Kipi Bora kati ya kununua Tofali na kufyatua mwenyewe

Kipi Bora kati ya kununua Tofali na kufyatua mwenyewe

Fanya utafiti then urudi kwenye hesabu mkuu...

Tafuta fundi akupe mchanganuo kama ukifyatua mwenyewe ni gharama kiasi gani utaingia na utapata tofali imara kiasi gani...linganisha na utaponunua...
 
Nunua. Ili kufyatua tofali 2500 unahitaji mifuko 100 ya cementi. Kama mfuko wa cementi ni 16-18,000/= *100 = 1,800,000/ lori za mchanga 14 @80000/= maji ya kufyatulia na kunyeshea lita 20,000, fundi wa kufyatua tofali@200/= kwa tofali. Piga hesabu uone wapi parefu. Bado fundi hajakuibia cementi

Mkuu kw hesabu yako mfuko mmoja unatoa tofali 25 mmhh! Sidhani kama ni sahihi machache sana!
 
Habari Wana ujenzi, nilikua naomba ufafanuzi kati ya kununua Tofali za block kutoka kiwandani na kupeleka site na kununua Material na kupeleka site na kufyatua pale pale site
Mfano kama nina million 2 hapo nikinunua Tofali kiwandani napata Tofali 2000 mpaka site je nikifyatua mwenyewe naweza kupata Tofali ngapi,?
Nunua Tofali mkuu. Huwezi kuokoa gharama wala kupata tofali bora zaidi kwa kufyatua mwenyewe.
Wapiga tofali, kwanza ni professionals wa hiyo kazi. Pili wanapata materials kwa bei ya chini mfano wanatumia magari yao wenyewe kubeba vifaa, wananunu material kama cement kwa jumla nk. Tatu wanatumia kitu inaitwa "economies of scale".

Kujihakikishia, nunua mifuko 5 ya cement na ufyatue kwa majaribio.
 
Wananunua cementi nyingi kwa bei ya jumla, na wanaletwa hadi site bure.

Wanapata Cementi ya mchongo,

wanafyatua tofali zaidi ya 25 kwa mfuko na kwa kua zinashindiliwa kwa mashine ni ngumu sana.

Akifyatua kwa mkono tofali 30 kwa mfuko zitakuwa za kiwango cha chini sana.

Sawa asante nimekuelewa
 
Nakushauli kaonge na wafyatua matofari unataka tofali la ubora upi wakupigie mahesabu apo kiwanda cha tofari kisha wakufyatulie
 
Habari Wana ujenzi, nilikua naomba ufafanuzi kati ya kununua Tofali za block kutoka kiwandani na kupeleka site na kununua Material na kupeleka site na kufyatua pale pale site
Mfano kama nina million 2 hapo nikinunua Tofali kiwandani napata Tofali 2000 mpaka site je nikifyatua mwenyewe naweza kupata Tofali ngapi,?
Kwa milioni mbili, kama utaamua kupiga tofali mwenyewe, lazima uweke humo gharama za mafundi, mchanga, maji na hata mashine na vibao vya tofali unless unapiga kwa kutumia vibao vya kawaida. Hivyo basi ili ujue utapata tofali ngapi, ni lazima uainishe hizo gharama nyingine. Ila binafsi, napenda kupiga mwenyewe kwani unao uwezo wa kusimamia UBORA NA IDADI na pia kudhibiti wizi wa sementi na hata mchanga unaoweza kufanywa na mafundi wetu hawa wenye njaa kali!
 
Asikudanganye mtu, Kanunue tofali. Faida wanayopata hao jamaa ni ndogo sana. Ni faida ambayo hauwezi kusema itakusaidia. Mpaka linaitwa tofali lina hatua nyingi sana ambazo kila moja ina gharama yake.
 
Nunua. Ili kufyatua tofali 2500 unahitaji mifuko 100 ya cementi. Kama mfuko wa cementi ni 16-18,000/= *100 = 1,800,000/ lori za mchanga 14 @80000/= maji ya kufyatulia na kunyeshea lita 20,000, fundi wa kufyatua tofali@200/= kwa tofali. Piga hesabu uone wapi parefu. Bado fundi hajakuibia cementi
Hisabati za wapi hizi boss..? Yani tofali 2500 zitumie mifuko 100? Kwaiyo mfuko mmoja wa cement unatoa tofali 25 tu
 
Nunua. Ili kufyatua tofali 2500 unahitaji mifuko 100 ya cementi. Kama mfuko wa cementi ni 16-18,000/= *100 = 1,800,000/ lori za mchanga 14 @80000/= maji ya kufyatulia na kunyeshea lita 20,000, fundi wa kufyatua tofali@200/= kwa tofali. Piga hesabu uone wapi parefu. Bado fundi hajakuibia cementi
mfuko mmoja ni tofali 25?Hiyo ratio nzuri sana .sema siyo mhimu unaweza fanya hata mfuko kwa tofali 30-35

Hao wanaouza wanafiatua matofali 50-55 kwa mfuko
 
Ukitaka akufyatua mwenyewe hiyo 2M itatoa tofari nyingi zaidi kuliko utaza nunua but je, una muda? Mafundi hawachelewi kukupiga, atakuibia cement halafu mfuko 1 anatoa tofari 50 and hence ubora unakua HAFIFU sana; gawana riziki na wengine, kanunue. Huo ndio ushauri wangu
 
Back
Top Bottom