Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Golikipa wa zamani wa timu za Majimaji ya Songea, Simba Sc na Yanga Sc, Doyi Moke raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amefariki Dunia baada ya kuchomwa moto na Wananchi wenye hasira kali
Inaelezwa asubuhi ya Machi 6, 2025 Doyi ambaye alikuwa tayari amepatwa na matatizo ya akili na amekuwa akitembea barabarani kama ‘chizi’ alitoka kwake akielekea nyumbani kwa mwanaye ambapo mahali alipoenda huko Bukavu kuna wafungwa ambao walitoka gerezani na walishakuwa na tabia ya kuwaingilia watu ndani na kuwaibia vitu.
Kwa hiyo Wananchi waliamua kujichukulia Sheria mkononi kutokana na kitendo cha wafungwa hao kufanya vitendo hivyo ambapo inaelezwa kuwa Wananchi walikutana na Doyi ambaye alikuwa anatoka kwa mwanaye na kumjumuisha miongoni mwa wahalifu hao.
Wananchi hao walimfunga minyororo sambamba na watu wengine watatu na kumchoma moto kama inavyoonekana pichani.