Kipengele cha kuwabeba Polisi wasishtakiwe katika Muswada mpya chafutwa na Serikali

Kipengele cha kuwabeba Polisi wasishtakiwe katika Muswada mpya chafutwa na Serikali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
1644389078824.png

Serikali imefuta Ibara ya 24 iliyokuwa inapendekeza kifungu kipya 47A kwa lengo la kutoa mamlaka kwa polisi kufanya operesheni za kificho kwa madhumuni ya kuzuia utendaji wa makosa.

Akitoa taarifa mbele ya Bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi amesema kwamba katika Muswada huo wa Sheria ya Marekebisho mbalimbali na 7 uliopitishwa hapo jana, kifungu hicho tata kimeondolewa rasmi.

Awali tangu kuzuka kwa taarifa za kupelekwa kwa muswada huo kwa hati ya dharura, kuliibuka kwa maswali na sintofahamu kwenye mitandao ya kijamii ikihoji mantiki ya kuwakingia kifua askari polisi endapo watafanya jinai na kuhalalisha mauaji ya raia.

Maoni ya wananchi hao yanakuja ikiwa siku chache tangu Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuonesha kushangazwa kwake na hatua ya jeshi la Polisi nchini kupitia mkuu wake IGP Simon Sirro kutangazia umma kwamba jeshi hilo limeunda tume kuchujichunguza kwa madai ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini mkoani Mtwara Mussa Hamisi (25).

Hivi karibuni kumekuwa na mlolongo wa matukio ya ukiukwaji wa kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi jambo linalotajwa kuitia doa serikali, licha ya matamko kadhaa ya viongozi wa nchi kutaka jeshi hilo lijitafakari.
 
IMG-20220209-WA0003.jpg

===
Kelele zetu za kupinga kipengele kinachotaka Polisi awapo kwenye majukumu yake na akitenda jinai asishitakiwe kimeifikia Serikali na tayari AG Feleshi amesema kifungu hicho chote cha 47A kimeondolewa kwenye muswada.

Sasa muswada wa Sheria ya Marekebisho mbalimbali Na.7 uliopitishwa jana na Bunge umefanyiwa marekebisho.
 
Kwa hiyo, kwanza kilipitishwa na Bunge (maana yake wabunge hawakuona umuhimu wa kukiboresha) hadi Rais asikie kilio cha wananchi? Kama ni kweli, then naona hapa wabunge wametukosea sana kama wawakilishi wetu.

Ndiyo maana kilitakiwa kile kipengele cha 'Katiba ya Warioba' kuhusu wapiga kura kuwaajibisha wawakilishi wao (wabunge wa kuchaguliwa) kiwekwe kwenye Katiba yetu ya sasa au kama tukiwa na Katiba Mpya kirejeshwe maana kiliondolewa kwenye ile Katiba iliyopendekezwa kwa wakati ule iliyokuwa ikijulikana kwa jina la "Katiba iliyochakachuliwa".
 
Kwa hiyo, kwanza kilipitishwa na Bunge (maana yake wabunge hawakuona umuhimu wa kukiboresha) hadi Rais asikie kilio cha wananchi? Kama ni kweli, then naona hapa wabunge wametukosea sana kama wawakilishi wetu. Ndiyo maana kilitakiwa kile kipengele cha 'Katiba ya Warioba' kuhusu wapiga kura kuwaajibisha wawakilishi wao (wabunge wa kuchaguliwa) kiwekwe kwenye Katiba yetu ya sasa au kama tukiwa na Katiba Mpya kirejeshwe maana kiliondolewa kwenye ile Katiba iliyopendekezwa kwa wakati ule iliyokuwa ikijulikana kwa jina la "Katiba iliyochakachuliwa".
Hayo ni maoendekezo ya mabadiliko ya sheria ndio waliweka hicho kifungu na kimeondolewa kabla ya wabunge kukijadili.
 
Kwa hiyo, kwanza kilipitishwa na Bunge (maana yake wabunge hawakuona umuhimu wa kukiboresha) hadi Rais asikie kilio cha wananchi? Kama ni kweli, then naona hapa wabunge wametukosea sana kama wawakilishi wetu...
Hata rais nae ni mpenda sifaa tuu.kwani kabla ya kuupeleka bungeni balaza la waziri ambalo yeye ni mwenyekiti wa kikao, hawakuujadili kwanza huo muswaada?
 
View attachment 2113292
===
Kelele zety za kupinga kipengele kinachotaka Polisi awapo kwenye majukumu yake na akitenda jinai asishitakiwe kimemfikia Rais Samia Suluhu Hassan na tayari amemuagiza AG Feleshi kukichomoa kifungu hicho...

Mama anajua anachokifanya na hulka ya Polisi wetu anaijua.

Safi sana Mama uishi miaka mingi
 
Kwa hiyo, kwanza kilipitishwa na Bunge (maana yake wabunge hawakuona umuhimu wa kukiboresha) hadi Rais asikie kilio cha wananchi? Kama ni kweli, then naona hapa wabunge wametukosea sana kama wawakilishi wetu...
Bunge hili ni la 100%, kila kitu 100%, hakuna hapana, sijui au imeharibika.
 
Hao wabunge chochote kinachopelekwa na serikali lazima wakipitishe, kitu pekee watapinga ni malipo yao kupunguzwa.
Kama ni kweli raisi aliagiza kiondolewe kifungu kwenye mswaada uliopo bungeni (unajadiliwa), hilo ni kosa la kikatiba. Raisi hana mamlaka ya kuagiza mswaada unaojadiliwa kubadilishwa bila kuongea na wahusika na kuwasikiliza maoni yao. Na haya maongezi yangefanywa baada ya kuondolewa mswaada bungeni na baadaye akaurudisha bungeni wakikubaliana. Au angefuata sheria na utaratibu angeungoja huo mswaada upitishwe na akaungoja ofissini kwake ambapo angekataa kutia sahihi, na kuurudisha bungeni na maelekezo kwa nini hakuutia sahihi. Baada kurudishwa bunge lingeweza kuurudisha kwake bila mabadiliko ambapo ingetegemea umepitishwa kwa wabunge kiasi gani. Kama ni theluthi mbili au zaidi ingekuwa ndiyo mwisho wa mchezo, raisi hana uwezo kwa kukataa..yaani analazimika kuutia sahihi. Kama ni chini ya theluthi mbili, angevunja bunge na kuitisha uchaguzi.

Mimi sitetei hicho kipengele kuwepo ila naona kuna athari nyingi kwa raisi kuchukuwa simu na kupiga bungeni kuagiza kipengele fulani kuondolewa. Kwa sasa kuna wale wanaoshangilia kwa sababu ni kweli hicho kipengele kilikuwa na matatizo na ukakasi, hasa pale police anapewa immunity kuondolewa liability akitenda makosa ya jinai. Lakini kuna siku nyingine raisi anaweza pia kunyanyua simu kutaka mabadiliko au kuondolewa kifungu ambacho labda sisi wananchi tunakitaka. Je, akifanya hivyo tutamwambia anaingilia shughuli za bunge? Je kikija kifungu cha kumuajibisha raisi mstaafu kwa makosa ya jinai aliyotenda akiwa kazini au baada ya kustaafu unafikiri atakubali kujitia kitanzi? Akitoa agizo kifungu hicho kiondolewe tutalalamika ameingilia bunge?

Raisi anayo nafasi yake ya kikatiba ya kukataa sheria au vifungu katika sheria. Anatakiwa avitumie hivyo vifungu na siyo kutoa amri mabadiliko yafanyike. Kama hili limeongelewa mitandaoni na akazibuka angetumia taratibu aliyopewa na katiba na siyo kutumia taratibu ambayo anakatazwa na katiba kuinjgilia mihimili mingine. Kwa wale MACHADEMA kuweni waangalifu kushangilia bila kufanya "critical analysis" ya mnachokishangilia. Kama ninyi ni waumini wa kufuata katiba ama hii au ile mnayodai, cha muhimu kwenu ni kuifuata katiba na siyo kuingia kwenye mitego midogo kama hii. Mimi nakubaliana na yule aliesema raisi SSH anatafuta kiki na sifa ndogondogo bila kugundua athari zake za uvunjivu wa katiba aliyoapa kuisimamia na kuitii. Katiba inamtaka asiingilie mihimili mingine (bunge/parliament na mahakama/judiciary).
 
Back
Top Bottom