Kipi bora kununua Hiace mpya kwa 30M ama kuchukua Tata Marcopolo kwa mkopo

Kipi bora kununua Hiace mpya kwa 30M ama kuchukua Tata Marcopolo kwa mkopo

Huu pia ushauri mzuri niliwahi jiuliza kwanini hakuna mabasi ya mchana kwa route za mbali mfano Mbeya huwa kuna abiria wengi sana nyakati za mchana.
Mbeya wana akili sana! Nimesafiri kwenda Makambako SAA moja usiku kutoka Dar na Coaster inakwenda Mbeya na imejaza! The same, unaanzisha route ya mchana kutoka Dar kwenda Mwanza au Mbeya au Kahama au Arusha! Kama gari ni yako, ukichoka au ukikosà abiria unalala!
 
Kwa ushauri wangu namshauri atafute data zaidi kabla ya kufanya maamuzi.
Maana sio kila unachosikia kipo kama unavyosikia. Hizo namba za hela zote ni nadharia ukiifanya hiyo biashara INAWEZA KABISA isiwe kama unavyo plan.
Biashara yoyote ile ni kujikana na kuwa mvumilivu, kuna wakati inakwenda kama ulivyo plan na kuna wakati haiende vizuri kabisa.
Je kwenye hiyo Biashara unayotaka kuifanya ndipo unapo tegemea kupata mahitaji yako ya kila siku?
Hajawai kuifanya kabisa. Ndomana amesema anatarajia 200k kwa siku
 
Bro nikweli kabisa unayo yasema ila biashara yoyote ni kukaza moyo na kujikana kwa muda then matunda utakuja kuyaona baadae.
Umewaza vizuri ila tafuta Data za kutosha.
Ingekuwa mimi ningechagua Hiace kwakuwa hakuna atake kuwa ananidai wala sintakuwa na marejesho yoyote. Ila ujue hapo unapambana kiume hakuna kutumia sana mapaka unaanza kukopa kwa kuwa una Haice.
Sijawahi ifanya mkuu. Ndo my first time. Am sure hakuna aliyezaliwa anajua wote tunajifunza
 
Bro nikweli kabisa unayo yasema ila biashara yoyote ni kukaza moyo na kujikana kwa muda then matunda utakuja kuyaona baadae.
Umewaza vizuri ila tafuta Data za kutosha.
Ingekuwa mimi ningechagua Hiace kwakuwa hakuna atake kuwa ananidai wala sintakuwa na marejesho yoyote. Ila ujue hapo unapambana kiume hakuna kutumia sana mapaka unaanza kukopa kwa kuwa una Haice.
Sure kaka.
 
keisangora,

Mkuu kwanza nikupongeze kwa hatua uliyofikia ni jambo jema sana kwani watanzania wengi tunafanya biashara za kwenye makaratasi na kuona faida kubwa sana wakati hali halisi haiko hivyo.Naomba nitoe kaushauri kangu kadogo:-
Hiyo hera unaweza tafuta eneo ambalo ni zuri na limechangamka ufungue duka la jumla la vinywaji,pombe kali na vyakula,ajili vijana wa2 wa kukusaidia kazi ya kusambaza bidhaa kwenye maduka ya kawaida.Pambana kutafuta bidhaa kwa bei ya chini ili uweze kuuza kwa ushindani nakuhakikishia kwa siku huwezi kosa 100K-200K.
Biashara ya magari ni nzuri ila haipaswi kuwa tegemeo la kufanya maisha yaende,ukiamua kufanya biashara ya magari hakikisha una shughuri nyingine ya kufanya maana kuharibika kwake ama kupata hajali hakunaga taarifa,nimeifanya kwa mda wa mwaka sasa ila naona changamoto ni kubwa ingawa hera inapatikana.All the best mkuu
 
Vyakula aina gani mkuu.pia asante sana kwa ushauri wako kaka/ dada

Vyakula kama Unga wa ngano kg 25,Sembe kg 25,kg 10 & kg 5, Biscuits,Pipi, sabuni kama jamaa,kleensoft kiroba na ndoo,sukari kg 50 & kg 25,mafuta ya ndoo, dawa za mbu Kama Rungu & Hit.Kumbuka hapo utauza kwa katoni/1/2 katoni.
 
@uniq,Kama ana 40M kwa nini asichukue Coaster ikawa inapiga route za kupeleke misiba mikoani,gari haichoki haraka inabaki na upya wake kwa muda mrefu
 
Hapo nakubaliana na wewe kama anaweza pata Coaster kwa bei hiyo mimi kubali kwa asilimia 100
Kama ana 40M kwa nini asichukue Coaster ikawa inapiga route za kupeleke misiba mikoani,gari haichoki haraka inabaki na upya wake kwa muda mrefu
 
Hapana, anatakiwa kuwa na meneja mwaminifu yeye akomae na mengine
Na akitaka meneja wa kusimamia biashara ya gari ni kheri akamfanya mke wake,hapo kidogo biashara inaweza kufanyika
 
Mkuu hii hela fungua hardwire
Wewe ndio una akili na maono ya mbali.
Biashara ya usafiri si ya kufanya kwa mkopo yaani ni pasua kichwa Sana.
Si rahisi upate pesa ya kukuwezesha kupeleka marejesho ya mkopo halaf nyingine ubakiwe nayo akiba.
Kama hao walionunua kwa cash tu wanayumba yaani nimeshuhudia wengi tu walioanza hii biashara ya magari inawapasua kichwa Hadi wengine wanasusa na kuzipaki Costa zao uwani na wengine wanaziuza kwa Bei ya kutupa kwa ajili ya hasira.
Kwa hyo kwa upande wangu Mimi hainiingii akilini ukope gari ya milioni 100 halafu uniambie utailipa kwa kutegemea hyo gari na kumbuka barabarani Kuna Mambo mengi Kama ajali na vinginevyo.
 
Back
Top Bottom