Kipi kigumu kwenye kufuta mchezo kwa maamuzi mabovu ya Refa? Madhara yake ni yapi kiasi cha mtu mmoja kuwa na maamuzi ya mwisho yasiyoweza kubadilika?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hili ndio swali ninalijiuliza huku nikizingatia uwekezaji wa gharama kubwa unaofanywa na vilabu plus wachezaji kuvuja jasho halafu kunakuwa na sheria/kanuni inayompa mtu mmoja anaeitwa mwamuzi kuwa na maamuzi ya mwisho na kibaya zaidi hayabadiliki hata ikithibika alitoa maamuzi yasiyo sahihi.

Na ni kwanini dunia nzima inatumia nguvu kubwa kujadili maamuzi mabovu ya marefa na watu hawajadili kabisa sheria ibadilishwe mchezo ufutwe/urudiwe?

Kama kwenye kupanga matokeo ikithibitika matokeo yalipangwa, matokeo yanafutwa na timu ilionewa inapewa ushindi huku timu iliohusika kupanga matokeo ikiadhibiwa. Ni kwanini refa anapofanya maamuzi mabovu na ikathibitika hivyo, matokeo yasifutwe?

Yaani FIFA inajali zaidi incovinience za kubadili maamuzi ya refa kuliko jasho wanalotoka wachezaji na uwekezaji unaofanywa na vilabu kutafuta ushindi?

FIFA wanataka mpaka nini kitokee ndio waone kuna umuhimu wa maamuzi ya refa kutenguliwa?

Mimi sielewi, na zaidi siwaelewi walimwengu wapenda soka kwanini nao wao wamekuwa kama nyumbu kusisitiza tu kuwa maamuzi ya refa ni ya mwisho na hawaongelei kabisa umuhimu wa maamuzi ya refa kubadilishwa?

Yaani wanamichezo wanatumia muda mwingi kuhioji na kulalamikia tatiozo ila hawahangaiki kabisa kuhoji chanzo cha tatizo ambalo ni mtu mmoja kupewa maamuzi ya mwisho!! Pathetic!!

Hata mahakamani kwenye kufanya maamuzi mazito, majaji hupiga kura, ila kwenye soka eti mtu mmoja tu ndio anaamua kila kitu na maamuzi yake ndio ya mwisho!!!

Wanasema mchezo wa soka ni wa kikatili, ila ukweli ni kuwa, kanuniu na sheria za huu mchezo ni za kikatili zaidi kulikoi nature ya mchezo wenyewe.
 
Kwa kusema kweli wana yanga wote tumeumia sana lakini hatuna budi kuganga yajayo, kikubwa tumejifunza baadhi ya vitu. Kwanza hatuna streika katili pale mbele(one chance one goal), pili game za mtoano tunatakiwa kuzimaliza uwanja wa nyumbani.
 
Kwanza, Kwenye mechi, sio refa peke yake anaamua, kuna wasaidizi washika vibendera wa pembeni na nyakati hizi kuna hadi VAR.

Pili, kinachoitwa maamuzi mabovu ya refa wakati mwingine ni kutokana na hisia na matamanio tu ya mashabiki wafia timu.

Tatu, sio kila maamuzi mabovu yangeweza kuleta matokeo tofauti ya mwisho ya mchezo.

Nne, kwenye mechi moja maamuzi mabovu yanaweza kufanyika pande zote na hivyo kuziathiri pande zote sawia. Mfano, Timu moja inaweza kunyimwa penalty au red card sahihi na timu nyingine ikakataliwa goli sahihi.

Tano, Inconvenience nalo ni jambo la msingi sana kuangaliwa kwa sababu kama kwenye ligi utahitaji kurudia mechi tatu kutokana na makosa ya uchezesaji ina maana unavuruga utaratibu mzima wa ligi.

Sita, Hata kama kulikuwa na makosa ya refa katika mechi kwa nini yaiathiri timu iliyofaidika nayo kwa kurudia mechi na wakati haikuhusika, haikumshawishi au kumtuma refa huyo kufanya hayo makosa.

Saba, Hakuna mechi inaweza kuchezwa bila refa kutofanya makosa, makosa ya kibinadamu ni sehemu ya mchezo, yanafanywa na wachezaji pamoja na marefa pia. Muhimu isiwe ni upangaji wa matokeo.
 
Duh aisee watu mko vizuri kichwani Safi sana nimekupa salute umenishawishi japo mimi ni yanga damu damu mwananchi
 
Yaani wana Yanga bado hamjatoka Tu usingizini......bado mnaiota nusu fainali.........

Mungu amuhifadhi sana Yule refa.... katuepusha na mengi sana
 
Hata hivyo, leo hii Simba hamna tena la kutuambia maana tulikuwa tunaingia nusu hatua ambayo kwenu imekuwa ngumu kwa misimu mitano mfululizo.

Pia, tukio hili limefunika kabisa matokeo mabovu ya Simba ya kupigwa ndani nje, vinginevyo tungewaponda sana huku tukiwa teyari tumetinga nusu fainali.

Huyu Refa katukatili sana.
 
Huy Refa katukatili sana.
Hahahaaa!!

Mimi furaha yangu ni Yanga kutolewa tu
 
Refa ametukosea sana Wananchi.
 
Attachments

  • 5682167-4b4fb6a42c070f3306c0f595187ea8a-1.mp4
    3.1 MB
Kwanza, Kwenye mechi, sio refa peke yake anaamua, kuna wasaidizi washika vibendera wa pembeni na nyakati hizi kuna hadi VAR.

Pili, kinachoitwa maamuzi mabovu ya refa wakati mwingine ni kutokana na hisia na matamanio tu ya mashabiki wafia timu.

Tatu, sio kila maamuzi mabovu yangeweza kuleta matokeo tofauti ya mwisho ya mchezo.

Nne, kwenye mechi moja maamuzi mabovu yanaweza kufanyika pande zote na hivyo kuziathiri pande zote sawia. Mfano, Timu moja inaweza kunyimwa penalty au red card sahihi na timu nyingine ikakataliwa goli sahihi.

Tano, Inconvenience nalo ni jambo la msingi sana kuangaliwa kwa sababu kama kwenye ligi utahitaji kurudia mechi tatu kutokana na makosa ya uchezesaji ina maana unavuruga utaratibu mzima wa ligi.

Sita, Hata kama kulikuwa na makosa ya refa katika mechi kwa nini yaiathiri timu iliyofaidika nayo kwa kurudia mechi na wakati haikuhusika, haikumshawishi au kumtuma refa huyo kufanya hayo makosa.

Saba, Hakuna mechi inaweza kuchezwa bila refa kutofanya makosa, makosa ya kibinadamu ni sehemu ya mchezo, yanafanywa na wachezaji pamoja na marefa pia. Muhimu isiwe ni upangaji wa matokeo.
Mueleweshe huyu mfia yanga.
 
Mleta mada hakuitaja Yanga. Kwanini sisi tunashindwa kujadili mada? Kumbuka makosa haya yanaweza kuipata timu yoyote ile kama hakutakuwa na maboresho.
 
Kwanza, Kwenye mechi, sio refa peke yake anaamua, kuna wasaidizi washika vibendera wa pembeni na nyakati hizi kuna hadi VAR.

Pili, kinachoitwa maamuzi mabovu ya refa wakati mwingine ni kutokana na hisia na matamanio tu ya mashabiki wafia timu.

Tatu, sio kila maamuzi mabovu yangeweza kuleta matokeo tofauti ya mwisho ya mchezo.

Nne, kwenye mechi moja maamuzi mabovu yanaweza kufanyika pande zote na hivyo kuziathiri pande zote sawia. Mfano, Timu moja inaweza kunyimwa penalty au red card sahihi na timu nyingine ikakataliwa goli sahihi.

Tano, Inconvenience nalo ni jambo la msingi sana kuangaliwa kwa sababu kama kwenye ligi utahitaji kurudia mechi tatu kutokana na makosa ya uchezesaji ina maana unavuruga utaratibu mzima wa ligi.

Sita, Hata kama kulikuwa na makosa ya refa katika mechi kwa nini yaiathiri timu iliyofaidika nayo kwa kurudia mechi na wakati haikuhusika, haikumshawishi au kumtuma refa huyo kufanya hayo makosa.

Saba, Hakuna mechi inaweza kuchezwa bila refa kutofanya makosa, makosa ya kibinadamu ni sehemu ya mchezo, yanafanywa na wachezaji pamoja na marefa pia. Muhimu isiwe ni upangaji wa matokeo.
Umemalizaa kila kitu.
 
eti upangaji wa matokeo unaufaham vizur upangaji wa matoke kijana au kweny maisha yak ya soka umewah shuduia upangaji wa matokeo nafikili kawaulize viongozi wa juve wakupe majibu upangaji wa matokeo upuje
 
Zamani ni Tanzania tu walikuwa utopolo wenye akili ni wawili Ila Sasa hivi Afrika na dunia wameshajua Kuna timu imejaza wajinga.
Mlipotolewa fainali mkaanza kudai kanuni zibadilishwe kuhusu magoli ya mechi za nyumbani na ugenini.
Sasa hivi mnataka Sheria zibadilishwe kwa kuhisi mmeonewa kimaamuzi.
Hakuna timu Tanzania iliyonufaika na maamuzi mabovu Kama yanga. Kama hizo Sheria zingekuwepo mwaka Jana msingekuwa mabingwa na hata mwaka huu msingekuwa kileleni.
Kama kulikuwa na maamuzi mabovu yaliyowanufaisha. na hamkulalamika Sheria zibadilishwe kwanini mnalalamika Sasa.
 
Kwa kusema kweli wana yanga wote tumeumia sana lakini hatuna budi kuganga yajayo, kikubwa tumejifunza baadhi ya vitu. Kwanza hatuna streika katili pale mbele(one chance one goal), pili game za mtoano tunatakiwa kuzimaliza uwanja wa nyumbani.
Kuzimaliza nyumbani Kwa kushika bomba dakika 90+
 
Back
Top Bottom