Kipi cha kuanza pindi unapopata ajira: Kuoa, nyumba, biashara au gari?

Kipi cha kuanza pindi unapopata ajira: Kuoa, nyumba, biashara au gari?

Huwa inategemeana na Aina ya Ajira, kuna Ajira zingine Hadi upate chombo cha Moto miaka 2,

Uje utafute kiwanja mwaka 1, hapo uvute pumzi ya kusimamisha ukuta na mengineyo, kama kibunda ni cha kutosha Jenga Kwanza, kinachofata biashara tafuta pisi uoe

Kama unaona mambo yatakuwa mengi "usiwinde mnyama ambae unajua huwezi kumuua"
 
Kila mtu ana vipaumbele vyake katika Maisha.

Kuna wengine suala la Kuoa sio kipaumbele chao, wengine suala la kujenga sio kipaumbele chao n.k

Binafsi kipaumbele changu cha kwanza ilikuwa familia. Nilipoona nina uhakika wa kumtunza Mke, nilivuta Jiko faster.

Nilipoona wife anapata shida ya daladala na Bajaji wakati wa kuhudhuria Kliniki kipindi cha Ujauzito, nikanunua Usafiri.

Baada ya kuona watoto wameanza kuongezeka na kulazimika kupanga nyumba kubwa, nikalazimika kununua uwanja na kujenga.

Maisha ni yako brother, jitahidi kuwa na machaguo sahihi kwaajili ya kesho yako na Watoto wako
 
Kuoa na kupata familia ni muhimu na umri unakwenda. Gari muhimu linarahisisha usafiri na maisha pia linakupa hadhi fulani.

Nyumba inakupa makazi ila huwa haiishi. Biashara inakupa fedha ya ziada nje ya mshahara hivyo ni rahisi kupata nyumba na gari baada ya biashara.

Ni kipi cha kukipa kipaumbele ukiwa muajiriwa?​
Kutoa sadaka, unamrudishia MUNGU wako (nasema MUNGU wako, utajua ni yupi) shukrani ya kupata ajira, Sawa na wale waabudu wazimu, huwa LAZIMA warudishe sadaka
 
k na kupata familia ni muhimu na umri unakwenda. Gari muhimu linarahisisha usafiri na maisha pia linakupa hadhi fulani.

Nyumba inakupa makazi ila huwa haiishi. Biashara inakupa fedha ya ziada nje ya mshahara hivyo ni rahisi kupata nyumba na gari baada ya biashara.

Ni kipi cha kukipa kipaumbele ukiwa muajiriwa?​
Unaweza kufanya yote inategemea kipato chako tu, kama unaanza na ka mshahara chini ya 2M! Inaweza ikakuchukua miaka kumi kujenga!
Mi ajira ya kwanza nilianza na 300k, ilikuwa 2009,nikapiga chini baada ya mwaka, nikaingia mgodini Congo, salary 17M kwa mwezi, nilioa baada ya six month,
 
Jenga kwanza jihakikishie makazi yako ya kudumu.
makazi ya kudumu we ni mti.... angalau ungesema atafute rasilimali isiyohamishika ambayo itakuwa na continues flow of income.... ndio mengine ya kujenga ya kuishi au kuoa yatakapotokea...ukioa na kzi ikiharibika...ukajenga na kazi ikaharibika....tuwe na positive mindset...kuna bro wangu alifanya vyote tofauti na ushauri wangu mke kamweka home kajenga kazaa..covid hii hapa... mradi ukasitishwa....utamhurumia kashaoomba msaada mpaka sasa anaona aibu haombi tena...kazi haipatikani umri ushaenda...hajui biashara na alimpiga bit mkewe kufanya biashara...ni huruma kwa kweli..
 
Kuoa na kupata familia ni muhimu na umri unakwenda. Gari muhimu linarahisisha usafiri na maisha pia linakupa hadhi fulani.

Nyumba inakupa makazi ila huwa haiishi. Biashara inakupa fedha ya ziada nje ya mshahara hivyo ni rahisi kupata nyumba na gari baada ya biashara.

Ni kipi cha kukipa kipaumbele ukiwa muajiriwa?​
Boda boda inarahisisha Maisha kwenye Kuwai😂😂
 
Unaweza kufanya yote inategemea kipato chako tu, kama unaanza na ka mshahara chini ya 2M! Inaweza ikakuchukua miaka kumi kujenga!
Mi ajira ya kwanza nilianza na 300k, ilikuwa 2009,nikapiga chini baada ya mwaka, nikaingia mgodini Congo, salary 17M kwa mwezi, nilioa baada ya six month,
🙏
 
Na sisi kataa ndoa tunaanzaje ?

"Clarify your value "

Kila kitu huwa kina umuhimu Ila kinachotakiwa ni kuwa na vipaumbele katika kukimiliki hicho kitu

So it is matter of time and space that matter most .

Mfano ikiwa wewe ni kataa ndoa basi kuoa sio kipaumbele chako

Hivyo hela ya kuoa waweza kuiwekeza sehemu nyingine Kama katika biashara au ujenzi n.k
 
Mm bwana kujenga ndo lilikua swala langu no moja.Hizi dharau kanakuja katofo ka baba mwenye nyumba kanauliza hivi mjinga gani leo zamu yake kusafisha choo 🤣🤣🤣🤣dah...hapana bora nikae kwangu watoto wangu hata wakila dagaa wako kwao hata nikifa wanapakushika.
Kesho tunaambiwa bahiri😂😂
 
Back
Top Bottom