Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna kusoma kuelewa na kusoma kuwahi kucomment.Hatuwezi kumpima kwa timu za Mbeya kwanza , Prison na Biashara. Subiri kimataifa ndo ulete hoja yako Maana mechi zote za kimataifa tena kwa vitimu dhaifu alipasuliwa kama hayumo golini vile.
Zanaco na kapumbu wake walimtia 2
Rivers na kitompe wake walimtia 2.
Ko tuvute subira kwanza akifanya vizuri kimataifa haki yake tutampa tu kama anastahili.
Zile mechi na Rivers United zilikuwa ndondoYuko vizuri tunasubiri kumuona kwenye michuano ya kimataifa
Unaboa, H unamwachia nani? Shule ulisoma ujinga?Nimekuwa nikiona mijadala mbalimbali ikiendelea hapa wakishindanishwa magolikipa diarra na Manura kwamba nani ni bora, Naweza kusema golikipa Djigui diarra kuna vitu vingi sana kamzidi manura achilia mbali kufanya vizuri kwenye ligi ya Tanzania, uyu diarra walio wengi wamekuja kumjua aliposajiliwa yanga lakini kl4abla ya hapo awajui ni mchezaji wa aina gani na amepitia kwenye njia zipi mpaka amefikia apo alipo, kuna baadhi wanakimbilia kusema manura ni bora kuliko diarra kwa kuwa eti ameifikisha simba robo fainali ya confederation cup, lakini hapo hapo awajui uyo diarra kacheza kombe la dunia under 20, under 23, kacheza chan nusu fainali mara kibao na bado anaendelea kuitwa timu ya taifa ya Mali mpaka sasa hivi, kitendo cha kuitwa timu ya taifa ya Mali ata kama ajapata nafasi ya kucheza ni wake up call ya kukujulisha ya kuwa uyo bwana kiwango chake kiko vizuri, Jana nimeona wachezaji walioitwa timu ya taifa ya Mali akuna mchezaji ata mmoja anaecheza pale Mali bali wote wanacheza ulaya na ni mchezaji mmoja tu anaecheza barani Africa aliyeitwa nae sio mwingine ni Djigui Diarra anaecheza yanga ya Tanzania, Kwa namna yoyote ile uwezi kulinganisha namna Mali walivyo na utitiri wa wachezaji bora wanaokipiga nje ya taifa lao na Tanzania, utakuwa unawakosea heshima, Kwaiyo kupata nafasi tu ya kuitwa timu yao ya Taifa basi uwe umefanya kazi ya ziada na sio ya kitoto, Manura anaweza kubaki kuwa kipa bora kwa magolikipa wetu wa kitanzania hapa kwakuwa baada ya kina Mwamed mwameja, juma kaseja sijaona kipa mwingine ambae anaweza kumchalenji kwa sasa kwenye soka letu la Tanzania, wengi viwango vyao ni vidogo sana, lakini unapokuja kwenye suala la kumshindanisha na makipa wa kigeni waliopo hapa kwa sasa bado anaendelea kuwa chini ya diarra kivyovyote vile, Tuchukue mfano mdogo tu uyo Manura angekuwa ni raia wa Mali na kocha wa Mali akapewa achague kati ya Manura na Diarra unafikiri angemchagua nani kwenye timu ya taifa ilo ukiwaondoa makipa alioita ibrahim mounkoro wa tp mazembe na yule wa Malmo ya Italia? Kwaiyo mi nafikiri Manura abaki na umanura wake hapa tanzania na Diarra abaki kama diarra
Muda mwingine ukae kimya sio kuja kuhara humu, unasahau hiyo 2019 huyo Manula alipigwa 5,5,4.Kipa anapopimwa kwa mafanikio ya team ya Taifa huwa nashangaa sana. Vipi kwenye Club hachezi?
Unavyosema manura mafanikio yake ni kuifikisha Simba robo fainali Confederation Cup, bado nashangaa.
Ni huyu huyu Manura aliyecheza Ligi ya mabingwa msimu uliopita Mechi kumi kabla ya robo fainali na kuruhusu bao 2 pekee?
Ni huyuhuyu manura aliyeongoza kwa saves AFCON 2019 group stages?
Staki kuzungumzia ligi kuu maana ni kufuru itakuwa, kafanya makubwa mno zaidi ya mara tano kama sio Sita mfululizo anakuwa kipa bora kwenye ligi yetu.
Ni vizuri kushangilia ila Usishangilie kipumbavu,
Huwezi tumia team za taifa za Vijana kupima mafanikio ya mchezaji ( ndio maana yanaitwa ya vijana, hakuna userious huko).
Ni mashindano hayo ya Vijana ambayo wachezaji sio pro unataka kutumia kumpima Diarra kama ni bora.
Asa najiuliza inamaana huyu mtu alicheza team ya vijana tu mpira wake ukaishia hapo?
Hakuwahi cheza Club? Vipi huko?
Tuache Masikhara Jamani, tukiacha story za kina Mwameja ambao hatujawaona wengi wetu ( Hata kama ulikuwepo nna uhakika hujawaona, hakukuwa na TVs wakati huo, kuwaona ni
Mpaka uwanjani. Ntashangaa mtu wa Rukwa ukisema uliwaona kina Pazi wakati Ulikuwa kwenu Sumbawanga) Manula ndie kipa bora Kuwahi kutokea Tanzania. ( kwa niliowashuhudia).
Imekuwa kuhara tena?Muda mwingine ukae kimya sio kuja kuhara humu, unasahau hiyo 2019 huyo Manula alipigwa 5,5,4.