SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 3,577
- 5,664
Simba ina watu kama si wajuaji kupitiliza basi ni wazembe sana... kuna vitu kwenye mpira vinaonekana wazi na havihitaji kuwa na degree ya sayansi ya mpira wala kuwa kocha.
Msimu wa 2024/25 wakati unatamatika kipindi kile kila mtu aliona kuwa genge la Mutale na nduguze kwenye safu ya kiungo ushambuliaji ni magalasa, lakini dirisha kubwa Simba wakaona wanajua sana wakawa wanasingizia makocha na kufukuza kila uchwao... Maji yalipofika shingoni walisajili watu stahiki..
Msimu uliofuata wa 2025/26 mapungufu makubwa ya wazi yalionekana bila kupepesa ni KIPA na STRAIKA maana mpaka inafikia mtu kama MPANZU ndo mtu wa mwisho wa timu kama Simba ujue kuna shida,, lakini kuna wajanja wanatuambia KIPA anafaa na wakaleta na PA OMAR JOBE mwingine ambaye hata mstaafu JOHN BOCCO anamzidi...
La kushangaza huyu KIPA anafungwa goli la aina moja mpaka unajiuliza kwani timu haina KOCHA WA MAKIPA ??
Kwa hili genge lililopo Simba hata msimu huu ni kama ya msimu uliopita..