Ushauri wangu wa kwanza, ACHANA KABISA NA HUU MPANGO WA KUFUNGA AC KWA SASA. Kwanini? Inavyoonekana uchumi wako haukuruhusu na pia msukumo wako ni tamaa tu (hamu? Ushamba?) lakini hicho kitu sio uhitaji wako wa lazima kwa hali yako ya maisha ya sasa.
Kabla ya kufunga AC inapaswa utambue kuhusu hizi gharama:
1. Kununua AC yenyewe.
2. Kuboresha mazingira (nyumba au chumba) kwa ajili ya hiyo AC kuja kufungwa.
3. Kuifunga hiyo AC (Installation)
4. Umeme wa kuiendesha hiyo AC
5. Service ya AC (Maintenance&Repair).
PIli, vitu kama hivi sio vya kukimbilia kuvinunua kwa mkopo, tena wakopeshaji wenyewe ni dealers wa bidhaa, na bahati mbaya kuliko zote, brand ya hiyo bidhaa huijui na bidhaa yenyewe huna uzoefu nayo. Huo tunauita ni ujinga, na huo ujinga wako ndio faida kubwa ya hao wauzaji.
Mwisho kabisa, kama wewe ni sikio la kufa (yaani kufa na kupona umedhamiria ni lazima ufunge AC kwa sasa) basi huu ushauri hapa chini;
Wewe nenda kwa mafundi wa Air condition, Dar wapo wengi sana kuanzia hapo Magomeni, Kariakoo, Buguruni, Kinondoni, Mwenge nk.
Pita kwenye ofisi zao, tupia macho huku na huku, jaribu kuuliza mambo mawili matatu kuhusu Bei, ubora, wauzaji, matengenezo, spare na mengineyo kuhusu Air condition. Kuna kitu kikubwa utagundua.