kwnye NEGATIVE MPUMBAFF.. kama huoni ttz hapo bora unyamaze kuliko kutumiwa na hao wachache ambao leo hii ukipata shida hakuna atakae kujua.. kwa mara ya kwanza
nasikitika hii forum hairuhusi matusi
 
Mimi ninachosema ni kwamba nimesikitika sana na kipigo alichopata Dkt Ulimboka. Aidha nilisikitishwa zaidi na kitendo cha Dkt Ulimboka kutokutii amri halali ya mahakama inayobatilisha mgomo na kuagiza atekeleze agizo hilo kwa kutoa msimamo kwenye vyombo vya habari. Kitendo cha kugoma, licha ya kwamba Mahakama ishatoa agizo; na pia sentiments zilizotolewa na watu/makundi/asasi/taasisi mbalimbali kimetoa ishara kuwa MAT haikuwa tayari kuingia katika majadiliano, na wameamua kutumia nafasi yao kama watabibu kuwaadhibu wanaowatibu ili kuonyesha misuli yao kwa Serikali. Kutafsiri kuwa Serikali ndio inahusika na shambulio kwa Dkt Ulimboka ni jambo ambalo sikubaliani nalo kwa sasa, mpaka ushahidi upatikane utakaoonyesha bayana kuwa Serikali imehusika. Inawezekana Dkt Ulimboka alikusudia kwenda kutekeleza agizo la mahakama, lakini mahafidhina wachache MAT wakaamua kumshughulikia ili kutoa taswira nyengine. Inawezekana pia kuwa kuna watu wana uchungu kuona Watanzania wasio na hatia wanateseka kutokana na mgomo ambao tayari mahakama ya nchi imeuita batili wamechukua hatua mikononi mwao; au kuna masuala ya ugomvi wa Dkt ulimboka nje ya mgomo ambayo yametekelezwa na wabaya wake ili kuficha taswira hiyo. MAPENDEKEZO YA KISIASA KATIKA SUALA HILI, hususan ya kuitisha maandamano sio masuala ya kushabikia kwa sasa. Tuangalie dhahma zinazoendelea Syria na uharibifu wa mali na upotevu wa maisha tujifunze. Kwa sasa Tanzania tunapaswa tuiheshimu sana serikali yetu na kuipa SUPPORT ili tuweze kupata KATIBA MPYA. Masuala ya kuleta vurugu yataturudisha nyuma miaka 500.

Mwisho kabisa, namtakia Dkt ulimboka matibabu mema na apone haraka ili aje kutusaidia katika tiba ya nchi na uongozi wa MAT; na kuwasihi wanachama wa MAT wasigome, na wamuhudumie Dkt Ulimboka na Watanzania wengine sawia.

Wakatabahu


Acha kutupotosha. Dr Ulimboka sio Kiongozi wa MAT, na wala hausiki kabisa na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kabisa, kiongozi wa MAT anaitwa Dr Namala Mkopi na ndiyealiyekuwa na wajibu wa kuzungumza na vyombo vua habari. Aidha unajaribu kujenga hoja kuwa upo uwezekano kuwa Dr Ulimboka kadhuruwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi baada ya kujkos ahuduma za matibabu; huku ni kujaribu kuisafisha serikali ya kidhalimu iliyomtendea Dr ulimboka mateso hkama hayo. Wanancho wote wanatambua kua miongoni mwamadaia ya madakatari ni kuboreshwa kwa mazingira ya utolewaji wa tiba na kuongezwa kwa mafungu ya ununuzi wa vifaa na madawa baada ya vyombo vyote vyenye wajibu wa kuishauri serikali hii dhalimu kama vile bunge n.k kushindwa kuishawishi serikali dhalimu ya CCM kuboresha hudum,a za afya hapa nchini kwa kuongeza bajeti ya afy ilihali fedha na raslimali zetu vikifujwa kwa kuwekwa katika mabemnki ya nje.

Inavyoelekea wewe ni mmoja wa watu mlioratibu zoezi la kumdhuru Dr Ulimboka ili kuleta picha kuwa ni baadhi ya wahafidhina ndani ya MAT. Nafikiri ilikuwa ni jambo la buasara wale wenye fedha huko Uswisi pia mkawafanya hivi hivi
 
nyie ni maiti zinayotembea. Hamjui mtendalo. Mngekaa kule serengeti na nyani na masokwe. Ulimboka atatibiwa na mapambano yanaendelea. ****!!!!!

Ala kumbe siku hizi wavujaji wamezagaa namna hii, acha kuvuja wewe.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
 
Swali langu mi nahoji kwann madaktari wameudumie yeye wakati wamegoma? Mwacheni naye aonje machungu wanayopata wagonjwa hapo hapo Muhimbili kwa kuendeleza mgomo wao, Mkuki kwa Nguruwe sio?

Kwa hiyo serikali imefanya unyama huu, tena kumpeleka msitu wa PANDE ili kueneza propaganda kuwa wao wenyewe wanajitibu?. Kama wewe ni afisa wa serikali utakuwa una akili ndogo sana na hufirii zaidi ya upana wa sahani yako ya chakula. Kilichopo hata si kuwafanya madaktari warudi kazini, hilo ni suala dogo sana kilichopo ni je wanaweza kuwa devoted kwa moyo mkunjufu kuokoa maisha ya wagonjwa?. Hebu fikiria risks wanazokumbana nazo madaktari kazini, kuanzia kuambukizwa magonjwa mpaka kuona graphic images of human remains (during autopsy) au hata upasuaji.

Madaktari wanapaswa kuungwa mkono na wananchi wote, kama wewe uliishashuhudia nduguyo akifariki huku madaktari wakimuangalia na wasijue cha kufanya kwa kusosa madawa au hata vifaa vya kisasa vya kugundua tatizo basi ni lazima uta sympathyse madaktari.
 
jitahidi kujenga hoja acha ushabiki,
ulimboka ni nani awe na thamani kuliko ma elfu ya watanzani wanaoteseka kwa mgomo?
madaktari walipo goma sijaona mtu hata mmoja akiwaita wanyama kwa mateso wanayopata watanzania wasio na hatia kwani wao sio serikali.

Labda umemuelewa vibaya, hajaleta ushabiki bali kakuambia ukampe pole Bi. mkubwa ambaye umesema yupo hospital anajifungua kwa uchungu, acha jazba!!
 

Liwalo na liwe ni ujumbe uliobeba maana nzito lakini hata Muhammar Gadaf aliwahi kuwafananisha wapinzani wake na Panya mwisho wa siku akaishia kujificha kwenye mitaro.Mtoto wa mkulima ukumbe umefika mahali pake.


480093_416306165079474_1787286762_n.jpg
 
Ulimboka hasiefunzwa na mamaye hufunzwa na dunia....umepata unachostahili na umejua ni namna gani wagonjwa tuna maumivu.....bravo kwa yeyote alimshughulikia muhaini Ulimboka.
 
we ndio mshabiki mpumbafu kabisa huna soni,kabisa wananchi wameanza kufa leo, wanakufa kila siku kwa kukosa hata dawa ya kuzuia damu wakizaa,kukosa nyuzi za kushonwa ,unambiwa scan machine hazifanyi kazi ocean road,muhimbili kwenyewe,x-ray ni mikoa kumi tu zinafanya kazi,zahanati asilia 51 hazina watendaji,ambulance zimeletwa pikipiki ,watoto wanakufa kila siku kwa kukosa oxygen mie sio mjinga mwenzio naipenda nchi hii na sitakubali ujinga wa baba yako mtawala mbumbumbu anayepeleka nchi yetu kwenye moto wa petroli

Najua utaniita mpumbavu ukijifanya eti ni mwanaharakati lakini kimsingi pamoja na takwimu zako uchwara bado hufikiri kwa makini,
hivi kama mama au baba yako angekua ICU sasa,ungekua na hicho kiburi chakuwataka waendelee kugoma?
najua kinachokusumbua ni siasa za vyama au ushabiki.
 
Napata shida kidogo kwamba nikupe pole wewe au wale wagonjwa ambao kwa lengo lenu la kugoma na kuiwajibisha serikali wengi wanateseka,wengine wanakufa,mama zetu wanajifungua kwa uchungu bila ya kua na msaada wowote,haya ni mateso makubwa,
Hemu tujiulize vipi kama ulimboka na yeye kama akitelekezwa aachwe bila ya huduma yoyote?
ni vyema madaktari watafute njia tofauti yakuibana serikali kwani watanzania wasio na hatia wanakufa kwa kosa la serikali
Wewe mshamba nini hivi unaona staili gani iliyobaki yakuwabana hawa mafisadi, unadhani ni halali wao wanajitibu kwa Bilioni 9 nchi za nje wakati hospitali za serikali zimetengewa bilioni 4
icon8.png
 
Tunaomba chama cha madaktari kuusimamia usalama wa huyu kamanda popote atakapokuwa kwani hawa jamaa wanaweza kuwa wameshampiga sumu na pia wanaweza kumrudia. "KUMBUKENI MABWEPANDE NI YA ZOMBELIZATION siyo ya maigizo, so kama mtu kafikishwa huko alikuwa amekwisha"

Kwa hili serikali haiwezi kukwepa kwani tangu jana naibu mwanasheria mkuu wa serikali alishapiga mkwara kwamba leo tutaona na leo PM bungeni amesema liwalo na liwe na ndiyo tumeshaanza kuliona kabla ya hata serikali haijatoa tamko juu ya huu mgomo wa madaktari. aluta continua
 
Nadhani serikali dhaifu huamua mambo dhaifu.

Waandishi watachukua picha humu, ni vizuri zingekuwa zinawekewa copyrit ya jf au sign inayo onesha imetoka jf.
 
hapa jambo la msingi ni kuchukua HATUA kuitisha maandamano nchi nzima ya kulaani kitendo hicho , iwe au isiwe serikali lakini maadam imetokea wakati suala liko katika wakati mgumu basi serikali iwajibike
 
Acha kutupotosha. Dr Ulimboka sio Kiongozi wa MAT, na wala hausiki kabisa na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kabisa. Inavyoelekea wewe ni mmoja wa watu mlioratibu zoezi la kumdhuru Dr Ulimboka ili kuleta picha kuwa ni baadhi ya wahafidhina ndani ya MAT. Nafikiri ilikuwa ni jambo la buasara wale wenye fedha huko Uswisi pia mkawafanya hivi hivi

Tuelimishe Dkt Ulimboka ni Kiongozi wa nani?

Na Je yeye anahusika vipi na Mgomo huu?

Je Dkt Ulimboka hana ushawishi MAT?

Kama Dkt Ulimboka hana ushawishi MAT na hana influence kwenye mgomo; kwanini TUHUMA zisizo vielelezo zinatolewa dhidi ya Serikali?

Mimi naamini kuwa Serikali yenyewe inasikitishwa na tukio hili; ila kwa kuwa watu mumeona mambo yakitokea Syria na Misri; basi mumeanza kukomaa. EVENTUALITY YA INCITEMENT SIO SUALA UTAKALOLIPENDA. Tuendelee na salama yetu na tuitake Katiba Mpya ije mapema na haraka. vurugu hazina tija. katiba Mpya Muarobaini wa mengi.
 
OOOh My GOD, I feel tears shed my eyes

Sidhani kama itatokea maishani mwangu nikaipenda tena SERIKALI YA CCM!

Kama Mungu yupo pamoja nasi atakuponya Dr. Ulimboka. Our prayers are with you

Amevunjwa mikono yote miwili,shingo na sehemu za siri zimeasiwa.Hii taarifa kutoka chanzo cha uhakika kutoka muhimbili
 
Back
Top Bottom