Kipi Bora kati ya kununua Tofali na kufyatua mwenyewe

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
Habari Wana ujenzi, nilikua naomba ufafanuzi kati ya kununua Tofali za block kutoka kiwandani na kupeleka site na kununua Material na kupeleka site na kufyatua pale pale site.

Mfano kama nina million 2 hapo nikinunua Tofali kiwandani napata Tofali 2000 mpaka site je nikifyatua mwenyewe naweza kupata Tofali ngapi,?
 
Kufyatua ni best option maana utapata matofali ya ubora unaotaka na kwa uhakika 100%

Mtaji wa hili ni MUDA tu.

Kununua n labda kwa kazi ndogo ndogo,ila kazi kubwa kama kupandisha nyumba,Fensi,nk (Fyatua mkuu).
 
Uko sahihi, kufyatua mwenyewe ni bora sababu unaweza kufyatua tofali imara tofauti na kununua ambao tofali haziwi imara.
 
Muda ninao tena wa kutosha tu wa kuweza kusimamia
Nunua. Ili kufyatua tofali 2500 unahitaji mifuko 100 ya cementi. Kama mfuko wa cementi ni 16-18,000/= *100 = 1,800,000/ lori za mchanga 14 @80000/= maji ya kufyatulia na kunyeshea lita 20,000, fundi wa kufyatua tofali@200/= kwa tofali. Piga hesabu uone wapi parefu. Bado fundi hajakuibia cementi
 
Sasa wale wa kuuza wanapataje faida ikiwa cement mifuko yote hiyo plus gharama zingine?
 
Nunua tu kidogo kidogo, kufyatua ni kazi, kuna kumwagia maji matofali, ukikosea unadhoofisha uimara wa tofali. Ukoa muda wako kwa kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
Basically unafuu upo kwenye kufyatua mwenyewe thats why kuna watu wanafyatua na kuuza na bado wanapata faida kubwa na maendeleo yao tunayona mkuu, Okoa pesa mkuu
 
Sasa wale wa kuuza wanapataje faida ikiwa cement mifuko yote hiyo plus gharama zingine?
Wananunua cementi nyingi kwa bei ya jumla, na wanaletwa hadi site bure.

Wanapata Cementi ya mchongo,

wanafyatua tofali zaidi ya 25 kwa mfuko na kwa kua zinashindiliwa kwa mashine ni ngumu sana.

Akifyatua kwa mkono tofali 30 kwa mfuko zitakuwa za kiwango cha chini sana.
 
Nunua. Ili kufyatua tofali 2500 unahitaji mifuko 100 ya cementi. Kama mfuko wa cementi ni 16-18,000/= *100 = 1,800,000/ lori za mchanga 14 @80000/= maji ya kufyatulia na kunyeshea lita 20,000, fundi wa kufyatua tofali@200/= kwa tofali. Piga hesabu uone wapi parefu. Bado fundi hajakuibia cementi
kaka hii hesabu umeitoa wapi
 
Habari Wana ujenzi, nilikua naomba ufafanuzi kati ya kununua Tofali za block kutoka kiwandani na kupeleka site na kununua Material na kupeleka site na kufyatua pale pale site
Mfano kama nina million 2 hapo nikinunua Tofali kiwandani napata Tofali 2000 mpaka site je nikifyatua mwenyewe naweza kupata Tofali ngapi,?
Hata mimi niko kwa hiyo dilemma nahitaji tofali nyingi sana ..nipo na miezi miwili tu kujenga nyumba ya ghorofa moja . Likizo yangu ni miezi miwili
 
Nunua tofali mkuu..kachague tofali ngumu ununue...tofali moja 950 sio 1000...
 
Nunua. Ili kufyatua tofali 2500 unahitaji mifuko 100 ya cementi. Kama mfuko wa cementi ni 16-18,000/= *100 = 1,800,000/ lori za mchanga 14 @80000/= maji ya kufyatulia na kunyeshea lita 20,000, fundi wa kufyatua tofali@200/= kwa tofali. Piga hesabu uone wapi parefu. Bado fundi hajakuibia cementi
Mfuko mmoja tofali 25???? Hizo ni tofali za kisima au foundation ya ghorofa?
 
Tumia Msingi
Mfuko 1 wa Cement tofali 30
Kuta Mfuko mmoja wa Cement tofali 25.

Hakikisha unatumia mchanga wa kuchimba na sio mchanga wa mtoni.

Mwagilia maji ya kutosha.
Tofali za msingi ziwe hafifu (30/bag) kuliko za kuta (25/bag)?
 
Back
Top Bottom