Kipi bora kununua air condition au kuchukua ya mkopo kutoka kampuni ya baridi baridi ?

ndio mkuu ndio maana natafanya hesabu za air condition hapa
Bado huna uchumi wa kumiliki air conditioner mkuu. Kwanini unataka ujitutumue kwa mikopo ya kipumbavu na ya kipuuzi kama mwanamke mjinga?

Ingekuwa ni mashine ya kufanyia biashara kuingiza kipato ningekwambia chukua ya mkopo kama huna cash ya kununua. Sasa unataka ukope sijui ili ufurahishe mademu zako.
 
Kama unafikiria kuwa na AC ya mkopo ni kama unalazimisha kuwa na kitu usichokuwa na uwezo nacho.
Yaani mtu ukope AC ya kufunga ndani chumbani? Khaaa .
Nilikuwa naona watu wanaokopa simu kama wajinga ila wewe ni mjinga zaidi
Kulipo kukopa AC ndugu ni kheri ukakope kiwanja .
Watu wengine sijui mnaakili za wapi naomba nikupe pole kwa akili hizo za kijinga
 
Kitu Cha milioni unakinunua 2M?
 
Jaribu Hisense,naona kama hii brand wanafanya vizuri kwenye electronics devices....
 
1. Kukopa AC ni gharama zaidi kuliko kununua.
2. Gharama ya kununua si kubwa kama kuihudumia. BTU 9000 inverter itakula karibu unit 5 kwa siku (kama utatumia usiku tu). Na kama utaitumia kila siku, hii ni sawa na zaidi ya Tsh. 50,000 ya umeme nje ya matumizi yako ya sasa.
3. Kila baada ya miezi miwili au mitatu kuna service (kuisafisha). Fundi analipwa Tsh. 20,000. Labda ujifunze uwe unaisafisha mwenyewe. Nadhani si kazi sana.
4. Joto la 2023 lilinifanya nichukue kwa ajili ya bedroom. Nilijuliza sana kuchukua Baridi² au yangu, nikaamua kununua. Hadi sasa inachapa kazi bila shida. TCL BTU 9000 Inverter. Warranty miaka 2.
 
Kwa biashara go for barid baridi , kwa matumizi binafsi jichange tu
 
Chukua Ac ya Hisense - Je utaweza kununua Umeme vizuri? Mimi natumia Hisense Mpya kabisa Toka Mwaka 2022 Mbaka Leo Linadunda kinyama - Tatizo Umeme, usije kununua likaja kugeuka pambo la nyumbani

Namsikitikia kwa kweli . Swali lako ni zuri taweza kununua umeme?
Kuna jamaa alijichanganya akakopa gari kupitia mhahara wake makato yalivyoanza kuja kipindi kinafika anakosa fedha za kununulia mafuta anapaki gari
 
1Deposit180,000.00
280,000.00X24.001,920,000.00
2,100,000.00

Utakuwa umelipa hela ya kununua Ac mbili hapo mwisho wa mwaka wa pili bora ujichange tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…