Kipi Bora kati ya kununua Tofali na kufyatua mwenyewe

Mkuu hesabu hii haiwahusu wauzaji, au wanafidia gharama kwenye ubora wa tofali zao?
 
Hata mimi niko kwa hiyo dilemma nahitaji tofali nyingi sana ..nipo na miezi miwili tu kujenga nyumba ya ghorofa moja . Likizo yangu ni miezi miwili
Mbona muda wakutosha kabisa huo....kama 200 million ipo kwa shati nipe tenda hiyo kisimamisha mjengo
 
Aisee nunua ,utakuja kunishukuru.
 
Ndugu yangu. Kwa uwelewa wangu vyote ni bora ila kila sehemu ina unafuu wake na ugumu.
2m. Kwa mkoa wa tabora unapata tofali 2000 za 5nchi, 6inch ni tofal 1800. Hvi. Lakini ukifyatua utapat faida ya tofali 200 hv.
nije kwenye mchangunuo. Saruji mfuko 23000. Mfuko kwa foundation wall ni 25-30 ratio.
mfyatuaji ni 200 kwa tofali.
. Mashne kukodi 10,000, tofali 2000 ni siku 4-6.
. Mchanga 4mcub=180-215blocks ya inch 5, unahita gari 9-10. TRIP 40,000-50'
. Maji ya kufyatulia na kumwagilia ni lita 20000-23000. Kila pipa 4000@7000. Pipa moja ni sawa na lita180- 200.
. Kama huna kisima au bomba kila ndoo 200. Ndoo ni sawa na lita 20.
. Kila mfuko kuleta site ni 300-500 zidisha.
. Muda wa kusimamia upigaji, umwagiliaji wa siku 7-12. Staking gharama nayo.
. Na kila ifikapo kuanzia muda wa saa 5 asubuh, huwezi pata tofali bora.

. Kununua changamoto hapo juu hakuna, ila huna chaguo la mchanga, ila ukitaka kununua tofali nunua iliyo kwenye vibrate mashne, huwa ina ratio ya 40 hadi 50, ila huwa na mchanganyo sawa, maji mengi na mkandamizo mkubwa, hiyo hazipasuki kupeleka site.
. Ni umasikini tu, kwangu kununua tofali ni nafuu zaidi kwa ajili ya quality na kufyatua ni nzuri kwa quantity.
 
Kama uneweza kukodi mashine ya umeme ukafyatua mwenyewe sawa.. ila kama huna pochi nene.. nenda kanunue tu mkuu..

Usi complicate sana life..
 
Mkoa gan huu mnaoibiwa hivi
 
Mifuko 100 tofali 2500 manake mfuko mmoja tofali 25, hiyo ni ratio yako tu mkuu. Tanzania hii huwezi pata tofali za kiwango hicho na wauzaji wasingekuuzia tofali kwa shilingi 900 mpaka 1200. Minimum kwa tofali za mtaani ni tofali 45 kwa mfuko. Fuso hizi size ya kati moja inafyatua mifuko 7, kama ana muda na upatikanaji wa mchanga ni rahisi afyatue. Kwa vyovyote vile atakuwa na faida na si hasara, kwa mifuko Mia moja lazima atafunga kazi na tofali 4700 au zaidi. Make kuna wakati watazidisha kidogo mchanga hivo utakuta kila mfuko unapata tofali 2 au 3 ziada. Cha msingi maji asubuhi na jioni kwa siku 7
 
Uko sahihi, binafsi huwa nafyatulisha mwenyewe.
Kufyatua kuna FAIDA ndugu.
Mfano,Mwanza.
Saruji, mfuko 1@sh. 21,000/, then mifuko yako 100= sh.2,100,000/ vibarua kwa kila mfuko wa saruji ni sh.5000/
Nafuu ni kuwa utachagua watumie mashine (manual) au watumie mkono tu.
Idadi ya tofali,ratio nzuri na imara ni 45 kwa mfuko.
Aina ya mchanga, tumia wa mvua, yaani mwekundu.ukikauka ni jiwe......
Utajikuta unaokoa saaana.
 
Mkuu nina site mwembe mdogo nataka nianze ujenzi mwakani Mungu akipenda. Unaweza nipa mwongozo zaidi? Au pia kuni link na hao mafundi waliofyatua tofali
 
Nunua tofali
 
Mkuu upo right
Binafsi niwahi fyatua tofali za kujengea ghorofa , viwanda na nyumba za matajiri
Mswahili wa kuunga unga hawezi nunua zile tofali.
Tofali ina moramu. ndogo ndogo, ina mchanga na mfuko mmoja ni tofali 20-21, halafu zinalala kwenye karo la maji na kukaushwa siku kadhaa kabla ya kwenda sight. Inabidi uwe mwanaume wa shoka kununua zile tofali zina bei si kitoto.
At least watu wazitumie kwenye msingi tu huko juu waweke za mtaani.
 
Kama maji ulipo yanapatikana kirahisi fyatua mwenyewe...mimi nilifyatua mwenyewe tofali elfu 3,,mfuko mmoja walikuwa wanatoa tofali 30 na garama ya tofali moja ni sh 200
 
Nijuavyo Mimi kufyatua ni nafuu na vizuri zaidi Ila inahitajika usimamizi wa karibu na pia ni inapoteza muda. Ila Kama huna haraka na una muda wa kusimamia ni vzr kufyatua
 
fyatua ni mzur mfuko mmoj unatoa tofal 35. ufund 5000. unamwagia tu siku 3 unajikijta laki 6 una tofal 1000
 
Daah 😁😁😁 hii ratio ya mfuko mmoja wa cement kwa tofali 25 ni kwa public constructions hasahasa majengo ya serikali ukitumia hii kwenye nyumba zetu za vyumba vitatu ni kujiongezea gharama tu
 
Kufyatua ni best option maana utapata matofali ya ubora unaotaka na kwa uhakika 100%

Mtaji wa hili ni MUDA tu.

Kununua n labda kwa kazi ndogo ndogo,ila kazi kubwa kama kupandisha nyumba,Fensi,nk (Fyatua mkuu).
Jamaa hajasema matofali ya kununua hayana ubora.
Stay on line.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…