Kipa na Beki Kagera Sugar wasimamishwa kwa tuhuma ya kuhujumu dhidi Yanga SC

Kipa na Beki Kagera Sugar wasimamishwa kwa tuhuma ya kuhujumu dhidi Yanga SC

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Wakuu kama mnavyokumbuka timu ya Kagera Sugar ilifungwa na Yanga ya Dar jumla ya Goli 6 kwa 2. Na kama mnavyokumbuka Yanga imekuwa ikishutumiwa kununua ama timu nzima au baadhi ya wachezaji ili kurahisha mazingira ya ushindi wa kimbunga.
======================

Uongozi wa Kagera Sugar umewasimamisha wachezaji wake wawili golikipa Hussein Sharif ‘Casillas’ na beki Erick Kyaruzi kwa tuhuma za kuihujumu timu wakati wa mchezo wa liopoteza kwa kufungwa magoli 6-2.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo Hamisi Madaki amethibisha kuwasimamisha wachezaji hao kwa muda usiojulikana kwa ajili ya kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazowakabili.

“Tunaendelea na uchunguzi kwasababu kunaonekana kulikuwa na hujuma katika mechi yetu na Yanga kwahiyo tumeona tuendelee na uchunguzi na tumeona wakae kando wakati tunaendelea na uchunguzi huo.”

“Aina ya magoli tuliyofungwa kila mtu aliyaona na yanatia wasiwasi mkubwa. Suala sio idadi ya magoli suala ni aina ya amagoli mtu aliayofungwa, hata kama ni goli moja lakini kama linatia wasiwasi lazima tuchukue hatua.”

“Makosa ya namna ile hatukuridhika nayo ndiyo maana tunafanya uchunguzi. Hata beki goli alilofungisha unaona dhahiri kwamba halikupashwa kuwa goli ndiyo maana tunafanya uchunguzi.”

“ nikiwa kama Mtendaji mkuu wa klabu, hiyo taarifa sina sisi tumewasimamisha na hata barua tulizowaandikia tumesema tumewasimamisha . Suala la kuwaondoa kabisa hilo siwezi kulisemea, taarifa nilitoa mbele ya wachezaji na benchi la ufundi baada ya kukaa viongozi na benchi la ufundi tulikubaliana kuwasimamisha.”

“Tumewasimamisha kwa muda usiojulikana mpaka tukamilishe uchunguzi, hii si mara ya kwanza watu wanasahau historia, tumeshawahi kusimamisha wachezaji na kuwafukuza kabisa hapo kabla.”

Katika mchezo huo, Hussein Sharif alifungwa magoli matatu kipindi cha kwanza kabla ya kufanyiwa mabadiliko kumpisha David Burhani ambaye pia alifungwa magoli matatu.

Kyaruzi yeye alirudisha pasi fupi kwa golikipa wake ambapo Donald Ngoma aliuwahi mpia huo na kufunga bao.

TAKUKURU fanyika kazi hii timu inatia aibu Taifa.
c.c Makoye Matale na sembo
 
Wakuu kama mnavyokumbuka timu ya Kagera Sugar ilifungwa na Yanga ya Dar jumla ya Goli 6 kwa 2. Na kama mnavyokumbuka Yanga imekuwa ikishutumiwa kununua ama timu nzima au baadhi ya wahezaji ili kurahisha mazingira ya ushindi wa kimbunga.
Taarifa zinazosomwa Azam TV zinasema kuwa Wachezaji wawili wa Kagera Sugar, Husein Sharifu 'Casillas Munyama' na Erick Kyaruzi wamesimamishwa na kuondolewa kambini.Wanatuhumiwa kupewa mlungura na Yanga katika kipigo cha 6-2.

TAKUKURU fanyika kazi hii timu inatia aibu Taifa.
c.c Makoye Matale na sembo

Haya majungu, kama wanaushahidi wapeleke kwenye taasisi ya rushwa
 
Kocha sio shabiki lialia kweli kwa timu hiyo ilio chapwa six
 
Nakumbuka wakati ule Arsenal walichukua rushwa wakapigwa nane na Man U.
Baadaye nao Man U ya babu Ferguson wakachukua rushwa na kupigwa 6 na Man City.
Teh teh, Yanga bhana juzi tena wamehonga mtu wakashinda 4 bila.
Yule mwingine akishinda 3 bila ni kwa ubora wake tu. Teh teh teh
Nani anabisha?
 
Nakumbuka wakati ule Arsenal walichukua rushwa wakapigwa nane na Man U.
Baadaye nao Man U ya babu Ferguson wakachukua rushwa na kupigwa 6.
Teh teh, Yanga bhana juzi tena wamehonga mtu wakashinda 4 bila.
Yule mwingine akishinda 3 bila ni kwa ubora wake tu
Nani anabisha?
Umetisha mkuu kuna watu humu kila yanga ikishinda basi imehonga, mkia akishinda basi kwa uwezo wake.... Sasa sijui yanga ina muhimu gani kununua wachezaji wa ghali na kulipa mishahara mikubwa ikiwa inaweza kununua mechi
 
Simba haijawahi hawa kuwaziwa kununua mechi, lakini kwa nini Yanga tu. Kagera sugar sio wajinga kusimamisha wachezaji
 
Simba haijawahi hawa kuwaziwa kununua mechi, lakini kwa nini Yanga tu. Kagera sugar sio wajinga kusimamisha wachezaji
Hizi huwa ni story tu kiongozi hakuna mtu aliyewahi kuthibitisha kuhongwa lazima tuwe wa kweli team ya yanga nayo ipo vizuri kiuchezaji, wanawachezaji mahiri kabisa, tujaribu kuwa wa kweli katika kukubari matokeo
 
Wakuu kama mnavyokumbuka timu ya Kagera Sugar ilifungwa na Yanga ya Dar jumla ya Goli 6 kwa 2. Na kama mnavyokumbuka Yanga imekuwa ikishutumiwa kununua ama timu nzima au baadhi ya wahezaji ili kurahisha mazingira ya ushindi wa kimbunga.
Taarifa zinazosomwa Azam TV zinasema kuwa Wachezaji wawili wa Kagera Sugar, Husein Sharifu 'Casillas Munyama' na Erick Kyaruzi wamesimamishwa na kuondolewa kambini.Wanatuhumiwa kupewa mlungura na Yanga katika kipigo cha 6-2.

TAKUKURU fanyika kazi hii timu inatia aibu Taifa.
c.c Makoye Matale na sembo
Basi mkia nawo wanauza mechi
 
Simba haijawahi hawa kuwaziwa kununua mechi, lakini kwa nini Yanga tu. Kagera sugar sio wajinga kusimamisha wachezaji
na WA Jana VP acheni propaganda ,mabingwa WA kusambaza hizi habari Ni mashabiki WA simba,kila yanga akishinda kahonga na bado dozi zitaendelea Tu subiri mbao nae mtasema kauza game
 
Hizi huwa ni story tu kiongozi hakuna mtu aliyewahi kuthibitisha kuhongwa lazima tuwe wa kweli team ya yanga nayo ipo vizuri kiuchezaji, wanawachezaji mahiri kabisa, tujaribu kuwa wa kweli katika kukubari matokeo
Kweli Mkuu hvi kwa nn Yanga mpk leo haijawahi kusikia ikimsema Ally Mustapha kwa magoli anayofungwa na Simba kuwa anauza mechi tena ya kizembe sana
 
Kweli Mkuu hvi kwa nn Yanga mpk leo haijawahi kusikia ikimsema Ally Mustapha kwa magoli anayofungwa na Simba kuwa anauza mechi tena ya kizembe sana
Mkuu mashabiki wengi wa simba ni shida huwa wanaamini simba ndo inapaswa kushinda game tu, ikishinda yanga kahonga.... Simba anaongoza lingi sasa umesikia shabiki wa yanga akipiga kelele simba ananunua mechi au anapendelewa!?
 
Huu msimu wanautaka ubingwa kwa hali na mali ss wao nadhani ndyo mchezo wanaoutumia kuutafuta huo ubingwa Mkuu na hawataupata n'goooo kwa spidi hii ya game mbili tu goli kumi cjui ngoja si wameanza kutoka game za nje tuone umwamba wao na huko
 
Hv kule IPIELO Maniyu wamemsimamisha nani Kweli wakuu wangu??? baada ya kale kakipigo kadogo toka Cheisiii!!! ni Baily au Blind??? au De gea
 
Back
Top Bottom