SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 3,577
- 5,664
Uliyoongea ukweli mtupu. Yule kipa ni shati kabisa. Barker amewaonyesha viongozi aina gani ya wachezaji wa kusajili. Siku akiondoka Simba itarudi kwenye sajili za akina Mutale. Pale uongozi una shida.Simba ina watu kama si wajuaji kupitiliza basi ni wazembe sana... kuna vitu kwenye mpira vinaonekana wazi na havihitaji kuwa na degree ya sayansi ya mpira wala kuwa kocha.
Msimu wa 2024/25 wakati unatamatika kipindi kile kila mtu aliona kuwa genge la Mutale na nduguze kwenye safu ya kiungo ushambuliaji ni magalasa, lakini dirisha kubwa Simba wakaona wanajua sana wakawa wanasingizia makocha na kufukuza kila uchwao... Maji yalipofika shingoni walisajili watu stahiki..
Msimu uliofuata wa 2025/26 mapungufu makubwa ya wazi yalionekana bila kupepesa ni KIPA na STRAIKA maana mpaka inafikia mtu kama MPANZU ndo mtu wa mwisho wa timu kama Simba ujue kuna shida,, lakini kuna wajanja wanatuambia KIPA anafaa na wakaleta na PA OMAR JOBE mwingine ambaye hata mstaafu JOHN BOCCO anamzidi...
La kushangaza huyu KIPA anafungwa goli la aina moja mpaka unajiuliza kwani timu haina KOCHA WA MAKIPA ??
Kwa hili genge lililopo Simba hata msimu huu ni kama ya msimu uliopita..
Hapo kwa Maema ndio paliniacha hoi maana dili lake lina ukakasi mkubwa sana. Neo Maema alikuwa amemaliza mkataba wake na Mamelodi halafu akarudi kwanza Mamemlodi akasaini mkataba mpya halafu ndio Simba ikamchukua kwa mkopo. Ninavyojua wachezaji wote duniani wakimaliza mkataba wanakimbilia kusaini mikataba kama free agents ili wapate pesa nyingi lakini kwa mara ya kwanza nimeona vice vers kwa Maema.Magori ndio anajifanya yeye ndio kila kitu, baada ya usajili wa diriaha dogo kuwa mzuri alitaka yeye na mo ndio wapate sifa.
Ahmed Ally anamsifia kwa kumleta kibabage hovi mchezaji kama kibabage ndio unategemea atakubeba kimataifa.
Simba ilikuwa na mawinga wa kutosha lakini haikuwa na namba tisa ndio maana ilikuea inatumia mfumo wa false namba nine ila mchezaji wa kwanza kusajiliwa ni winga tena wa kimataifa. Maema wamemng'ang'ania wakati ni mchezaji wa kawaida.
Huyo kocha kama kaja kutafutia vibarua ndugu zake nae piga chini.