Kwa hiyo zisingekuwa kelele za mitandaoni sheria ingepitishwa,wabunge wetu wanamuwakilisha nani?Rais Samia ni mtu makini sana aise, Kazi iendelee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo zisingekuwa kelele za mitandaoni sheria ingepitishwa,wabunge wetu wanamuwakilisha nani?Rais Samia ni mtu makini sana aise, Kazi iendelee
Kwani tozo zina shida gani? Kazi ya tozo hii hapa 👇Wabunge ni mapoyoyo tu!Si ndio wao walipitisha tozo,kikokotoo?Wao wanajua jambo linaloletwa na serikali kazi Yao ni kusema ndiooooooo!
Taarifa ya AG inasema serikali imeamua kufuta kipengele chote Cha 47!
Kwa akili Yako serikali ni Bunge?
Naelewa unachokisema na nakubaliana na hoja yako ila uhalisia utazamwe.Kama ni kweli raisi aliagiza kiondolewe kifungu kwenye mswaada uliopo bungeni (unajadiliwa), hilo ni kosa la kikatiba. Raisi hana mamlaka ya kuagiza mswaada unaojadiliwa kubadilishwa bila kuongea na wahusika na kuwasikiliza maoni yao. Na haya maongezi yangefanywa baada ya kuondolewa mswaada bungeni na baadaye akaurudisha bungeni wakikubaliana. Au angefuata sheria na utaratibu angeungoja huo mswaada upitishwe na akaungoja ofissini kwake ambapo angekataa kutia sahihi, na kuurudisha bungeni na maelekezo kwa nini hakuutia sahihi. Baada kurudishwa bunge lingeweza kuurudisha kwake bila mabadiliko ambapo ingetegemea umepitishwa kwa wabunge kiasi gani. Kama ni theluthi mbili au zaidi ingekuwa ndiyo mwisho wa mchezo, raisi hana uwezo kwa kukataa..yaani analazimika kuutia sahihi. Kama ni chini ya theluthi mbili, angevunja bunge na kuitisha uchaguzi.
Mimi sitetei hicho kipengele kuwepo ila naona kuna athari nyingi kwa raisi kuchukuwa simu na kupiga bungeni kuagiza kipengele fulani kuondolewa. Kwa sasa kuna wale wanaoshangilia kwa sababu ni kweli hicho kipengele kilikuwa na matatizo na ukakasi, hasa pale police anapewa immunity kuondolewa liability akitenda makosa ya jinai. Lakini kuna siku nyingine raisi anaweza pia kunyanyua simu kutaka mabadiliko au kuondolewa kifungu ambacho labda sisi wananchi tunakitaka. Je, akifanya hivyo tutamwambia anaingilia shughuli za bunge? Je kikija kifungu cha kumuajibisha raisi mstaafu kwa makosa ya jinai aliyotenda akiwa kazini au baada ya kustaafu unafikiri atakubali kujitia kitanzi? Akitoa agizo kifungu hicho kiondolewe tutalalamika ameingilia bunge?
Raisi anayo nafasi yake ya kikatiba ya kukataa sheria au vifungu katika sheria. Anatakiwa avitumie hivyo vifungu na siyo kutoa amri mabadiliko yafanyike. Kama hili limeongelewa mitandaoni na akazibuka angetumia taratibu aliyopewa na katiba na siyo kutumia taratibu ambayo anakatazwa na katiba kuinjgilia mihimili mingine. Kwa wale MACHADEMA kuweni waangalifu kushangilia bila kufanya "critical analysis" ya mnachokishangilia. Kama ninyi ni waumini wa kufuata katiba ama hii au ile mnayodai, cha muhimu kwenu ni kuifuata katiba na siyo kuingia kwenye mitego midogo kama hii. Mimi nakubaliana na yule aliesema raisi SSH anatafuta kiki na sifa ndogondogo bila kugundua athari zake za uvunjivu wa katiba aliyoapa kuisimamia na kuitii. Katiba inamtaka asiingilie mihimili mingine (bunge/parliament na mahakama/judiciary).
Serikali imefuta Ibara ya 24 iliyokuwa inapendekeza kifungu kipya 47A kwa lengo la kutoa mamlaka kwa polisi kufanya operesheni za kificho kwa madhumuni ya kuzuia utendaji wa makosa.
Akitoa taarifa mbele ya Bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi amesema kwamba katika Muswada huo wa Sheria ya Marekebisho mbalimbali na 7 uliopitishwa hapo jana, kifungu hicho tata kimeondolewa rasmi.
Awali tangu kuzuka kwa taarifa za kupelekwa kwa muswada huo kwa hati ya dharura, kuliibuka kwa maswali na sintofahamu kwenye mitandao ya kijamii ikihoji mantiki ya kuwakingia kifua askari polisi endapo watafanya jinai na kuhalalisha mauaji ya raia.
Maoni ya wananchi hao yanakuja ikiwa siku chache tangu Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuonesha kushangazwa kwake na hatua ya jeshi la Polisi nchini kupitia mkuu wake IGP Simon Sirro kutangazia umma kwamba jeshi hilo limeunda tume kuchujichunguza kwa madai ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini mkoani Mtwara Mussa Hamisi (25).
Hivi karibuni kumekuwa na mlolongo wa matukio ya ukiukwaji wa kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi jambo linalotajwa kuitia doa serikali, licha ya matamko kadhaa ya viongozi wa nchi kutaka jeshi hilo lijitafakari.
Akili Yako Ina walakini!
Labda wanasema kweli.Mmmmh .. Tunapigwa na kitu kizito.
Kumbe tamaa mbele.......Na hiki bila shaka ni yeye ndio alikiandaa
Unapaswa kujiuliza kilipitaje kwenye baraza la mawaziri.Huyu Mama anakuja vvizuri.
Mbowe tu ndo anamuangusha.
Zako zina leakageAkili Yako Ina walakini!
Tuache Uhuni wa kishamba kwani ni nani alipendekeza kuwepo kwa hicho Kipengele?Serikali imefuta Ibara ya 24 iliyokuwa inapendekeza kifungu kipya 47A kwa lengo la kutoa mamlaka kwa polisi kufanya operesheni za kificho kwa madhumuni ya kuzuia utendaji wa makosa.
Bunge la hovyo sana hili.Kwa hiyo, kwanza kilipitishwa na Bunge (maana yake wabunge hawakuona umuhimu wa kukiboresha) hadi Rais asikie kilio cha wananchi? Kama ni kweli, then naona hapa wabunge wametukosea sana kama wawakilishi wetu.
Ndiyo maana kilitakiwa kile kipengele cha 'Katiba ya Warioba' kuhusu wapiga kura kuwaajibisha wawakilishi wao (wabunge wa kuchaguliwa) kiwekwe kwenye Katiba yetu ya sasa au kama tukiwa na Katiba Mpya kirejeshwe maana kiliondolewa kwenye ile Katiba iliyopendekezwa kwa wakati ule iliyokuwa ikijulikana kwa jina la "Katiba iliyochakachuliwa".
Kwani alikuwa hajui? Huo mswaada haukupita kwenye cabinet?Mama anajua anachokifanya na hulka ya Polisi wetu anaijua.
Safi sana Mama uishi miaka mingi
Ni wanafiki sana hawa watu.Bila ya watu kupiga kelele kwenye mitandao ya kijamii angenyamaza huyo
Hapo bado kumpa bichwa chui jike chifu hangaya kwamba kafanya hiviNi wanafiki sana hawa watu.
Wanamuwakilisha magufuliKwa hiyo zisingekuwa kelele za mitandaoni sheria ingepitishwa,wabunge wetu wanamuwakilisha nani?
Kama ni kweli raisi aliagiza kiondolewe kifungu kwenye mswaada uliopo bungeni (unajadiliwa), hilo ni kosa la kikatiba. Raisi hana mamlaka ya kuagiza mswaada unaojadiliwa kubadilishwa bila kuongea na wahusika na kuwasikiliza maoni yao. Na haya maongezi yangefanywa baada ya kuondolewa mswaada bungeni na baadaye akaurudisha bungeni wakikubaliana. Au angefuata sheria na utaratibu angeungoja huo mswaada upitishwe na akaungoja ofissini kwake ambapo angekataa kutia sahihi, na kuurudisha bungeni na maelekezo kwa nini hakuutia sahihi. Baada kurudishwa bunge lingeweza kuurudisha kwake bila mabadiliko ambapo ingetegemea umepitishwa kwa wabunge kiasi gani. Kama ni theluthi mbili au zaidi ingekuwa ndiyo mwisho wa mchezo, raisi hana uwezo kwa kukataa..yaani analazimika kuutia sahihi. Kama ni chini ya theluthi mbili, angevunja bunge na kuitisha uchaguzi.