Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Nimekuwa nikiona mijadala mbalimbali ikiendelea hapa wakishindanishwa magolikipa diarra na Manura kwamba nani ni bora, Naweza kusema golikipa Djigui diarra kuna vitu vingi sana kamzidi manura achilia mbali kufanya vizuri kwenye ligi ya Tanzania, uyu diarra walio wengi wamekuja kumjua aliposajiliwa yanga lakini kl4abla ya hapo awajui ni mchezaji wa aina gani na amepitia kwenye njia zipi mpaka amefikia apo alipo, kuna baadhi wanakimbilia kusema manura ni bora kuliko diarra kwa kuwa eti ameifikisha simba robo fainali ya confederation cup, lakini hapo hapo awajui uyo diarra kacheza kombe la dunia under 20, under 23, kacheza chan nusu fainali mara kibao na bado anaendelea kuitwa timu ya taifa ya Mali mpaka sasa hivi, kitendo cha kuitwa timu ya taifa ya Mali ata kama ajapata nafasi ya kucheza ni wake up call ya kukujulisha ya kuwa uyo bwana kiwango chake kiko vizuri, Jana nimeona wachezaji walioitwa timu ya taifa ya Mali akuna mchezaji ata mmoja anaecheza pale Mali bali wote wanacheza ulaya na ni mchezaji mmoja tu anaecheza barani Africa aliyeitwa nae sio mwingine ni Djigui Diarra anaecheza yanga ya Tanzania, Kwa namna yoyote ile uwezi kulinganisha namna Mali walivyo na utitiri wa wachezaji bora wanaokipiga nje ya taifa lao na Tanzania, utakuwa unawakosea heshima, Kwaiyo kupata nafasi tu ya kuitwa timu yao ya Taifa basi uwe umefanya kazi ya ziada na sio ya kitoto, Manura anaweza kubaki kuwa kipa bora kwa magolikipa wetu wa kitanzania hapa kwakuwa baada ya kina Mwamed mwameja, juma kaseja sijaona kipa mwingine ambae anaweza kumchalenji kwa sasa kwenye soka letu la Tanzania, wengi viwango vyao ni vidogo sana, lakini unapokuja kwenye suala la kumshindanisha na makipa wa kigeni waliopo hapa kwa sasa bado anaendelea kuwa chini ya diarra kivyovyote vile, Tuchukue mfano mdogo tu uyo Manura angekuwa ni raia wa Mali na kocha wa Mali akapewa achague kati ya Manura na Diarra unafikiri angemchagua nani kwenye timu ya taifa ilo ukiwaondoa makipa alioita ibrahim mounkoro wa tp mazembe na yule wa Malmo ya Italia? Kwaiyo mi nafikiri Manura abaki na umanura wake hapa tanzania na Diarra abaki kama diarra