Kipengele cha kuwabeba Polisi wasishtakiwe katika Muswada mpya chafutwa na Serikali

Kipengele cha kuwabeba Polisi wasishtakiwe katika Muswada mpya chafutwa na Serikali

Raisi kaagiza bunge mojawapo ya idara ya serikali... Au alipelekewa mswada akakataa!??
 
View attachment 2113292
===
Kelele zety za kupinga kipengele kinachotaka Polisi awapo kwenye majukumu yake na akitenda jinai asishitakiwe kimemfikia Rais Samia Suluhu Hassan na tayari amemuagiza AG Feleshi kukichomoa kifungu hicho.

Sasa muswada wa Sheria ya Marekebisho mbalimbali Na.7 uliopitishwa jana na Bunge utafanyiwa marekebisho.

Sasa ni rasmi Serikali imefuta Ibara ya 24 iliyokuwa inapendekeza kifungu kipya 47A.

Lengo la kifungu hiki lilikuwa ni kutoa mamlaka kwa Polisi kufanya operesheni za kificho kwa madhumuni ya kuzuia utendaji wa makosa - AG Feleshi, alilieleza Bunge
Hata Humphrey Polepole alikuwa amekipitisha?
Kweli Bunge letu limejaa wanafiki.
 
View attachment 2113292
===
Kelele zetu za kupinga kipengele kinachotaka Polisi awapo kwenye majukumu yake na akitenda jinai asishitakiwe kimeifikia Serikali na tayari AG Feleshi amesema kifungu hicho chote cha 47A kimeondolewa kwenye muswada.

Sasa muswada wa Sheria ya Marekebisho mbalimbali Na.7 uliopitishwa jana na Bunge umefanyiwa marekebisho.
Kupiga kelele kwa watu wasiostahili ni utovu wa nidhamu,humu ndani watu walikomaa ooh Rais afute nikawa nawajibu badala wawaambie walioko Bungeni wanakuja kwa Rais as if Rais yuko Bungeni kujadili mswaada.
 
Mama nimekupenda bure. Umefanya kitu kizuri maana hiki kipengele kilikuwa kimehalalisha ugaidi wa polisi dhidi ya kila mtu ukiwemo wewe mama hangaya. Heko muheshimiwa karibu kwangu update chai kesho hapa buseresere
Mwendelezo wa yaleyale,unatengeneza tatizo halafu unalitatua na vigelegele unapigiwa!Si ndio kama Yale mambo ya kikokotoo yalivyokuwa!
 
Sio mama,kuna wabunge kule tena wanasheria,mama yuko Bungeni?
Wabunge ni mapoyoyo tu!Si ndio wao walipitisha tozo,kikokotoo?Wao wanajua jambo linaloletwa na serikali kazi Yao ni kusema ndiooooooo!
Taarifa ya AG inasema serikali imeamua kufuta kipengele chote Cha 47!
Kwa akili Yako serikali ni Bunge?
 
Kwa hiyo, kwanza kilipitishwa na Bunge (maana yake wabunge hawakuona umuhimu wa kukiboresha) hadi Rais asikie kilio cha wananchi? Kama ni kweli, then naona hapa wabunge wametukosea sana kama wawakilishi wetu.

Ndiyo maana kilitakiwa kile kipengele cha 'Katiba ya Warioba' kuhusu wapiga kura kuwaajibisha wawakilishi wao (wabunge wa kuchaguliwa) kiwekwe kwenye Katiba yetu ya sasa au kama tukiwa na Katiba Mpya kirejeshwe maana kiliondolewa kwenye ile Katiba iliyopendekezwa kwa wakati ule iliyokuwa ikijulikana kwa jina la "Katiba iliyochakachuliwa".
Wapiga kura wanawawajibishaje hao wawakilishi wao??

Ni nani anaetoa muongozo wa namna ya kuwawajibisha hao wawakilishi??

Ni mambo gani ambayo wapiga kura watawawajibisha wawakilishi wao kwayo??

Baada ya uwajibishwaji, ni nini kitafuata?? Kama uwajibishwaji maana yake ni kufukuzwa ubunge, je tunachagua mbunge mwengine AMA la??

Ndani ya jimbo moja, je wananchi watawawajibisha wapiga kura mara ngapi ndani ya kipindi cha miaka 5??
 
Scandalous!
Wabunge wanaitikia wote ndiyooooo, hawa ndiyo wanaowakilisha wananchi
Wananchi wanaitikia wote siyoooooo!

Paskali naye anakuja na hoja za Spika Bora😆😁
Bongo siyo pakuhama
 
Kwa hiyo, kwanza kilipitishwa na Bunge (maana yake wabunge hawakuona umuhimu wa kukiboresha) hadi Rais asikie kilio cha wananchi? Kama ni kweli, then naona hapa wabunge wametukosea sana kama wawakilishi wetu.

Ndiyo maana kilitakiwa kile kipengele cha 'Katiba ya Warioba' kuhusu wapiga kura kuwaajibisha wawakilishi wao (wabunge wa kuchaguliwa) kiwekwe kwenye Katiba yetu ya sasa au kama tukiwa na Katiba Mpya kirejeshwe maana kiliondolewa kwenye ile Katiba iliyopendekezwa kwa wakati ule iliyokuwa ikijulikana kwa jina la "Katiba iliyochakachuliwa".
Wale wabunge hawaki kwa ajili ya wananchi.tusijidanganye kabisa.
 
Kwa hapa,mama amefanya jambo jema sana.
 
Wabunge lazima wawe na aibu kuwa wanategemea kila kitu RAIS awape mungozo wa nini kina faida kwa wananchi katika maamuzi yao! Mnakula mshahara mkubwa bila Kufanya kazi mnayostahili kufanya ; you should be ashamed!! HONGERA Rais kwa marekebisho hayo ya sheria!
Hili bunge bandia, ni vema lingefutwa. Kwenye kipindi hiki cha mpito, mambo yote yasimamiwe na Serikali maana hatuoni umuhimu wa bunge.
 
Anaandaa tatizo alafu analitatua mwenyewe.
Wasio ona mbali wanashangilia.
 
Anaandaa tatizo alafu analitatua mwenyewe.
Wasio ona mbali wanashangilia.
 
Back
Top Bottom