Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,175
- 2,294
Bila kuwaingiza wapinzani Bungeni, TANZANIA HAITOBOI. Hapa watahangaika tuna kucheza danadana na kufanya kazi kwa matukio badala ya kubadili sheria mbovu nyingi tu zilizopo sasa hivi. Sheria hizi zinachelewesha maendeleo hasa katika eneo la biashara. Wafanyabiashara wanaogopa kila kukicha na kufanya eneo/sector kubwa ya kujiajiri kudhorota.
Serikali imefuta Ibara ya 24 iliyokuwa inapendekeza kifungu kipya 47A kwa lengo la kutoa mamlaka kwa polisi kufanya operesheni za kificho kwa madhumuni ya kuzuia utendaji wa makosa.
Akitoa taarifa mbele ya Bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi amesema kwamba katika Muswada huo wa Sheria ya Marekebisho mbalimbali na 7 uliopitishwa hapo jana, kifungu hicho tata kimeondolewa rasmi.
Awali tangu kuzuka kwa taarifa za kupelekwa kwa muswada huo kwa hati ya dharura, kuliibuka kwa maswali na sintofahamu kwenye mitandao ya kijamii ikihoji mantiki ya kuwakingia kifua askari polisi endapo watafanya jinai na kuhalalisha mauaji ya raia.
Maoni ya wananchi hao yanakuja ikiwa siku chache tangu Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuonesha kushangazwa kwake na hatua ya jeshi la Polisi nchini kupitia mkuu wake IGP Simon Sirro kutangazia umma kwamba jeshi hilo limeunda tume kuchujichunguza kwa madai ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini mkoani Mtwara Mussa Hamisi (25).
Hivi karibuni kumekuwa na mlolongo wa matukio ya ukiukwaji wa kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi jambo linalotajwa kuitia doa serikali, licha ya matamko kadhaa ya viongozi wa nchi kutaka jeshi hilo lijitafakari.
Kimsingi KATIBA MPYA ndio jibu. Waamuzi ni wao. Tanzania ipo katika mkanyiko!