Kipi Bora kati ya kununua Tofali na kufyatua mwenyewe

Kipi Bora kati ya kununua Tofali na kufyatua mwenyewe

Ukitaka akufyatua mwenyewe hiyo 2M itatoa tofari nyingi zaidi kuliko utaza nunua but je, una muda? Mafundi hawachelewi kukupiga, atakuibia cement halafu mfuko 1 anatoa tofari 50 and hence ubora unakua HAFIFU sana; gawana riziki na wengine, kanunue. Huo ndio ushauri wangu
Hata akiamua kufyatua ATAGAWANA RIZIKI na huyo fundi mfyatuaji na kibarua wake au siyo! Natamani aje fundi mwenye data na facts on this issue! Ni kitu kinafikirisha na kina faida sana kwa future house owners! Kidadavueni kwa makini wana JF.
 
Habari Wana ujenzi, nilikua naomba ufafanuzi kati ya kununua Tofali za block kutoka kiwandani na kupeleka site na kununua Material na kupeleka site na kufyatua pale pale site
Mfano kama nina million 2 hapo nikinunua Tofali kiwandani napata Tofali 2000 mpaka site je nikifyatua mwenyewe naweza kupata Tofali ngapi,?
Bora kufyatua mwenyewe pia gharama ni ndogo kuliko kununua pia ubora

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Nunua. Ili kufyatua tofali 2500 unahitaji mifuko 100 ya cementi. Kama mfuko wa cementi ni 16-18,000/= *100 = 1,800,000/ lori za mchanga 14 @80000/= maji ya kufyatulia na kunyeshea lita 20,000, fundi wa kufyatua tofali@200/= kwa tofali. Piga hesabu uone wapi parefu. Bado fundi hajakuibia cementi
Kama eneo ni zuri kama kule kigambon mwembe mdogo mchanga unatoa hapo hapo site kisha utalipa pesa ya yfyatuaji maana majinbure yapo tele nikifyatua matofali 2400 kwa mifuko 80 ya sement kila mfuko mmoja ni tofali 30 jumla ya gharama nilitumia ni 901500.mifuko 40 ya mwanzo mafundi niliwapa 180000 na mifuko ya 40 ya mwisho nayo hivyohivyo nilsimamia mwenyewe maji nilichota mwenyewe kupanga mataofali nikisaidiana na mafundi.kumwagilia ni mimi mwenyewe

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Basically unafuu upo kwenye kufyatua mwenyewe thats why kuna watu wanafyatua na kuuza na bado wanapata faida kubwa na maendeleo yao tunayona mkuu, Okoa pesa mkuu
Wauzaji wengi wa tofali siku hizi wana mashine za kisasa zenye uwezo mkubwa wa kuchanganya simenti, mchanga na maji. Pia wana umwagiliaji mzuri wa tofali ili kuzikomaza. Je wewe unazo hizo mashine au utakodisha?? Au utatumia kibao?
 
Lengo: tofali 2500
Mahitaji
1. Cement: mifuko 100@18,000/ = 1,800,00
2. Mchanga: lori 14@80,000/ =1,120,000
3. Fundi: 2500*200 kila tofali= 500,000
4.maji 20,000l x1650/liter = 35,000
5. Kumwagilia 5000/day *7days = 35,000
Jumla 3,500,000.
Ukinunua
Gharama
Tofali 2,500x1000 = 2,500,000.
Usafiri: 40,000*12= 480 000
Jimla: 2 980,000
Tofauti ya kununua vs kupiga mwenyewe: 3, 500,000 -2,980,000 =520,000.
 
Nunua. Ili kufyatua tofali 2500 unahitaji mifuko 100 ya cementi. Kama mfuko wa cementi ni 16-18,000/= *100 = 1,800,000/ lori za mchanga 14 @80000/= maji ya kufyatulia na kunyeshea lita 20,000, fundi wa kufyatua tofali@200/= kwa tofali. Piga hesabu uone wapi parefu. Bado fundi hajakuibia cementi
Unakimbia gharama kwa kufata kitu kisicho na ubora?!

Ni bora aumie mara 1 kuliko kujitia unaepuka gharama sasa hivi upandishe nyumba hata kabla hujaamia Nyufa zishaanza tokelezea.

Sishauri mtu anunue tofali kbsa za kujenga nyumba ya Kuishi (otherwise ununue tofali sehemu rasmi (viwandani) ambazo tofali zao zimethibitishwa UBORA wake) Sio hayo matofali huko mitaani mtu kajinunulia tu mashine/vibao tyr anafyatua.. (hamna matofali huko)

Kitu bora lazima ni gharama hamna kitu Bora cha bei rahisi, Hata mtoa hii thread analielewa hilo.
 
Hata akiamua kufyatua ATAGAWANA RIZIKI na huyo fundi mfyatuaji na kibarua wake au siyo! Natamani aje fundi mwenye data na facts on this issue! Ni kitu kinafikirisha na kina faida sana kwa future house owners! Kidadavueni kwa makini wana JF.
Kama unavyo sema economically is weath kufyatua mwenyewe but uwe na muda wa ku supervise, kama muda upo ata save pesa kidogo tu but kama muda hana basi labda mkewe awe karibu kwa uangalizi otherwise i will recomend kununua. Mafundi wengi sio waaminfu im telling you, nimejenga nyumba kadhaa, najua ninacho kisema
 
Wauzaji wengi wa tofali siku hizi wana mashine za kisasa zenye uwezo mkubwa wa kuchanganya simenti, mchanga na maji. Pia wana umwagiliaji mzuri wa tofali ili kuzikomaza. Je wewe unazo hizo mashine au utakodisha?? Au utatumia kibao?
Wana mashine za kisasa lakini ratio yao ya cement ni MBOVU..tena MBOVU MBOVU MBOVU.
 
Unakimbia gharama kwa kufata kitu kisicho na ubora?!

Ni bora aumie mara 1 kuliko kujitia unaepuka gharama sasa hivi upandishe nyumba hata kabla hujaamia Nyufa zishaanza tokelezea.

Sishauri mtu anunue tofali kbsa za kujenga nyumba ya Kuishi (otherwise ununue tofali sehemu rasmi (viwandani) ambazo tofali zao zimethibitishwa UBORA wake) Sio hayo matofali huko mitaani mtu kajinunulia tu mashine/vibao tyr anafyatua.. (hamna matofali huko)

Kitu bora lazima ni gharama hamna kitu Bora cha bei rahisi, Hata mtoa hii thread analielewa hilo.
Tofali za kufyatua peke yako nguvu ya ushindiliaji wake haifikii hata nusu ya nguvu ya mashine ya umeme.

Mfyatuaji wa kutumia mashine ya kushindilia kwa mkono nguvu ya ushindiliaji inapungua with time kutokana na kuchoka, lakini mashine ya umeme nguvu iko constant.

Hata hivyo uchaguzi ni wako: kufyatua mwenyewe au kununua
 
Mkuu kinachohitajika ni hizo tofali zifikie minimum compression strength basi haijalishi zimefyetuliwa kwa machine au manually (binadamu), Pia inatakiwa ikumbukwe kuwa strength ya hizo tofali inaambatana na factors kama ratio, curing n.k .
 
Kwa kua hujajenga Ungepita kimya kimya tu
Tufanye umeshinda boss. Ila kwenye ujenzi wewe bado folena sana. Ila siku ukipata uwezo kujenga au kua na karakana ya utengenezaji wa tofali. Nitafute nikupe ushauri na mbinu bora katka sekta hii
 
Nunua. Wauzaji wata hesabu nzima ndizo mtakabidhiana site.
Hizi za kufyatua uta pigwa siment na wahuni. Vijana hufukia kwenye mchanga mifuko ya siment. Ukiacha 15. Masaa 2 tu una ambiwa zimeisha. Huwa wana tabia ya kuja na makasha matupu mapya. Au ukiwapa mgongo tu mifuko ina ondoka. Mgandamizo wa tofauli za kufyatua ww ni mdogo hivyo siyo imara. Ratio yake itakua ina vary tofali kwa tofali na wahuni wa ku kupiga siment 5 watafidia kwa kuweka mchanga mwingi. Bili za maji kumwagilia. Usumbufu wa kusimamia. Ku okoa muda. Nunua tu.
 
Mkuu kinachohitajika ni hizo tofali zifikie minimum compression strength basi haijalishi zimefyetuliwa kwa machine au manually (binadamu), Pia inatakiwa ikumbukwe kuwa strength ya hizo tofali inaambatana na factors kama ratio, curing n.k .
Kwa hiyo kushindilia kwa mkono kunaweza kufikia compression strength inayotakiwa consistently kwa tofali la kujengea nyumba?

Au tofali la kupiga kwa mkono na la kupiga kwa mashine ya umeme have the same compression strength?
 
Tofali za kufyatua peke yako nguvu ya ushindiliaji wake haifikii hata nusu ya nguvu ya mashine ya umeme.

Mfyatuaji wa kutumia mashine ya kushindilia kwa mkono nguvu ya ushindiliaji inapungua with time kutokana na kuchoka, lakini mashine ya umeme nguvu iko constant.

Hata hivyo uchaguzi ni wako: kufyatua mwenyewe au kununua
Tukisema mtu ufyatue tofali zako haina maana tofali za kufyatua lazima utumie mashine za analog mkuu.

Maisha mepesi sana mkuu,mbona unataka kujitesa?! Hivi hujui wapo watu wana mashine wamezinunua kwa ajili ya kukodisha tu na ni za umeme?!

Unafikiri kila mwenye site ya kuuza matofali zile mashine ni zao? Dunia ya sasa kila kitu kinawezekana ni wewe na pesa yako TU.

Yawezekana site ambapo mtu anajenga umeme haujafika,Pia kuna option B ya kwenda.kufyatulia tofali zako pale pale site wanapouza matofali Unafyatua tofali zako kwa ratio yako na mashine zao pale pale site kwao.

Ni pesa TU ukitaka kila kitu ufanye mwenyewe ununue mashine yako,kila kitu chako ndo ufyatue Utachelewa sana.

As i said before kitu kizuri lazima ukubali GHARAMA ukishalijua hilo mengine hayakusumbui. Formula ni ile ile ni mwendo wa ku apply tu una solve tatizo. kwisha.
 
Back
Top Bottom