Kipi bora kununua Hiace mpya kwa 30M ama kuchukua Tata Marcopolo kwa mkopo

Kipi bora kununua Hiace mpya kwa 30M ama kuchukua Tata Marcopolo kwa mkopo

Chukua hiace Ndugu yangu tata wakukamatia gari yako bure kisha wanapiga mnada marejesho ya mkopo n 3.5m kwa mwezi alafu hiyo hesabu ya 200k kwa cku itakushinda utabadili madereva mpaka uchoke ruti inayoweza angalau kidogo no chanika-gerezani ila Bari itachakaa ndan ya mwaka tu
 
Huwezi kupata Coaster kwa 40m tusidanganyane, ukiagiza ikiwa chini sana ni 60m labda kama ni Coaster zile tunaziita Box lakini Hizi mayai ambazo nyingi ni automatic huwezi kupata kwa 40m. Nimemnunulia MTU just last week used namba DER kwa 36m.
Hiyo ni kila kitu usajili na TRA ile gharama zao umeshalipa mana kuna muda ushuru Wa serikali unazidi gharama ya Gari japan
 
Hardware inaweza ikanipa 100-150k kwa siku kweli mkuu.
Hardware cement mfuko faida ni 500-1000.
Ninaangalia biashara nitakayotengeneza 150-200 padei. Nimefanya Savei ya biashara nyingi sana na changamoto zake zote.
Asante kwa wazo lako pia
Mkuu hiyo 150-200 sio faida halisi. Kuna uzi nautafuta humu (sikumbuki kama niliusoma humu ama kwingine) jamaa alishusha nondo juu ya biashara hii ya usafirishaji mpka nikafurahi. Hapo utatoa matumizi (mafuta, posho n.k) kuna hela ya services ndogondogo n.k Mambo ni mengi sana hapo bado hujatoa rejesho kwa wahindi. Bado fedha ya uchakavu. Unaweza kujikuta faida kwa siku ni 30-40, hapa haijalishi unalaza hela kiasi gani ikifika kwenye matumizi unaweza kutoa hela yote uliyohifadhi.
 
Muongozo naokupa...

Kheri tafuta Hiace au Coaster kabisa...

Tata, Eitcher , Isuzu za mkopo ni kichefuchefu... Hesabu ya 200,000 kwa siku unaiona nyingi, ila ujue gari hailali, inakesha, saa Tisa asubuhi mpaka 7usiku kila siku, kufukisha hiyo Million 120 ya mkopo ni kichefuchefu...

Cc: mahondaw
 
Lakin mkuu kuna jamaa kakushauri hardware wewe unasema unataka faida kubwa kwa siju, iwe 100k mpaka 150k.
Unaweza ingiza hyo na pesa usiione kutokana na pressure yake. Fanya biashara kwa kiasi cha pesa yako au hatakama unakopa mm sikushauri magari mkuu. Bora hata hyo h/w hatakama utaingiza 50k lakini niyakwako mkuu.
Ushauri mzuri afungue hardware ya 30m aende benk akope 20m .
Biashara zote zinalipa afanye itakayo mpendeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninaomba nikucheki pm ndugu kama inawezekana
Mkuu, fanya hardware Kama alivokuelekeza jamaa.

Hizo stories za faida jero achana nazo.

Simenti Ina faida ya 1000, ila haikai.

Na Kama uko eneo zuri, kwa siku kuuza mifuko 20- 50 ni kawaida Sana.

Ninaongea kwa uzoefu, Nina Hardware tangu 2015

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro mimi sina elimu kuhusu magari huo ndo ukweli..ila nimekua angalau nashuhudia Eicher nyingi hudumu kuliko Tata hasa ishu za mashine(injini) pia kibiashara hupendwa zaidi kuliko TATA hasa kwa abiria wenyewe(Muonekano) na hata wamiliki wenzako pia hata ikija ukitaka kuiuza ni rahisi kuliko TATA.

Nimeshea na kushauri asilimia japo 1 ninayoifahamu
Kwa ujumla TATA ni bora kuliko EICHER, body ya TATA ni imara sana pia huhimili njia za bongo kuliko EICHER ambazo huchakaa haraka sana
 
Kuna jamaa yangu ni anazungusha TATA route kkoo-kisewe mbgala wao wanapeleka 150k,ila kuhudumia TATA bora uchukue eicher spare zake ziko affordable kuliko huyo muhindi TATA.Tafuta coaster ipige route za shamba huko pwani to Dar
TATA ukipiga shamba hukosi kulaza 300,000/= kwa siku tena huwa gari linapumzika kuliko mikimbizano ya daladala jijini DAR. Ukiweza nenda Morogoro upate route ya Moro - Kisaki ama Moro - Mahenge. Pia route ya DAR to Kisaki ina abiria wa kutosha
 
Mpaka sasa mtoa mada yuko kwenye dillema, ujasiliamali ni jambo gumu linalohitaji maamuzi magumu lakini makini na yaliyochambuliwa
 
Sijaona mtu anazungumzia Fuso injini nyuma au Nissan Civillian. Yeyote mwenye uzoefu atujulishe na sisi kwa kulinganisha na coastwr/ eicher
 
Kiuchumi unatakiwa uwekeze asilinia 30 ya ulichonacho, ukiona inaenda enda u naongeza tena 30% then remaining balance 40%.
Sasa wewe unataka uchukue zote uweke kwenye biashara mpya mbaya zaidi na kukopa juu.
Ndugu yangu sikuombei mabaya lakini siku mambo yakibuma usipokuwa kichaa itakuchukua muda sana kuibuka.

Ukiwa na million 6 ukawekeza una uwezo wa kupata 80,000 kwa siku, ukiwekeza mara mbili yake ni 160,000.
Sasa ilichukua hiyo nusu ya pesa yako u nalaza mpaka kilo 3 kwa siku.
Aiseeee ngoja nikomae na ninachokifanya.
Mleta mada achana na hiyo kukopa kuna biashara kibao zina mauzo na faida za kutosha kwa siku unazoweza kutumia hiyo 30m na ukala mema ya nchi.
Kw

Dangote anautajiri wa around 12 bil za kimarekan, ana project ya kisima cha mafuta cha dolla bil 10...kwa zaid ya 80% n pesa yake inatumika

Haya mambo hayanaga formula mkuu, unaweza ukakopa ukapoteza zote. Unaweza usikupoke ukatumia zako bado ukapoteza zote , na kinyume chake

Hujaelewa point yangu naomba soma kwa utulivu utaelewa.
Huwezi kuanza uwekezaji wenye high risk kama hiyo Tata kwa hela zote na mkopo juu uwe unapeleka rejesho kwa mwezi, at least angeweka pesa zake zote mkopo usingekuwepo.
Come to Dangote yule haja anza yeye ni karithi kwa babu yake, baba yake na biashara yake imeshakomaa anakopesheka.
Mleta mada ni maskini kaka mimi tu na hizo pesa kazi pata kwa mkupuo.
Kasikia tu biashara inalipa na wahindi wa wanakopesha anataka aifanye.
Akifanya afanye ni hela zake lakini hakuna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom